Entertainment

SHATTA WALE AMVUA NGUO BURNA BOY, ATOA MATUSI MAZITO

SHATTA WALE AMVUA NGUO BURNA BOY, ATOA MATUSI MAZITO

Bifu la Shatta Wale wa Ghana na Burna Boy wa Nigeria linaendelea kushika kasi, Shatta Wale ameibuka na kuweka wazi kuwa yupo tayari kuingia ulingoni na African giant, Burna Boy.

Kupitia mfululizo wa tweets za matusi katika mtandao wa Twitter  Shatta Wale alionekana mwenye hasira huku akitoa vitisho kwa Burna Boy asikanyaga kwenye ardhi ya Ghana kwani atamshushia kichapo cha mbwa kitakachoimuacha na majeraha.

Shatta ametoa kauli hiyo mara baada ya Burna Boy kudai kuwa hatomvumilia msanii yeyote anayetaka kuigawanya tasnia ya muziki Afrika ambapo alienda mbali zaidi na kusema kwamba yupo tayari kuzichapa na Shatta Wale ambaye juzi kati amekuwa akiwashambulia mashabiki na wasanii wa Nigeria kwa kutosapoti muziki wa mataifa mengine ya Afrika.

Hata hivyo Burna Boy hajajibu chochote mpaka sasa kuhusiana na ishu ya Shatta Wale kumtolea uvivu

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *