Msanii nyota wa muziki barani Afrika, Diamond Platnumz, ametoa kauli inayotafsiriwa na wengi kama utabiri mzuri kwa mustakabali wa binti yake, Tiffah Dangote.
Kupitia ukurasa wa Instagram wa Tiffah, Diamond amejibu posti ya binti yake aliyokuwa akielezea nafasi yake katika familia yao kwa maneno mafupi lakini yenye uzito mkubwa akimuita “My Miss World”
Kauli hiyo ya Diamond imechukuliwa na mashabiki kama ishara ya matumaini na utabiri mzuri kwa binti huyo, wengi wakiamini kuwa Tiffah ana kila sifa ya kuwa nyota mkubwa siku za usoni, ikiwemo kufikia mafanikio makubwa kama kushiriki mashindano ya kimataifa kama Miss World.
Mashabiki wamehusisha kauli hiyo na malezi pamoja na mazingira ya kifamilia anayokulia Tiffah, wakiamini kuwa upendo na sapoti anayopata kutoka kwa baba yake vinaweza kumjenga kuwa kiongozi au nyota mkubwa wa baadaye, ikiwemo kufikia ndoto kubwa kama kushiriki mashindano ya kimataifa ya urembo kama Miss Dunia.