Eric Omondi apigwa marufuku kuhudhuria tamasha la Sol Fest

Eric Omondi apigwa marufuku kuhudhuria tamasha la Sol Fest

Mwimbaji mkuu wa Sauti Sol Bien-Aime Baraza amempiga marufuku mchekeshaji Eric Omondi kuhudhuria tamasha lijalo la Sol Fest. Katika taarifa aliyotoa kupitia ukurasa wake wa Instagram, Bien ameweka wazi kuwa Omondi hataruhusiwa katika ukumbi wa hafla hiyo kutokana na kitendo chake cha kuwazungumzia vibaya wasanii wa Kenya. Hitmaker huyo wa “Inauma” ameongeza kuwa tayari wameagiza timu yao ya usalama kumzuia Omondi kuingia katika ukumbi wa tamasha lao la kila mwaka. “Eric, mdomo wako mkubwa umekuponza! Usiwalaumu wanamuziki. Hakuna mtu anayetaka kukuona kwenye Sol Fest kwa hivyo tafadhali kaa mbali!!!”, “Timu ya usalama ya Sol fest africa asubuhi ya leo imepokea maagizo makali ya kutoruhusu huyu jamaa na mbwa wake waliokopwa, karibu na ukumbi wa tamasha!.. “Binafsi, nimewasilisha zuio dhidi yake. Kwa hiyo, nawasihi nyote mumuepuke kama majanga!!!, Aliandika Instagram. Hata hivyo, Eric Omondi alijibu kwa kusema kwamba anataka tiketi 20 za VIP na mbwa wake kupewa ulinzi maalum atakapohudhuria Sol Fest Disemba 9 mwaka huu. Onyo hilo la Bien linajiri saa chache baada ya Omondi kusema kwamba atahitaji mbwa wasiopungua 20 ili aweze kuhudhuria Sol Fest kutokana na maisha yake kuwa hatarini. Eric Omondi amekuwa akiwashambulia wasanii wa Kenya kila mara akisema kuwa wamezembea kwenye suala la kutoa nyimbo na kupelekea wasanii wageni kutawala tasnia ya muziki nchini.

Read More
 Bien wa Sauti Sol ajibu madai ya Crystal Asige kufungua kesi mahakamani dhidi ya Sol Generation

Bien wa Sauti Sol ajibu madai ya Crystal Asige kufungua kesi mahakamani dhidi ya Sol Generation

Mwimbaji wa Sauti Sol amefunguka kwa mara ya kwanza baada ya aliyekuwa msanii wa Sol Generation Crystal Asige kuwasilisha kesi mahakamani dhidi ya bendi hiyo maarufu kwa kukiuka mkataba wake. Akizungumza na Mpasho, Bien amesema bendi ya Sauti Sol iko tayari kukutana na seneta huyo mteule ambaye anawakilisha watu wanaoishi na ulemavu, mahakamani kupata mwanga kuhusu mgogoro unaozingira mkataba wake na lebo ya Sol Generation. “Tukutane kortini na kuweka hati zetu zote mezani. Tunaweza tu kufuata njia aliyochagua. Masuala hayo yanaweza kushughulikiwa vyema mahakamani kama alivyofanya,” Bien alisema. Kwa mujibu wa nyaraka za mahakama, Asige anaitaka mahakama kuwashurutisha wasanii wa Sauti Sol kuweka wazi kiasi cha pesa ambacho walipata kutoka kwa nyimbo alizoshirikisha tangu mwaka 2019. Nyimbo hizo ni pamoja na Lenga, Extravaganza, Ukiwa Mbali, Intro na Favourite Song. Lakini pia anaitaka mahakama kuagiza kundi la Sauti Sol kumlipa fidia huku akisisitiza wawasilishe taarifa zote za leseni kuhusu nyimbo alizoshirikishwa. Crystal Asige ameishtaki Sol Generation Records Limited, Bien-Aime Baraza, Polycarp Otieno, Willis Chimano, Delvin Mudigi na KLM Royal Dutch Airlines Kenya.

Read More
 Bien awapa somo wasanii wa Kenya jinsi ya kukuza muziki wao

Bien awapa somo wasanii wa Kenya jinsi ya kukuza muziki wao

Mwanakikundi wa Sauti Sol, Bien amekanusha madai yaliyoibuliwa na mchekeshaji Eric Omondi kuwa siri yake ya kuingia kwenye chati za Apple Music imetokana na kiki kwenye muziki wake. Bien amesema hajawahi tengeneza matukio kwa ajili ya kutangaza muziki wake huku akisema mafanikio yake yamechangiwa na kujituma kwenye suala la kutoa muziki mzuri. Msanii huyo ametoa changamoto kwa wasanii kuacha kutengeneza matukio yakuchafuana mtandaoni kwa lengo la kujitafuatia umaarufu na badala yake wawekeze muda wao kutoa muziki mzuri. Bien ni msanii pekee kutoka Kenya aliyefanikiwa kuingiza nyimbo mbili kwenye chati za Apple Music Top 100. Nyimbo hizo ni pamoja na; Inauma ambayo ilikamata nafasi ya 40 huku “Dimension” aliyomshirikisha Fully Focus ikikamata nafasi ya 87.

Read More
 Bien wa Sauti Sol amjibu Mchekeshaji Eric Omondi kwa kuwaponda wanamuziki wa Kenya

Bien wa Sauti Sol amjibu Mchekeshaji Eric Omondi kwa kuwaponda wanamuziki wa Kenya

Msanii wa Sauti Sol, Bien amemtolea uvivu mchekeshaji Eric Omondi kwa kukosoa wasanii wa kenya kutokana na kuzembea kuachia nyimbo. Kupitia ukurasa wake wa instagram bien amemtaka Omondi akome kuwashinikiza wasanii wa Kenya waachie muziki mzuri wakati uchekeshaji umemshinda. Mkali huyo wa ngoma ya “Inauma” amemtaka Omondi kuwekeza nguvu zake kwenye suala la kufufua tasnia ya ucheshi ambayo kwa mujibu wake imepoteza mwelekeo. Hata hivyo mashabiki wameonekana kumuunga mkono Bien huku wengine wakimtaka msanii huyo akubali ukweli muziki wa kenya umeshuka kwa kuwa wasanii hawatoi nyimbo nzuri ikilinganishwa na wasanii wa mataifa mengi. Kauli ya Bien imekuja mara baada ya Eric Omondi kushangazwa na hatua ya wasanii wa Kenya kushindwa kuingiza nyimbo nyingi kwenye chati ya muziki ya Apple Music ambayo imetawaliwa na wasanii wa Nigeria.

Read More
 BIEN WA SAUTI SOL AWATAKA WASANII WA KENYA KUIMBA NYIMBO ZA KIINGEREZA

BIEN WA SAUTI SOL AWATAKA WASANII WA KENYA KUIMBA NYIMBO ZA KIINGEREZA

Mwanamuziki wa Sauti Sol, Bien ametoa changamoto kwa wasanii nchini kuanza kutumia lugha ya kiingereza kwenye nyimbo zao ili muziki wa Kenya uweze kufika mbali zaidi. Bien amesema licha ya wasanii wa Kenya kutoa muziki mzuri wengi wao wamekuwa wakitumia lugha ya Sheng kwenye nyimbo zao jambo analosema limewafanya wasanii kushindwa kutanua wigo wa muziki wao kimataifa. Katika hatua nyingine Bien amekiri kuwa hakuwa anajitambua kimuziki kabla ya wasanii wa kundi la Sauti Sol kuanza kufanya kazi zao kama wanamuziki wa kujitegemea. Hitmaker wa “Inauma” amesema amejifunza mambo mengi kama msanii huru ikiwemo kutayarisha na kuandilka nyimbo zake mwenyewe.

Read More
 BIEN WA SAUTI SOL AFUNGUKA KUHUSU UCHAGUZI MKUU NCHINI KENYA

BIEN WA SAUTI SOL AFUNGUKA KUHUSU UCHAGUZI MKUU NCHINI KENYA

Mwana kikundi wa Sauti Sol, Bien amefunguka namna uchaguzi nchini Kenya ulivyoendeshwa. Katika mahojiano na Mungai Eve, Bien amesema mchakato mzima wa uchaguzi mkuu nchini ulikuwa wa haki na huru ambapo amewapongeza wakenya kwa kudumisha Amani kabla na hata baada ya uchaguzi. Hitmaker huyo “Inauma” amewataka wakenya kurejea kazini baada ya Rais mteule William Ruto kutangazwa na Tume huru ya uchaguzi IEBC hata kama kuna wale ambao hawakuridhishwa na matokeoa ya urais. Bien ametoa wito kwa serikali mpya itakayoingia mamlakani kuboresha sanaa nchini Kenya ili vijana waweze kupata ajira. Kuhusu mgogoro wao na muungano wa kisiasa wa Azimio la Umoja kutumia wimbo wao wa “Extravangaza bila ridhaa ya Sauti Sol, Bien amesema mawakili wao wanashughulikia suala hilo kuhakikisha wanapata haki.

Read More
 BIEN AFUNGUKA KUHUSU SAUTI SOL KUTOTUMBUIZA KWENYE MAJUKWAA YA KISIASA.

BIEN AFUNGUKA KUHUSU SAUTI SOL KUTOTUMBUIZA KWENYE MAJUKWAA YA KISIASA.

Mwanakikundi wa Sauti Sol Bien amefunguka mara baada ya Diamond Platnumz kupewa nafasi ya kutumbuiza kwenye mkutano wa kisiasa wa mrengo wa Azimio la Umoja juzi kati. Kulingana na Hitmaker huyo “Inauma”,  sio wasanii wote wana haja ya kutumbuiza kwenye majukwaa ya kisiasa. “We don’t want to be in political forums” Amesema Bien. Bien ametoa kauli hiyo kufuatia hatua ya mchekeshaji Eric Omondi kuwatolea uvivu wasanii wa Kenya kwa kutotumbuiza kwenye hafla ya kisiasa ya Azimio la Umoja huko Kasarani.

Read More
 BIEN: SILALI CHUMBA KIMOJA NA MKE WANGU

BIEN: SILALI CHUMBA KIMOJA NA MKE WANGU

Msanii wa kundi la Sauti Sol Bien kwa mara nyingine tena ameibuka na kauli yenye utata kuhusu maisha yake na mkewe Mtangazaji Chikki. Akipiga stori na Mambo Mseto ya Radio Citizen Bien amesema licha ya mkewe kuwa Meneja wake, wanaposafiri kwa ajili ya show kila mmoja hulala chumba chake. “Katika ndoa yetu kuna mipaka pia, kwa mfano kama nimeitwa mahali niko na shoo, nakaa kwa chumba cha hoteli mimi peke yangu. Huwa sitaki hata muziki hapo ndani. Nataka tu kukaa peke yangu nijisikilize na kujitathmini kuhusu jinsi nitakavyoifanya hiyo shoo” alisema. “Kwa hiyo kama unaniita kama ajenti ama promota, huwezi nitengea chumba kimoja mimi na mke wangu, sitaki kulala na yeye kitanda kimoja hiyo siku, nataka kuenda kujisikilizia,” alisema Bien. Hittmaker huyo wa ngoma ya “Inauma” amefafanua kwamba wakienda kwa shoo na mke wake mambo ya uchumba yanabaki nyumbani na kule wanaenda kama msanii na Meneja wake na kwa hiyo kuna umuhimu wa kila mmoja kutengewa chumba chake binafsi mbali na mwingine.

Read More
 BIEN AWAPA SOMO VIJANA WALIO CHINI YA UMRI WA MIAKA 30

BIEN AWAPA SOMO VIJANA WALIO CHINI YA UMRI WA MIAKA 30

Mwimbaji mkuu wa Kundi la Sauti Sol nchini Kenya Bien amesema hashauri watu waliopo katika umri wa miaka ya ishirini kuwa kwenye uhusiano wa kimapenzi kwani ni kupotezeana muda. Bien amesema watu walio katika umri huo wanapaswa kujijali wenyewe na kusafiri kwa kuwa mtu aliyeko katika umri huo bado anajitafuta ajue kitu gani hasa anakihitaji. “Siwezi kumpa ushauri mtu mwenye umri wa miaka ishirini awe kwenye mahusiano, ni kupoteza muda, angalau fanya kazi, usafiri pia uwe na watu wengine huku na huko.” alisema Bien. Aidha aliongeza kwamba mtu akiwa katika umri huo hajitambui na mtu aliye naye pia hajitambui “Unadhani unafanya nini? Mnajaribu kusuluhisha mambo pamoja lakini mwisho wa siku yaani nadhani ni bora kuwa peke yako ikiwa uko katika miaka ya 20” alimaliza Mwanamuziki huyo.

Read More
 BIEN WA SAUTI SOL AFUNGUKA KUHUSU KUPANGA UZAZI

BIEN WA SAUTI SOL AFUNGUKA KUHUSU KUPANGA UZAZI

Msanii kutoka kundi la Sauti Sol Bein Aim Baraza amesema kuwa yupo tayari kukata mshipa wa uzazi maarufu vascectomy punde atakapo pata watoto na mke wake Chiki Kuruka. Akizungumza kwenye kipindi cha Baldmen Session kwenye mtandao wa youtube Bein amesema kuwa kupanga uzazi barani Afrika ni swala ambalo limewachiwa wanawake. Bien amesema kuwa hawezi kumwachia mke wake mzigo huo pekee licha ya kuwa wanaume wengi wanaogopa kufanyiwa vasectomy. “Wanaume wengi hawako tayari kufanyiwa vasektomi lakini mimi niko tayari kuangalia vasektomi, nimechoka kuweka mzigo huu kwa vifaranga wetu, kwanza najua dawa mbalimbali za uzazi wa mpango zina madhara tofauti. “Amesema Bien kwenye kipindi anachoandaa. Lakini pia amefunguka kuwa mashabiki wamekuwa wakimshinikiza kupata mtoto na mke wake Chiki Kuruka licha ya kuwa kwenye ndoa kwa miezi 18 pekee. “Hata mimi Wakenya wameniangalia weird, I’ve stayed karibu for 18 months na sijafanya kitu lakini kila kitu na time yake,” alisema. “Sijawahi kuwa na hamu ya kuzaliana! Kwa hiyo haijawahi kunisumbua sana.” amesema

Read More
 BIEN ATOA YA MOYONI KUHUSU ERIC OMONDI KULETA MAGEUZI KWENYE MUZIKI KENYA

BIEN ATOA YA MOYONI KUHUSU ERIC OMONDI KULETA MAGEUZI KWENYE MUZIKI KENYA

Msanii wa Sauti Sol, Bien amedai kwamba anaunga mkono harakati za  mchekeshaji Eric Omondi kuleta mabadiliko kwenye tasnia ya muziki nchini. Katika mahojiano na Plug tv, Bien amesema kitu ambacho kinamfanya wakati mwingine kutofautiana kimawazo na Eric Omondi ni kutokana na mchekeshaji huyo kuingiza kiki nyingi kwenye masuala muhimu. Bien amesema licha ya kwamba wamekuwa wakitupia maneno makali mtandaoni na Eric Omondi, anaheshimu kila ambacho mchekeshaji huyo anakifanya kwa kuwa anajituma sana kwenye shughuli zinazomuingizia kipato. Katika hatua nyingine Bien amewataka wakenya waache kasumba ya kuwashambulia watengeneza maudhui na badala yake wawe mstari wa mbele kuunga mkono shughuli zao kwani kuwakosa kila mara ni ulimbukeni wa hali ya juu.

Read More
 BIEN WA SAUTI SOL AZIDI KUMSHAMBULIA EZEKIEL MUTUA

BIEN WA SAUTI SOL AZIDI KUMSHAMBULIA EZEKIEL MUTUA

Msanii wa Sauti Sol bien amemtolea uvivu Mwenyekiti wa Chama cha Hakimiliki na Muziki nchini Ezekiel Mutua baada ya kudai kuwa alipewa mamlaka ya kutoa kibali kwa nyimbo zao kutumika kwenye shughuli za kibiashara. Katika mahojiano na Eve Mungai, Bien amesema ameshangazwa na hatua ya Mutua kutoa ruhusa ya wimbo wa “Extrangaza” kutumika kwenye shughuli za muungano wa Azimio la Umoja bila idhini yao ikizingatiwa kuwa walitumia kiasi cha shillingi millioni 2 za Kenya kutayarisha video ya wimbo huo. Aidha ameenda mbali zaidi na kusema kuwa Ezekiel Mutua hajui majukumu yake kwani alipewa wadhfa huo kuangazia maslahi ya wanasiasa. Hata hivyo amedokeza kuwa wanaendelea na mazungumzo na uongozi wa azimio la umoja kupata suluhu ya mgogoro uliobuka kati yao huku akitoa wito kwa mashabiki waendelea kusikiliza na kucheza nyimbo zao kwenye maeneo ya umma.

Read More