Entertainment

Jeezy Adai Jay Z Alimtoa Kwenye Wimbo wa Beyoncé

Jeezy Adai Jay Z Alimtoa Kwenye Wimbo wa Beyoncé

Rapa kutoka Marekani, Jeezy, amefunguka kuhusu tukio lililomkuta nyuma ya pazia la utengenezaji wa wimbo maarufu wa Beyoncé “Drunk In Love”. Jeezy ameeleza kuwa awali alikuwa sehemu ya mradi huo, tayari akiwa ameandika verse yake kwa ajili ya kushiriki kwenye wimbo huo, lakini mambo yalibadilika ghafla.

Kwa mujibu wa Jeezy, baada ya maandalizi ya awali kukamilika, alipokea taarifa kutoka kwa Jay Z akielezwa kuwa hatakuwa tena kwenye wimbo huo, na kwamba Jay Z mwenyewe ndiye atakayeshirikiana na Beyoncé kwenye ngoma hiyo.

Kauli hiyo imeibua mjadala mkubwa mtandaoni huku mashabiki na wachambuzi wa muziki wakigawanyika. Wapo wanaodai huenda verse ya Jeezy haikuwa na mvuto wa kutosha, jambo lililomfanya Jay Z kuchukua nafasi hiyo. Hata hivyo, wengine wanaamini verse ya Jeezy ilikuwa kali kupita kiasi, hali iliyoweza kumfanya Jay Z kuhofia Jeezy angefika mbali zaidi kupitia wimbo huo.

Aidha, baadhi ya wapenzi wa muziki wameenda mbali zaidi kwa kusema kuwa verse ya Jay Z kwenye Drunk In Love haikuwa kali sana, na huenda ingekuwa busara zaidi kumuacha Jeezy ashiriki.