AKOTHEE KUFUNGULIWA MASHTAKA KWA TUHUMA YA KUMTELEKEZA MFANYIKAZI WAKE

AKOTHEE KUFUNGULIWA MASHTAKA KWA TUHUMA YA KUMTELEKEZA MFANYIKAZI WAKE

Siku chache baada ya Mwanamitido wa urembo nchini  Dennis Karuri kudai Akothee ndiye mteja mkorofi zaidi kuwahi kufanya naye kazi, shutuma nyingine imeibuliwa dhidi ya mwanamuziki huyo. Mfanyakazi wake wa zamani aliyefahamika kwa jina la Brenda amejitokeza na kudai kuwa Akothee amekataa kumlipa mshahara wake wa shillingi Sh60,000 licha ya kumfanyia kazi ya kushoot video kwenye shughuli zake kwa miezi miwili. Brenda amemtaja akothee kama mtu katili asiyekuwa na uhuruma  ambapo ametishia kumchukulia hatua kali za kisheria msanii huyo kwa kutothamini kazi aliyomfanyia. Hata hivyo, akothee amejibu tuhuma hizo kwa kusema kuwa  mlalamishi alifeli kutekeleza majukumu yake ipasavyo, hivyo hangelipwa kwa kazi ambayo hakufanya huku akitishia kumchukulia Brenda hatua za kisheria akisema hatakubali jina lake lichafuliwa na mtu yeyote.

Read More
 AKOTHEE AJIBU SHTUMA ZA KUDHARAU KAZI YA MWANAMITINDO WA UREMBO NCHINI DENNIS KARURI

AKOTHEE AJIBU SHTUMA ZA KUDHARAU KAZI YA MWANAMITINDO WA UREMBO NCHINI DENNIS KARURI

Msaniii nyota nchini Akothee amemjibu mwanamitindo wa urembo nchini Dennis Karuri aliyedai kuwa msanii huyo ndiye mteja mkorofi zaidi kuwahi kumhudumia tangu aanza kujishughulisha na maswala ya urembo. Kupitia ukurasa wake wa instagram Akothee amesema hana muda kupishana na watu wanaotafuta kiki wakitumia jina lake kwani nguvu zake zote amezielekeza kwenye ishu ya kuiweka afya yake sawa ikizingatiwa kuwa hajakuwa sawa kiafya siku za hivi karibuni. Hitmaker huyo wa “Sweet Love” amewataka waache kumhusisha kwenye shughuli zao kwani amechoshwa kuzushiwa tuhuma za uongo ambazo amesema huenda ndizo zimempelekea kulazwa hospitali katika nyakati tofauti. Kauli ya Akothee imekuja siku chache baada ya Dennis Karuri kwenye podcast ya Obinna kunukuliwa akisema kuwa kuna kipindi alimremba akothee lakini msanii huyo alimkatisha tamaa alipomuambia bidhaa zake za make up ni vumbi kwani zilimtoa vibaya.

Read More
 AKOTHEE AJUTA  KUWA MTU MAARUFU, ASEMA UMAARUFU UNAMTESA

AKOTHEE AJUTA KUWA MTU MAARUFU, ASEMA UMAARUFU UNAMTESA

Msanii na mfanyibiashara maarufu nchini Akothee amefunguka changamoto za kuwa mtu maarufu. Kupitia waraka mrefu aliouchapisha kwenye ukurasa wake wa Instagram Akothee amesema anajutia kuwa maarufu kwani anapata wakati mgumu sana kufurahia maisha yake ya faraghani kama watu wengine kwani mashabiki wamekuwa wakimrekodi kwa siri akiwa na familia yake maeneo  ya umma. Hitmaker huyo “Sweet Love” ameeleza kuwa kuna kipindi karibu warushiane makonde na shabiki yake mmoja ambaye alimshika akiwa anamrekodi kwa siri na familia yake. Hata hivyo amewaomba mashabiki zake wasiwe na mazoea ya kutaka kupiga nae picha akiwa maeneo ya umma kwani amechoshwa na tabia ya watu kuingilia maisha yake.

Read More
 AKOTHEE AKANUSHA TAARIFA ZA KUZUSHIWA KIFO MTANDAONI

AKOTHEE AKANUSHA TAARIFA ZA KUZUSHIWA KIFO MTANDAONI

Msanii wa muziki nchini Akothee amekanusha taarifa za kifo ambazo zilianza kusambaa mitandaoni mapema wiki hii. Kupitia ukurasa wake wa instagram Akothee ameandika ujumbe kuwatoa hofu mashabiki zake kwa kusema kwamba amesikitishwa na kitendo cha kuzushiwa kifo wakati bado yupo hai. R.I.P ? 🤔 Msilazimishia kifo kabla wakjati wangu haujafika. Sijachukua nafasi yako kwa hii dunia. 🙏 Acheni kuandika R.I.P mapema hivi . Nipo hai na Mungu ana sababu ya kuona siku nyingine. Hata nikifa leo hakuna mtu atachukua nafasi yangu…Akothee ameandika kupitia Instagram yake. Hitmaker huyo wa “Sweet Love “amesema yeye ni mzima wa afya na hata ugonjwa ambao ulikuwa ukimsumbua kwa muda sasa ameshapona. Ikumbukwe Akothee amekuwa akisumbuliwa na ugonjwa ambao hakuwa wazi kwa muda muda sasa jambo ambalo limepelekea baadhi ya watumiaji wa mitandao ya kijamii kumzushia kifo

Read More
 AKOTHEE ALAZWA HOSPITALI BAADA YA KUUGUA GHAFLA

AKOTHEE ALAZWA HOSPITALI BAADA YA KUUGUA GHAFLA

Staa wa muziki ambaye pia ni mfanyabiashara nchini Akothee amelazwa hospitali kwa mara nyingine mara baada ya kuugua ghafla. Akothee ameweka wazi hilo kupitia ukurasa wake wa Instagram kwa kusema kwamba alikimbizwa hospitali Disemba 11 alipougua ghafla nyumbani kwake. Hitmaker huyo wa “Sweet Love”  amesema ameshindwa kubaini maradhi yanayomsibu ila kwa sasa ni mwingi wa shukrani kwani ameanza kupata afueni. Bosi huyo wa Akothee Safaris ametambua mchango wa mpenzi wake Nelly Oaks ambaye amesimama nae mara tano hospitali alipokuwa amelazwa hospitalini. Wiki iliyopita binti yake Rue Baby alilazimika kuahirisha hafla ya kufuzu kwake kutoka chuo kikuu baada ya Akothee kulazwa tena hospitalini.

Read More
 AKOTHEE AREJEA TENA KEMPINSIKI BAADA YA KUUSUTA VIKALI UONGOZI WAKE

AKOTHEE AREJEA TENA KEMPINSIKI BAADA YA KUUSUTA VIKALI UONGOZI WAKE

Nyota wa muziki nchini Akothee amerejea tena katika hoteli ya kifahara ya Kempinski,ikiwa ni wiki mbili imepita baada ya kuhapa kutokanyaga kwenye hoteli hiyo. Hatua hiyo ya Akothee imeonekana kuwakera wakenya kwenye mitandao ya kijamii wengi wakisema msanii huyo ni mnafiki na kauli  chafu aliyoitoa juu ya hoteli ya Kempinski haiwezi haribu brand ya hoteli hiyo. Akothee alikuwa anahudhuria hafla ya kusherekea mafanikio ambayo kinara wa ODM Raila Odinga ameiletea taifa la Kenya wikiendi hii iliyopita. Ikumbukwe wiki kadhaa zilizopita Akothee aliichana hoteli ya kifahari ya Kempinski iliyoko jijini Nairobi kwa madai ya kuwa na uongozi mbaya kwani mameneja wa hoteli hiyo walimsumbua sana kipindi anasherekea mwaka mmoja wa kuzinduliwa kwa wakfu wake wa Akothee Foundation katika hoteli hiyo.

Read More