Entertainment

Khaligraph Jones Aomba Radhi Baada ya Video ya Usipime Kuzua Utata

Khaligraph Jones Aomba Radhi Baada ya Video ya Usipime Kuzua Utata

Rapa Khaligraph Jones, ameomba radhi mashabiki wake baada ya kuzua gumzo mtandaoni kufuatia kuonekana akirusha noti za dola katika video ya wimbo wake mpya uitwao Usipime.

Kupitia ujumbe alioutoa, Khaligraph Jones amesema kuwa dola zilizotumika kwenye video hiyo ni prop money maalum kwa ajili ya shooting za video na filamu, na sio pesa halisi.

Papa Jones, amesisitiza kuwa hana uwezo wa kugawa pesa kama ambavyo baadhi ya mashabiki walivyodhani, na akawataka waache kumuomba pesa.

Kauli yake imekuja mara baada ya kipande cha video wa wimbo wake mpya kusambaa akirusha pesa, kitendo kilichowafanya mashabiki wengi kuanza kumuomba pesa, wakiamini kuwa fedha alizokuwa akirusha ni za kweli.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *