
Mkali wa muziki wa Hiphop Duniani Snoop Dogg amethibitisha ujio wa Album yake mpya “Missionary” ambayo imetayarishwa na swahiba wake wa muda mrefu, Mtayarishaji mkongwe Dr. Dre.
Snoop amefunguka hayo kupitia podcast ya ‘Know Mercy’ na Mtangazaji Stephen A. Smith, ambapo amesema Album hiyo ipo jikoni inapikwa kwa sasa.
Kwa mujibu wa Snoop ‘Missionary’ itatoka chini ya Death Row Records/Aftermath Entertainment. Album ya kwanza ya Snoop Dogg ilikuwa inaitwa ‘Doggystyle’ na ilitoka November mwaka 1993 ikitengenezwa na Dr. Dre.