Ali Kiba Afunguka Suala la Mashabiki Kuwakataa Wasanii

Ali Kiba Afunguka Suala la Mashabiki Kuwakataa Wasanii

Staa wa muziki wa Bongo Fleva, Ali Kiba, amfafanua msimamo wake kuhusu mjadala unaotikisa tasnia ya muziki nchini Tanzania, ambapo baadhi ya mashabiki wameamua kuwakataa wasanii kwa kujihusisha na kampeni za kisiasa, hasa katika uchaguzi uliopita uliokumbwa na utata. Akizungumza kuhusu hali hiyo, Ali Kiba amesema hakuna mtu aliyefurahia kilichotokea kwenye uchaguzi huo, akibainisha kuwa mazingira yalikuwa magumu kwa kila upande. Hitmaker huyo wa Sella, amesema wasanii hawakuwa na nia ya kuwaumiza au kuwakwaza mashabiki wao, bali wengi wao walikuwa wanatafuta riziki na fursa za kujiendeleza kimaisha. Hata hivyo, Ali Kiba amesema mwitikio wa mashabiki umekuwa somo kubwa kwa wasanii, akieleza kuwa ni jambo jema mashabiki kufungua mioyo yao na kusema wazi maneno yote ya chuki na maumivu waliyonayo, badala ya kuyaficha.

Read More
 Mrembo wa Kenya Akiri Kuvutiwa na Alikiba, Atangaza Yuko Tayari kwa Date

Mrembo wa Kenya Akiri Kuvutiwa na Alikiba, Atangaza Yuko Tayari kwa Date

Mrembo mmoja kutoka Kenya amezua gumzo mtandaoni baada ya kukiri waziwazi kuwa amevutiwa kimahaba na nyota wa muziki kutoka Tanzania, Alikiba, na kueleza kuwa yuko tayari kutoka naye endapo atapata nafasi hiyo. Akizungumza kupitia mitandao ya kijamii, mrembo huyo amesema hana majuto yoyote kuhusu hisia zake, akisisitiza kuwa anampenda kwa dhati staa huyo wa wimbo Sella anayependwa kote Afrika Mashariki. Kwa mujibu wake, amekuwa akijaribu kwa muda mrefu kupata nafasi ya kukutana na Alikiba ana kwa ana, lakini juhudi hizo zimekuwa zikigonga mwamba. Ameongeza kuwa mapenzi yake kwa mwanamuziki huyo yamezidi nguvu kiasi cha kushindwa kuvumilia zaidi na kuamua kuweka hisia zake wazi hadharani. Alikiba alikuwa nchini Kenya wikiendi iliyopita, ambapo alitoa burudani ya kipekee katika tamasha maalum la kumuenzi hayati Raila Odinga, lililowaleta pamoja mashabiki wengi na wadau wa muziki kutoka pande zote za Afrika Mashariki.

Read More
 Alikiba Kutumia Show Yake Nchini Kenya Kumuenzi Raila Odinga

Alikiba Kutumia Show Yake Nchini Kenya Kumuenzi Raila Odinga

Msanii wa muziki wa hip hop nchini Kenya, Octopizzo, ameingia katika majonzi kufuatia kifo cha meneja wake na rafiki wa muda mrefu, Ongaya Vick, anayefahamika pia kwa jina la Cheeks Zone. Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Octopizzo ameeleza huzuni yake kuu akitangaza msiba huo, akisema Ongaya hakuwa tu meneja bali pia alikuwa mtu aliyemwamini na kumtia moyo tangu mwanzo wa safari yake ya muziki. Kwa mujibu wa Octopizzo, Ongaya ndiye alikuwa mtu wa kwanza kuona uwezo wake wakati wengi walikuwa na mashaka kama muziki wa rap ungeweza kumtoa kisanaa. Amesema tangu mwaka 2009, Ongaya amekuwa nguzo kuu ya ubunifu nyuma ya chapa ya Octopizzo, akisaidia kuijenga hadi kufikia mafanikio ya kimataifa. Rapa huyo ameeleza kuwa imani na maono ya marehemu yalimsaidia si tu katika taaluma yake ya muziki, bali pia kumfanya kuwa mtu bora zaidi maishani. Kwa sasa, marafiki na jamaa wanakusanyika katika makazi ya familia ya Ongaya eneo la Woodley, Nairobi, kwa maandalizi ya mazishi. Marehemu anatarajiwa kuzikwa nyumbani kwake Kakamega, ambako familia itamkumbuka kama mtu mwenye moyo wa upendo, ubunifu, na uongozi.

Read More
 Wasanii wa Bongo Fleva Watoa Salamu za Pole kwa Familia ya Raila Odinga na Wakenya

Wasanii wa Bongo Fleva Watoa Salamu za Pole kwa Familia ya Raila Odinga na Wakenya

Msiba wa Waziri Mkuu wa zamani wa Kenya, Raila Amolo Odinga, umeibua wimbi la huzuni na maombolezo kutoka pande mbalimbali za Afrika Mashariki, huku wasanii wakubwa wa Bongo Fleva kutoka Tanzania wakituma salamu za rambirambi kwa familia ya marehemu na wananchi wa Kenya. Mastaa wakiongozwa na Ali Kiba, Juma Jux, AY Maua Sama, Joh Makini, H Baba na wengine wengi wameungana kuonyesha masikitiko yao, wakimtaja Raila kama kiongozi wa kipekee, mwenye maono, ujasiri na upendo kwa watu wake. Kupitia mitandao ya kijamii, wasanii hao wameeleza kuguswa na kifo cha Raila, wakisema kuwa Afrika imepoteza kiongozi aliyeacha alama kubwa katika historia ya siasa na umoja wa bara hili. Wamepongeza maisha yake ya kujitolea kwa haki, demokrasia na usawa, wakisema Raila alikuwa mfano wa kuigwa kwa vizazi vingi vijavyo. Kwa pamoja, wamewatumia rambirambi kwa Rais William Ruto, familia ya Raila Odinga na wananchi wote wa Kenya, wakisisitiza kuwa wanawaombea faraja, nguvu na utulivu katika kipindi hiki cha maombolezo. Mashabiki kutoka pande zote za Afrika Mashariki wamepongeza hatua hiyo ya wasanii wa Tanzania, wakisema ni ishara ya umoja wa kijamii na kiutamaduni uliopo kati ya Kenya na Tanzania.

Read More
 Kings Music Watoa Tamko Kuhusu Kuondolewa kwa Video ya King Kiba

Kings Music Watoa Tamko Kuhusu Kuondolewa kwa Video ya King Kiba

Uongozi wa Kings Music Records wametoa tamko rasmi kuhusu tukio la kuondolewa kwa video ya wimbo maarufu wa King Kiba, Ubuyu, kutoka kwenye mtandao wa YouTube masaa machache tu baada ya kupandishwa tarehe 3 Julai, Alhamisi iliyopita. Kwa mujibu wa tamko hilo, uondoaji wa video hiyo ulitokana na vitendo vya watu wasioidhinishwa waliotumia mfumo wa kuripoti ukiukaji wa hakimiliki kwa makusudi vibaya, wakitumia majina ya uongo na madai yasiyo halali. “Tunatilia mkazo kuwa madai haya ya mtu wa tatu dhidi ya kazi yetu ni ya uongo, ya kuhuzunisha na hayakubaliki kabisa,” limesema andiko la Kings Music Records. Tukio hili limeleta taharuki kubwa miongoni mwa mashabiki na wadau wa muziki wa Bongo Flava, huku Kings Music Records wakisisitiza kwamba madhara yaliyosababishwa kwa msanii na biashara yao ni makubwa sana. “Hili si tu usumbufu wa kitaalamu, bali pia ni shambulio la moja kwa moja dhidi ya uadilifu wa kisanaa, uaminifu wa hadhira, na maisha ya wasanii katika sekta ya ubunifu,” limesisitizwa. Aidha, Kings Music Records wamesema tayari wameanzisha uchunguzi wa kisheria dhidi ya tukio hili na kwamba yeyote atakayebainika kushiriki katika udanganyifu huo atachukuliwa hatua kali za kisheria. “Hali hii si tishio kwa Alikiba peke yake, bali ni tishio kwa mfumo mzima wa ubunifu,” limesema tamko hilo. Ingawa ushindani ni sehemu ya kawaida katika tasnia ya muziki, kampuni hiyo imelaani vikali vitendo vya hila na udanganyifu kama hivi, kwa niaba ya wasanii na wabunifu wa muziki, hasa kwa lengo la kulinda hadhi ya Bongo Flava na tasnia ya muziki nchini Tanzania. Kwa mashabiki wa King Kiba, Kings Music Records wamesisitiza wanawashukuru kwa subira yao, sapoti thabiti, na imani katika nguvu ya muziki. Pia wametoa shukrani za dhati kwa wote waliochangia kutatua suala hili kwa haraka, haki na ushirikiano.

Read More
 Ali Kiba awajia juu mameneja wa WCB kwa kutumia jina lake vibaya

Ali Kiba awajia juu mameneja wa WCB kwa kutumia jina lake vibaya

Staa wa muziki wa Bongo Fleva Ali Kiba ameamua kutoa ya moyoni baada ya Mameneja kutoka lebo ya WCB, Babu Tale na Sallam SK kutoa list ya wasanii waliofanya vizuri kwa mwaka 2022. Kwenye orodha hiyo katika List alioiweka Sallam SK amewekwa nafasi ya 7 huku kwenye List ya BabuTale hayupo. Sasa kupitia ukurasa wake wa Instagram King Kiba amesema wawili hao wanajaribu kutumia jina lake kutengeneza mazingara ya kuitangaza show ya Diamond Platnumz itakayofanyika Desemba 31 mwaka huu. “I think mmeshajulika kama nilazima mchokenolewe, Ndio mfunction ,ili jambo lenu liende, mmekaa kikao kujadili na kurank wasananii. WHO ARE YOU? Nitaongea jambo lenu likiisha”, Alisema. Kwenye ujumbe wenye mafumbo ndani yake, ameonekana kumlaumu msanii Harmonize kwa kitendo cha kuzungumzia orodha hiyo kwa kusema imewapa nguvu zaidi kufanikisha jambo lao kwa kuwa wamezoea kutumia kiki kwenye shughuli zao. “Nilitamani kumwambia Njomba kimbulu asiwachokunoe maana mtakua mmekamilisha malengo yenu kwabahati mbaya Njomba Hajawagundua ila mimi nawajua vizuri for your . Najua hata hiki nilicho kiongea hapa kitawasaidia kwasababu mimi ni KING wenu,” Aliongeza.

Read More
 Ali Kiba awashauri wasanii kuzingatia maadili mema kwenye utayarishaji wa kazi zao

Ali Kiba awashauri wasanii kuzingatia maadili mema kwenye utayarishaji wa kazi zao

Mwimbaji wa Bongofleva Ali kiba amekosoa baadhi ya wasanii kuimba na kufanya video zisizo na maadili ambazo zinaharibu jamii hasa watoto. Kwenye mahojiano yake na Idhaa ya Kiswahili ya Sauti ya America (VOA), Boss huyo wa King’s Music pia ametoa ushauri kwa wanamuziki kulinda maadili ya jamii kwa kuzingatia malezi hasa ya vijana ambao hivi leo dunia imekuwa kama kijiji na matendo yote ya wanamuziki yanashuhudiwa mubashara kupitia mitandao ya kijamii na vijana hao. Ali Kiba kwa sasa yupo nchini Marekani kwenye ziara yake ya Kimuziki, na Jumamosi hii tarehe 12 anatarajia kufanya show yake ya kwanza huko Louiseville, Kentucky.

Read More
 Mke wa Ali Kiba awaacha mashabiki njia panda kuhusu ndoa yake

Mke wa Ali Kiba awaacha mashabiki njia panda kuhusu ndoa yake

Mke wa Ali Kiba ameacha maswali mengi kwenye vichwa vya mashabiki wa hitmaker huyo wa “Utu” baada ya kuandika ujumbe wenye ukakasi kwenye akaunti yake ya Instagram. Kupitia insta story yake Amina ameandika “Rasmi nipo huru” ujumbe ambao wengi wametafsiri kama ndoa yake na Ali Kiba imefikia mwisho. Kama utakumbuka vizuri, mwezi Februari mwaka huu mitandao mikubwa ya habari nchini iliripoti kuwa Amina ameomba talaka na ametaka alipwe kiasi cha shillingi laki 2 kwa mwezi kwa ajili ya matunzo ya watoto.

Read More
 ALI KIBA ATANGAZA KUREJEA KWA ZIARA YA ONLY ONE KING NCHINI MAREKANI

ALI KIBA ATANGAZA KUREJEA KWA ZIARA YA ONLY ONE KING NCHINI MAREKANI

Hitmaker wa “Utu”, Msanii Ali Kiba ametangaza kurejea kwa ziara yake ya muziki nchini Marekani “Only One King” ambayo alitangaza kuiahirisha Septemba 1, mwaka 2022 kufuatia kugundulika kuwa na ugonjwa wa Corona. Ziara hiyo ambayo ilikuwa ianze September 2, sasa imetangazwa kurejea kuanzia mwezi Oktoba na Novemba mwaka huu. Aidha King Kiba amesema tarehe rasmi zitatangazwa hivi karibuni. “My USA Fans, After A Little Delay Due to Reasons Beyond Our Control, I’m Happy To Announce “My Only One King US Tour” is Back This October-November. New Dates and Cities To Be Announced Soon. For Bookings & Inquiries Please Call 323.868.6114” Ameandika Instagram. Only One King US Tour 2022 inatarajiwa kufanyika Houston, Minneapolis, Phoenix, Des Moines, Atalanta, Lexington, Manchester, Chicago na Dallas.

Read More
 ALI KIBA ATANGAZA UJIO WA ZIARA YAKE YA MUZIKI

ALI KIBA ATANGAZA UJIO WA ZIARA YAKE YA MUZIKI

Staa wa muziki wa Bongofleva Ali Kiba ametangaza rasmi ujio wa ziara yake kimuziki ya kimatifa inayokwenda kwa jina la “Only One King” Boss huyo wa King’s Music ametangaza ujio huo kupitia ukurasa wake wa Instagram ambapo amesema ataanzia tour hiyo nchini Marekani, Septemba mwaka huu. Ali Kiba amesema, ana miaka takribani minne hajafanya ziara ya kimuziki nchini Marekani, hivyo sasa ni wakati wa kukutana na mashabiki wake wa huko. “Let the International Tours begin!! And my first tour will be in USA !!! It’s been 4 years since I was in the united states to connect with my fans, i would like to officially announce I will be starting my USA Tour this September” ameeleza ALIKIBA kupitia kurasa zake za mitandao ya kijamii. Hata hivyo ameeleza hivi karibuni ataweka wazi tarehe na mahala atakapofanya ziara hiyo nchini Marekani. “Tour dates will be announced soon be ready to party and be entertained. For Bookings & Inquires please Call 323.868.6114” – ALIKIBA.

Read More
 ALI KIBA NA HARMONIZE WANG’ARA KWENYE TUZO ZA TANZANIA MUSIC AWARDS 2021

ALI KIBA NA HARMONIZE WANG’ARA KWENYE TUZO ZA TANZANIA MUSIC AWARDS 2021

Tuzo za Tanzania Music Awards 2021 zimetolewa usiku wa kuamkia Aprili 3 huko Jijini Dares-Salaam, nchini Tanzania ambapo nyota wawili wa muziki wa BongoFleva, Ali Kiba na Harmonize wameibuka na ushindi kwenye vipengele vingi zaidi. C.E.O wa Kings Music, Ali kiba ameibuka mshindi na tuzo 5 za Tanzania Music Awards (TMA) kwenye vipengele vya Album bora (One Only King), video bora ya mwaka (Salute FT RudeBoy), mtunzi bora wa mwaka, Mwanamuziki bora wa Afrika Mashariki na Mwanamuziki Bora wa Kiume Chaguo la Watu mwaka 2021. Kwa upande wa Harmonize, yeye ameshinda tuzo 3 za Tanzania Music Awards kwenye vipengele vya Mtumbuizaji bora wa kiume, Msanii bora wa mwaka na Kolabo bora Afrika (Attitude ya Harmonize FT Awilo Longomba). Wasanii wengine walioshinda tuzo hizo ni pamoja na Nandy, Professa Jay, Darassa, Marioo, Diamond Platnumz, Young Lunya, Chemical, Saraphina, Baddest 47, Snura, Sholo Mwamba, Khadja Yusuph, Mzee Yusuph na wengine wengi.

Read More
 ALI KIBA AMPONGEZA KHALIGRAPH JONES KUMSHIRIKISHA KWENYE INVISIBLE CURRENCY ALBUM

ALI KIBA AMPONGEZA KHALIGRAPH JONES KUMSHIRIKISHA KWENYE INVISIBLE CURRENCY ALBUM

Nyota wa muziki nchini Tanzania, Ali  Kiba ameaonesha furaha yake kushirikishwa kwenye album mpya ya Rapa Khaligraph Jones, iitwayo ‘Invisibale Currency’. Kupitia ukurasa wake wa instagram Ali Kiba amemshukuru papa jones kwa kumpa shavu kwenye invisible currency album huku akipigia debe album hiyo iliyoachiwa rasmi Machi 07 mwaka wa 2022 ikiwa na jumla ya nyimbo 17 za moto. Khaligraph jones alimshirikisha ali kiba kupitia wimbo namba 9 uitwao “Wanguvu”. Wasanii wengine walioshirikishwa kwenye album ya mtu mzima khaligraph jones ni pamoja na Prince Indah, Mejja, Balck Way, Adasa, Kev The Topic, Scar Mkadinali, Xenia Manasseh, Rubeboy na Dax.

Read More