LOVE DAMINI YA BURNA BOY YAWEKA REKODI BOOMPLAY
Mwanamuziki kutoka Nigeria Burna Boy anaendelea kufanya vizuri kupitia album yake mpya na ya sita katika muziki wake iitwayo “Love, Damini” ambayo ilitoka rasmi Julai 8 mwaka huu. Habari njema ni kwa mashabiki wa mkali huyo ni kwamba, ameweka rekodi katika mtandao wa Boomplay kwa album yake hiyo yenye mwezi mmoja na siku kadhaa tangu itoke kufikisha Streams zaidi ya Milioni 100. Kufuatia hilo Burna Boy anakuwa msanii mwenye jumla ya Streams nyingi katika akaunti yake ya Boomplay akiwa na Streams Milioni 402.4 Mbali na hayo, album ya “Love, Damini” yenye hits mbalimbali kama “Kilometre” inashikilia rekodi ya muda wote kwa kuingiza nyimbo nyingi mfululizo kwenye chart mpya za muziki za Billboard US Afrobeats. Burna ameingiza nyimbo 19 zote toka kwenye album yake “Love, Damini.”
Read More