Entertainment

Mama Fina amkingia kifua mwimbaji wa Kadongo Kamu Hassan Nduga kwa tuhuma za wizi

Mama Fina amkingia kifua mwimbaji wa Kadongo Kamu Hassan Nduga kwa tuhuma za wizi

Mganga wa kienyeji kutoka nchini Uganda Mama Fina ameamua kumkingia kifua mwimbaji wa Kadongo Kamu Hassan Nduga baada ya kutuhumiwa kuhusika kwenye wizi wa pesa za kugharamia matibabu ya msanii Ronald Alimpa aliyehusika kwenye ajali mbaya ya barabarani wiki iliyopita.

Mama Fina amenyosha maelezo kwa kusema kuwa hakumpa Hassan Nduga pesa za Ronald Alimpa kama inavyodaiwa bali alitoa shillingi laki 5 za kugharamia matibabu ya msanii huyo na akampa mama yake mzazi.

Mwanamama huyo amesisitiza kuwa bado anaendelea kumtumia pesa za mahitaji ya msingi msanii huyo ambaye bado anauguza majeraha mabaya ya ajali.

Kauli ya Mama Fina inakuja baada ya familia ya Ronald Alimpa kumchafulia jina Hassan Nduga kwa madai ya wizi wa shillingi laki 5 za kugharamia matibabu ya hitmaker huyo wa “Seen Don” alizopewa na mama Fina.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *