Entertainment

Msanii Diamond Afunguka Kuhusu Kipaji Chake cha Kuandika Mashairi

Msanii Diamond Afunguka Kuhusu Kipaji Chake cha Kuandika Mashairi

Msanii nguli wa muziki wa Bongo Fleva, Diamond Platnumz, amefunguka wazi kuhusu kipaji chake cha kipekee katika uandishi wa nyimbo, akieleza kuwa hiyo ndiyo silaha yake kubwa katika mafanikio ya muziki wake.

Kupitia mahojiano ya hivi karibuni, Diamond amesema ubora wake unajengwa zaidi na uwezo wake wa kuandika mashairi yenye hisia na ujumbe mzito, jambo ambalo limechangia kwa kiasi kikubwa kupendwa na mashabiki ndani na nje ya Tanzania.

“Watu wengi wanajua tu napiga shoo, naimba, lakini ukweli ni kwamba uandishi wa mashairi ndiyo silaha yangu kubwa. Hapo ndipo nguvu yangu ipo,” amesema Diamond.

Ameeleza kuwa mbali na nyimbo zake binafsi, amekuwa akiandika pia nyimbo kwa wasanii wengine, hususan wale walioko chini ya lebo yake ya WCB Wasafi, lakini pia amewahi kusaidia wasanii wa nje ya lebo hiyo. Hata hivyo, hakutaja majina ya wasanii au nyimbo alizohusika nazo, lakini amesisitiza kwamba mchango wake katika uandishi wa nyimbo umechangia mafanikio ya wengi kwenye tasnia.

Kauli hiyo inazidi kuthibitisha nafasi yake kama mmoja wa wasanii waandamizi na wabunifu zaidi katika muziki wa Afrika Mashariki, huku akiendelea kushika nafasi ya juu kwenye chati mbalimbali za muziki barani Afrika.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *