BURNA BOY AKAVA JARIDA LA ES MAGAZINE LA NCHINI UINGEREZA
Staa wa muziki kutoka nchini Nigeria Burna Boy ambaye anafanya vizuri kupitia kazi zake mbalimbali, ametokea mbele ya kava la Jarida la Es Magazine la nchini Uingereza. Jarida la Evening Standard Magazine ni jarida kutoka London, Uingereza ambalo hujihusisha kwa kutoa habari za burudani kutoka kwa mastaa wakubwa ulimwenguni. Kwenye Jarida hilo Burna Boy amefunguka mengi kuhusiana na muziki wake, mpaka kufikia hapo alipo. Uwezo wake mkubwa wa kujaza kwenye Arena, dili mbalimbali alizozipata kama PEPSI, kukutana na mastaa wakubwa, kushiriki kwenye album za wasanii kutokea Marekani. Hata hivyo, Burna boy anakuwa msanii wa tatu kutoka Afrika kupata nafasi ya kukava jarida la ES, mwaka 2019 WizKid alikava Jarida hilo na mwaka 2020 ikawa zamu ya Davido kutokea kwenye jarida hilo. Ikumbukwe, Burna Boy kupata nafasi ya kukava kwenye jarida hili kubwa ulimwenguni kunampa nafasi ya kuzingatiwa, kuongeza mashabiki na watu kupata nafasi ya kuweza kumfuatilia zaidi.
Read More