Malkia wa TikTok nchini Kenya, Azziaad Nasenya, ametoa wito kwa wasanii wa Kenya kuungana na kutengeneza wimbo wa pamoja wa kumuenzi marehemu Raila Odinga.
Kupitia ujumbe kwenye ukurasa wake wa Instagram, Azziaad amewataka mastaa kama Khaligraph Jones, Okello Max, Prince Indah, na Bahati kuingia studio na kutoa wimbo wa pamoja wa kuomboleza kifo cha kiongozi huyo mashuhuri wa kisiasa.
Azziaad amesema huu ni wakati mzuri kwa sekta ya muziki kuonyesha umoja na uzalendo, ikizingatiwa nafasi kubwa ambayo Raila alikuwa nayo katika historia ya taifa hilo. Mrembo huyo amewahimiza wasanii hao kukamilisha wimbo huo kabla ya mwisho wa siku kama ishara ya heshima kwa kiongozi huyo aliyeacha alama kubwa kwa vizazi vingi.
Kwa sasa, wasanii kadhaa akiwemo Bahati, Akothee na Prince Indah tayari wameachia nyimbo zao maalum za kumuomboleza Raila, huku mashabiki wakisifia juhudi zao za kuonyesha upendo na heshima kwa mwanasiasa huyo mkongwe.