
Msanii maarufu wa muziki wa Kenya, Nadia Mukami, amefichua kwamba yeye na mchumba wake, Arrow Bwoy, walilazimika kuahirisha harusi yao baada ya kugundua kwamba walikuwa wanatarajia mtoto wao wa pili.
Kupitia mahojiano ya hivi karibuni, Nadia ambaye anafanya vizuri na ngoma yake mpya ‘Overdose’ alieleza kuwa walikuwa tayari wameweka mikakati yote muhimu kwa ajili ya tukio hilo maalum, lakini ujio wa mtoto mpya uliwalazimu kuahirisha harusi hiyo.
“Tulikuwa tumepanga kila kitu, lakini sasa tumelazimika kuifuta,” alisema Nadia kwa huzuni lakini pia kwa matumaini.
Ingawa mashabiki wengi walikuwa na matarajio makubwa ya kushuhudia harusi hiyo ya wanamuziki wawili maarufu, Nadia alisisitiza kuwa afya na ustawi wa familia yao ni jambo la kipaumbele kwa sasa. Hata hivyo, hakufunga mlango wa uwezekano wa harusi hiyo kufanyika siku za usoni
Nadia na Arrow Bwoy, ambao walimpokea mtoto wao wa kwanza mwaka wa 2022, wamekuwa wakiendelea kudumisha uhusiano wao wa kimapenzi hadharani huku wakishirikiana pia katika kazi za muziki.