GRAVITY OMUTUJJU: BEBE COOL SIO RAFIKI YANGU WA KARIBU, SIMPENDI

GRAVITY OMUTUJJU: BEBE COOL SIO RAFIKI YANGU WA KARIBU, SIMPENDI

Rapa kutoka Uganda Gravity Omutujju amefunguka na kudai kuwa hataki kuwa rafiki wa msanii mwenzake Bebe Cool licha ya kufanya wimbo wa pamoja. Katika mahojiano yake ya hivi karibuni Omutujju amesema hana ugomvi wowote na msanii huyo ila hajawahi pata amani akiwa karibu na bebe cool kwa sababu ni mnafiki mkubwa. Bebe Cool na Gravitty Omuttuju walifanya wimbo wa uitwao “Kerere” mwaka wa 2017 lakini hawakuweza kutoa video ya wimbo huo. Mwaka wa 2020 kwenye moja ya mahojiano gravity omutujju alimulaumu Bebe Cool kwa kushindwa kuandaa video ya wimbo huo jambo ambalo limetafsiriwa na wajuzi wa mambo kwenye mitandao ya kijamii kuwa huenda ndio sababu ya wawili hao kutokuwa na mahusiano mazuri.

Read More
 ZIZA BAFANA AMCHANA BEBE COOL KISA ORODHA YAKE YA WASANII WALIOFANYA VIZURI MWAKA 2021

ZIZA BAFANA AMCHANA BEBE COOL KISA ORODHA YAKE YA WASANII WALIOFANYA VIZURI MWAKA 2021

Mwanamuziki anayesuasua kimuziki nchini Uganda Ziza Bafana hana furaha kabisa baada ya kutoonekana kwenye orodha ya wasanii wa kila mwaka ambayo hutolewa na msanii mwenzake Bebe Cool. Bafana, ambaye alifanya vizuri mwaka wa 2021 kwa kuachia magoma makali anadai kuwa Bebe Cool alipoteza mweelekeo katika tasnia ya muziki nchini Uganda kwani siku hizi hajakuwa akiachia muziki mzuri kama kipindi cha nyuma. Hitmaker huyo wa “Embuzi” amesema Bebe Cool,anatumia orodha yake ya kila mwaka ya wasanii waliofanya vizuri kutengeneza mazingira ya kuzungumziwa kwenye vyombo vya habari nchini Uganda. Ikumbukwe Bebe Cool hajawahi kuwa na uhusiano mzuri na mwanamuziki mwenzake Ziza Bafana baada ya msanii huyo kuanza kujihusisha na matumizi ya dawa za kulevya miaka kadhaa iliyopita.

Read More
 BEBE COOL AKANUSHA TETESI ZA KUKUTWA NA KIRUSI CHA OMICRON

BEBE COOL AKANUSHA TETESI ZA KUKUTWA NA KIRUSI CHA OMICRON

Msanii mkongwe kwenye muziki nchini Uganda Bebe Cool amefunguka kuhusu ugonjwa uliompelekea kukimbizwa hospitali mwishoni mwa juma lilopita. Kupitia ukurasa wake wa Facebook Bebe Cool ameweka wazi kuwa alikuwa anaugua malari, ugonjwa ambao hakuwa fikiria utampata. Hitmaker huyo “Gyenvudde” amesema kwa sasa amepata ufahamu wa kwanini Wizara Afya nchini Uganda imekuwa mstari wa mbele kusisitiza umuhimu wa kukabiliana na ugonjwa wa malaria. Tamko la Bebe Cool limekuja mara baada ya tetesi kusambaa kwenye mitandao ya kijamii zikidai kuwa msanii alikimbizwa hospitali baada ya kukutwa na kirusi cha Omicron

Read More
 BEBE COOL KUZINDUA TUZO YAKE YA MUZIKI AMBAYO ITAGHARIMU SHILLINGI MILLIONI 127

BEBE COOL KUZINDUA TUZO YAKE YA MUZIKI AMBAYO ITAGHARIMU SHILLINGI MILLIONI 127

Msanii mkongwe kwenye muziki nchini Uganda Bebe Cool alitangaza mwishoni mwaka 2021 aliahidi kuzindua tuzo yake ya kila mwaka kwa ajili ya kutambua juhudi za wasanii wanaofanya vizuri kwenye tasnia ya muziki nchini Uganda. Kwenye mahojiano yake ya hivi karibuni Bebe Cool amesema ametanga shillingi millioni 127 za Kenya ambayo itatumika kuendesha shughuli ya kuzindua tuzo yake ambayo inatarajiwa kuanza mwaka huu. Hitmaker huyo “Gyenvudde” amesema waasanii watatunukiwa pesa taslimu badala ya tuzo za glassi ambazo wamekuwa wakipewa na waandaaji wa tuzo zenye thamani ya takriban shillingi elfu 63 za Kenya. “Tuzo za Uganda hazina maana. Nazindua tuzo yangu ambayo itakuwa tofauti. Tuzo ya Bebe Cool itaghrarimu kati ya shillingi billioni 1.5 hadi  billioni 2 pesa za Uganda..alisema kwenye mahojiano na runinga moja nchini Uganda. Bebe cool amesisitiza kuwa katika kipindi cha miaka miwili ijayo tuzo yake itakuwa yenye bora afrika mashariki na kati.

Read More
 BEBE COOL AWACHANA WAANDAJI WA TUZO ZA MUZIKI UGANDA

BEBE COOL AWACHANA WAANDAJI WA TUZO ZA MUZIKI UGANDA

Mkongwe wa muziki kutoka nchini Uganda Bebe Cool amewatolea uvivu waandaji wa tuzo za muziki nchini humo kwa kuwapa wasanii tuzo ambazo hazina muhimu wowote. Akiwa kwenye moja ya Interview Bebe Cool amesema waandaji wa tuzo nchini Uganda wamekuwa na mazoea ya kuwapa wasanii tuzo ambazo msanii hawezi uuza na akapata pesa za kujikimu kimaisha. Bosi huyo wa Gagamel amedokeza mpango wa kuja na tuzo yake mwakani na washindi watapokezwa kati ya shillingi laki moja na laki tatu kulingana na kipengele ambacho msanii husika atakuwa ameteuliwa kushiriki. Kauli ya Bebe Cool imekuja  siku chache mara baada ya Spice Diana kuwachana waandaji wa tuzo nchini uganda wasimteue  kwenye tuzo zao bila kumshirikisha.

Read More