Entertainment

RAYVANNY ATANGAZA TAREHE RASMI YA KUACHIA FLOWERS II EP

RAYVANNY ATANGAZA TAREHE RASMI YA KUACHIA FLOWERS II EP

CEO wa Next Level Music na Member wa WcB msanii Rayvanny ameachia Track list ya , EP  yake iitwayo Flowers II’.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram Rayvanny ameshare artwork ya EP hiyo yenye Jumla ya Nyimbo 9 za moto ambapo amesema itaingia rasmi Sokoni Februari 10, mwaka wa 2022.

Kwenye Followers II EP Rayvanny amewashirikisha wasanii kama Zuchu, Roki, Nadia Mukami, Marioo, na Ray C huku akisema kuwa EP hiyo ni zawadi maalum kwa ajili ya siku ya wapenda nao, Valentine’s day.

EP hiyo itakuwa kama muendelezo wa EP yake ya kwanza ya Flowers iliyotoka mwanzoni mwa mwaka wa 2021 ikiwa na jumla ya nyimbo 8 ikiwemo HitSong yake ya “Teamo”

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *