Bahati Awahimiza Wanaume Kuachia Wake Zao Mali Ndoa Inapovunjika
Msanii wa muziki wa Kenya, Bahati, ameibua mjadala mtandaoni baada ya kuwataka wanaume waachie wake zao mali na kila kitu iwapo wataachana au kupeana talaka. Akizungumza katika mahojiano yaliyosambazwa kwenye mitandao ya kijamii, Bahati amesisitiza kuwa amani ya moyo na kuanza upya ni jambo la maana zaidi kuliko kushikilia mali au vitu vya kidunia. Kwa mujibu wa msanii huyo, ni bora mwanaume aondoke mikono mitupu lakini akiwa na utulivu wa nafsi, kuliko kuingia kwenye malumbano yasiyoisha kuhusu mgawanyo wa mali. Bahati, ambaye mara nyingi huzungumza kwa ujasiri kuhusu masuala ya ndoa na mahusiano, amesema kuwa wanaume wanaojikuta wakipigania mali huishia kuchoshwa kiakili na kifedha. Hata hivyo amewashauri badala yake wajikite katika kujijenga upya na kusonga mbele. Kauli hiyo imezua maoni tofauti miongoni mwa mashabiki. Baadhi wamepongeza msanii huyo kwa kuhimiza amani na ukomavu, huku wengine wakisema wanaume nao wanastahili haki na si sahihi kuondoka bila chochote walichokifanyia kazi.
Read More