SHATTA WALE AMVUA NGUO BURNA BOY, ATOA MATUSI MAZITO

SHATTA WALE AMVUA NGUO BURNA BOY, ATOA MATUSI MAZITO

Bifu la Shatta Wale wa Ghana na Burna Boy wa Nigeria linaendelea kushika kasi, Shatta Wale ameibuka na kuweka wazi kuwa yupo tayari kuingia ulingoni na African giant, Burna Boy. Kupitia mfululizo wa tweets za matusi katika mtandao wa Twitter  Shatta Wale alionekana mwenye hasira huku akitoa vitisho kwa Burna Boy asikanyaga kwenye ardhi ya Ghana kwani atamshushia kichapo cha mbwa kitakachoimuacha na majeraha. Shatta ametoa kauli hiyo mara baada ya Burna Boy kudai kuwa hatomvumilia msanii yeyote anayetaka kuigawanya tasnia ya muziki Afrika ambapo alienda mbali zaidi na kusema kwamba yupo tayari kuzichapa na Shatta Wale ambaye juzi kati amekuwa akiwashambulia mashabiki na wasanii wa Nigeria kwa kutosapoti muziki wa mataifa mengine ya Afrika. Hata hivyo Burna Boy hajajibu chochote mpaka sasa kuhusiana na ishu ya Shatta Wale kumtolea uvivu

Read More
 BURNA BOY KUICHAFUA MADISON SQUARE GARDEN APRIL 28, 2022

BURNA BOY KUICHAFUA MADISON SQUARE GARDEN APRIL 28, 2022

Burna Boy ametangaza rasmi onesho lake ambalo litafanyika katika ukumbi mkubwa na maarufu wa Madison Square Garden uliopo New York nchini Marekani. Onesho hilo ‘One Night In Space’ litafanyika April 28 mwaka 2022 ambapo Burna Boy ataweka rekodi ya kuwa msanii wa kwanza toka Afrika kuibariki steji hiyo kama msanii kinara. Uongozi wa Madison Square Garden pia umeutumia ukurasa wao wa Instagram kutangaza onesho hilo na tiketi zitaanza kuuzwa mnamo Disemba 16. Ukumbi wa MSG una uwezo wa kubeba watu 20,789. Justin Bieber ndiye anashikilia rekodi ya kuujaza ukumbi huo kwa haraka zaidi, show zake mbili za ‘Believe Tour’ zilikuwa Sold out ndani ya sekunde 30 mwaka 2012. Kabla, mwanadada Taylor Swift ndiye alikuwa akishikilia rekodi hiyo kwa kuujaza kwa sekunde 60 mwaka 2009

Read More
 BURNA BOY ATAKA BANGI IRUHUSIWE NIGERIA, ADAI HAINA MADHARA

BURNA BOY ATAKA BANGI IRUHUSIWE NIGERIA, ADAI HAINA MADHARA

Nyota wa muziki kutoka nchini Nigeria Burna Boy amesema kwamba ni vyema sheria ikaruhusu matumizi ya bangi nchini humo kwani haina madhara kama ambavyo wengi wanasema. Akihojiwa kwenye kipindi cha ‘Home Grown Radio’ jijini Los Angeles, Burna ameeleza kwamba watu wengi wanatumia bangi lakini hawataki kutangaza hadharini lakini kiukweli hamna madhara mabaya yoyote mtu akitumia. “Kila mtu anatumia bangi lakini hakuna anayetaka kusema au kukutwa nayo.” amesema Burna Boy. Lakini pia Hitmaker huyo wa Kilo metre amesema watu wazima na viongozi wamefanikiwa kutoa elimu kwa jamii kwamba endapo mtu akitumia bangi basi atakuwa chizi jambo ambalo yeye amelikataa na kusema kuwa ni uongo,  hivyo ni bora sheria iruhusu matumizi ya bangi.

Read More
 BURNA BOY AKAVA JARIDA LA ES MAGAZINE LA NCHINI UINGEREZA

BURNA BOY AKAVA JARIDA LA ES MAGAZINE LA NCHINI UINGEREZA

Staa wa muziki kutoka nchini Nigeria  Burna Boy ambaye anafanya vizuri kupitia kazi zake mbalimbali, ametokea mbele ya kava la Jarida la Es Magazine la nchini Uingereza. Jarida la Evening Standard Magazine ni jarida kutoka London, Uingereza ambalo hujihusisha kwa kutoa habari za burudani kutoka kwa mastaa wakubwa ulimwenguni. Kwenye Jarida hilo Burna Boy  amefunguka mengi kuhusiana na muziki wake, mpaka kufikia hapo alipo. Uwezo wake mkubwa wa kujaza kwenye Arena, dili mbalimbali alizozipata kama PEPSI, kukutana na mastaa wakubwa, kushiriki kwenye album za wasanii kutokea Marekani. Hata hivyo, Burna boy  anakuwa msanii wa tatu kutoka Afrika kupata nafasi ya kukava jarida la ES, mwaka 2019 WizKid alikava Jarida hilo na mwaka 2020 ikawa zamu ya Davido kutokea kwenye jarida hilo. Ikumbukwe, Burna Boy kupata nafasi ya kukava kwenye jarida hili kubwa ulimwenguni kunampa nafasi ya kuzingatiwa, kuongeza mashabiki na watu kupata nafasi ya kuweza kumfuatilia zaidi.

Read More