Entertainment

Pipi Jojo: Ningepoteza Career au Mzazi Ningeendelea na Chief Godlove

Pipi Jojo: Ningepoteza Career au Mzazi Ningeendelea na Chief Godlove

Msanii wa muziki wa Bongoflava, Pipi Jojo, ameweka wazi sababu iliyomfanya kuachana na meneja wake wa zamani, Chief Godlove, akisema kuwa kuendelea kufanya kazi pamoja kungemlazimu kupoteza moja kati ya mambo mawili muhimu maishani mwake.

Akizungumza baada ya kutemana na meneja huyo ambaye kwa muda mrefu amekuwa akisimamia masuala ya muziki wake, Pipi Jojo amesema kuwa hali iliyokuwa ikijitokeza ingemweka katika nafasi ngumu ya kuchagua kati ya kuendeleza taaluma yake ya muziki au kulinda mahusiano yake ya kifamilia.

Kwa mujibu wa msanii huyo, aliona ni busara kuchukua hatua mapema ili kuepuka athari ambazo zingeharibu mustakabali wake binafsi na wa kikazi.

Hata hivyo, Pipi Jojo ambaye alikuwa akipiga stori na Clouds FM, hakuweka wazi kwa undani kile kilichosababisha mgogoro huo, bali amesisitiza kuwa uamuzi huo ulilenga kulinda maisha yake ya baadaye pamoja na uhusiano wake na familia.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *