BAHATI ATUHUMIWA KUIBA IDEA YA WIMBO WA JE UNANIFIKIRIA KUTOKA KWA MARIOO

BAHATI ATUHUMIWA KUIBA IDEA YA WIMBO WA JE UNANIFIKIRIA KUTOKA KWA MARIOO

Mkali wa muziki nchini Bahati ameingia tena katika mijadala kwenye mitandao nchini  baada ya kudaiwa kuiba  idea ya wimbo wa  ‘For You’ wa msanii  wa Bongofleva Marioo Kulingana na ripoti inayosambaa mitandaoni, inadaiwa Bahati ametumia mdundo na ubunifu wa video wa wimbo huo kwenye wimbo wake mpya wa”Je unanifikiria”, hivyo kuibua maswali mengi miongoni mwa wadau wa muziki nchini ambao walienda mbali zaidi na kuhoji kuwa msanii huyo amekosa ubunifu kwenye muziki wake. Hata hivyo Bahati hajetoa tamko lolote kuhusiana na madai hayo yaliyoibuliwa na baadhi ya watumiaji wa mitandao ya kijamii.

Read More
 BAHATI APEWA TUZO BOOMPLAY

BAHATI APEWA TUZO BOOMPLAY

Nyota wa muziki nchini Bahati ametunukiwa tuzo ya silver Plaque na mtandao wa kupakua na kusikiliza muziki wa boomplay Kenya. Hii ni baada hitmaker huyo wa “Pete yangu” kufikisha zaidi ya streams millioni 8 kupitia nyimbo zake zote zilizopakiwa kwenye mtandao  huo. Kupitia ukurasa wake wa Instagram bahati amewashukuru mashabiki zake kwa kuendelea kufuatilia kazi zake ambazo zinazidi kuonyesha mafanikio makubwa ndani na nje ya Kenya. Tuzo hizo maarufu kama ‘Boomplay Plaques’ hutolewa kutambua jitihada za wasanii wanaofanya vizuri kwenye App ya Boomplay.

Read More