Gossip

Khadija Kopa Akiri Kumkingia Kifua Diamond Anapogombana na Zuchu

Khadija Kopa Akiri Kumkingia Kifua Diamond Anapogombana na Zuchu

Malkia wa muziki wa Taarab, Khadija Kopa, amefunguka kuhusu uhusiano wake na mkwe wake Diamond Platnumz, akisema huwa anamkingia kifua kila mara anapokuwa na mgogoro na binti yake Zuchu.

Akipiga stori na Juma Lokole, Kopa amesema huwa upande wa Diamond kwa sababu anamchukulia kama mwanae wa sasa na hataki kuvuruga ndoa yao.

Amesema kuwa alianza kumpenda Diamond hata kabla hajaingia katika mahusiano ya kimapenzi na Zuchu, kutokana na heshima na bidii yake katika kazi ya muziki.

Mwanamama huyo ameeleza pia kama mzazi, ni wajibu wake kuhakikisha amani na upendo vinatawala katika familia, hivyo anapochagua kumtetea Diamond, anafanya hivyo kwa nia njema ya kulinda ndoa ya mtoto wake.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *