
Msanii maarufu wa muziki wa Hip Hop nchini Uganda, Gravity Omutujju, amezua gumzo mitandaoni baada ya kukiri wazi kuwa ana hisia za kimapenzi kwa Zuena Kirema, mke wa mwanamuziki mashuhuri Bebe Cool.
Katika mahojiano na TikToker mmoja maarufu, Gravity alifunguka kwa mara ya kwanza kuhusu hisia zake kwa Zuena, akieleza kuwa amekuwa na “crush” naye kwa muda mrefu, na licha ya ndoa ya Zuena na Bebe Cool kuwa imara, bado anampenda kisiri.
“Sijawahi kumuambia lakini ukweli ni kwamba nina ‘crush’ naye. Ni mwanamke mrembo sana, na hata kama ameolewa, siwezi kuficha hisia zangu,” alisema Gravity kwa ucheshi.
Zuena Kirema, ambaye ameolewa na Bebe Cool kwa zaidi ya muongo mmoja na wana watoto pamoja, hajatoa tamko lolote kuhusu kauli hiyo ya Gravity. Bebe Cool pia hajaonekana kuguswa moja kwa moja na taarifa hiyo, ingawa mashabiki wake wengi wameonyesha mshtuko na wengine kuchukulia kama mzaha wa kawaida wa mastaa.