Others

Khaligraph Jones Avaa Kinyago cha Alien Kutangaza Wimbo Mpya na Johny Vigeti

Khaligraph Jones Avaa Kinyago cha Alien Kutangaza Wimbo Mpya na Johny Vigeti

Rapa wa Kenya Khaligraph Jones amewasisimua mashabiki wake baada ya kujitokeza hadharani akiwa amevaa kinyago inayofanana na kiumbe wa anga (alien) huku akitangaza ujio wa wimbo wake mpya.

Kupitia ujumbe aliouchapisha mtandaoni, Khaligraph amefichua kuwa anajiandaa kuachia wimbo mpya akishirikiana na rapa mwenzake Johny Vigeti. Kulingana na tangazo hilo, wimbo huo unatarajiwa kutoka rasmi tarehe 11 Machi.

Khaligraph amesema kuwa mashabiki wanapaswa kujiandaa kwani kazi hiyo itakuwa kali na yenye ushindani mkubwa wa kimuziki. Amesisitiza kuwa ushirikiano huo na Vigeti umeandaliwa kwa ubora mkubwa ili kuwapa wapenzi wa muziki wa hip hop ladha tofauti.

Kwa sasa, mashabiki wanasubiri kwa hamu kusikia matokeo ya muunganiko huo wa wasanii wawili wanaoheshimika katika tasnia ya rap nchini Kenya. Wengi wanaamini wimbo huo unaweza kuwa moja ya nyimbo zitakazotikisa majukwaa ya muziki mara tu utakapozinduliwa.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *