Rapa wa Marekani, Cardi B, amewatuliza wananchi wa Saudi Arabia baada ya mjadala mtandaoni kuhusu maadili na sheria za nchi hiyo kabla ya ziara yake inayotarajiwa kufanyika mwishoni mwa mwaka huu jijini Riyadh.
Katika mazungumzo yake kupitia Insta Live, Cardi B amesisitiza kuwa atatii kikamilifu sheria na taratibu zote za Saudi Arabia pindi atakapowasili kwa ajili ya onyesho lake.
Pia amebainisha kuwa hana tabia ya kutumia pombe na anajitambua kama mwanamke mwenye maadili, hivyo hana sababu ya kwenda kinyume na kanuni za nchi hiyo.
Cardi B anatarajiwa kutumbuiza kwenye moja ya matamasha makubwa ya mwisho wa mwaka, hafla inayotarajia kuvutia mastaa mbalimbali wa kimataifa.