Entertainment

Bien Akanusha Kuvunjika kwa Kundi la Sauti Sol

Bien Akanusha Kuvunjika kwa Kundi la Sauti Sol

Mwanamuziki Bien-Aimé Baraza ameweka wazi msimamo wa kundi la Sauti Sol kufuatia madai yanayoendelea mtandaoni kwamba wamevunja rasmi ushirikiano wao wa muda mrefu.

Akizungumza kuhusu tetesi hizo kwenye runinga ya Citizen, Bien amesisitiza kuwa kundi hilo halijawahi kuachana, na kwamba walitangaza tu kuchukua mapumziko ya muda.

Kwa mujibu wa Bien, uhusiano kati ya wanachama wa Sauti Sol bado ni mzuri na hakuna mgogoro unaotishia mustakabali wa urafiki wao au kazi yao ya pamoja. Ameeleza kuwa mapumziko hayo yanalenga kuwapa nafasi ya kujikita katika miradi binafsi bila shinikizo, huku wakidumisha utambulisho wao kama kundi.

Hata hivyo, Bien amewatoa hofu, akisisitiza kuwa mapumziko hayo si mwisho wa safari yao ya pamoja, bali njia ya kukuza uwezo wao binafsi na kurudi wakiwa na nguvu mpya.

Kauli zake zimekuja wakati mashabiki wengine wakitaka ufafanuzi kuhusu hatma ya Sauti Sol, hasa baada ya wanachama wa kundi hilo kuendelea kushughulika zaidi na miradi ya kibinafsi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *