Content Creators Wa Kenya Wamuacha Chief Godlove na Hasara

Content Creators Wa Kenya Wamuacha Chief Godlove na Hasara

Billionea Chief Godlove anakadiria kupata hasara ya maelfu ya pesa baada ya gari lake kupasuliwa kioo ndani ya Nairobi CBD, tukio lililotokea wakati akikutana na content creators mbalimbali jijini humo. Licha ya hasara hiyo, Chief Godlove amesema tukio hilo liligeuka kuwa ushuhuda wa upendo mkubwa na mshikamano wa dhati kutoka kwa content creators wa Kenya. Ameeleza kuwa alichokutana nacho siku hiyo kilizidi thamani ya hasara aliyopata, kwani alipokea faraja, moyo wa kujali na sapoti kubwa kutoka kwa watu aliokutana nao. Kwa mujibu wake, ingawa kioo cha gari lake kilipasuka katika hali ya msongamano na juhudi za watu kulazimisha kumuona, tukio hilo lilimfunulia ukubwa wa upendo aliokuwa nao kutoka kwa jamii ya waandaaji wa maudhui. Kutokana na kuguswa na tukio hilo, Chief Godlove ametangaza kuwa Jumapili ijayo content creators wote watakutana Nairobi CBD, ambapo ameahidi kugharamia chakula na vinywaji vyote kama ishara ya shukrani kwa upendo alioupokea

Read More
 Chief Godlove Afunguka Sababu za Kusafirisha Magari yake Kenya

Chief Godlove Afunguka Sababu za Kusafirisha Magari yake Kenya

Bilionea Chief Godlove amefunguka kuhusu uamuzi wake wa kusafirisha baadhi ya magari yake ya kifahari kutoka Dar es Salaam, Tanzania hadi Nairobi, Kenya. Kupitia mitandao ya kijamii, Godlove amesema hatua hiyo imechochewa na changamoto ya uhaba wa mafundi wenye ujuzi wa kutosha kuyahudumia magari hayo nchini Tanzania. Mwanamitandao huyo, amesema kuwa magari yake yanahitaji huduma maalum za kitaalam ambazo hazipatikani kwa urahisi nchini humo. Huduma hizo zinajumuisha uoshaji na marekebisho ya kiufundi (service) yanayohitaji ujuzi wa hali ya juu. Godlove amesema kuwa atakaporejea Dar es Salaam, atafanya tathmini ya iwapo atanunua magari mengine ya kifahari au ataendelea kutumia yaliyopo.

Read More
 Chief Godlove Awaziba Mdomo Waliomcheka Mtandaoni

Chief Godlove Awaziba Mdomo Waliomcheka Mtandaoni

Bilionea maarufu mtandaoni, Chief Godlove, amewaziba mdomo watu waliomcheka kufuatia taarifa zilizosambaa mitandaoni zikidai magari yake yalipigwa mnada kutoka na madeni. Kupitia ujumbe wake mzito, amejigamba kuwa hatafilisika milele kwa kuwa bado ana uwezo mkubwa kifedha. Amesisitiza kuwa hakuna mtu yeyote anaweza kumwambia chochote kuhusu maisha au mafanikio. Godlove amesema kejeli alizopokea zimemfungua macho na kumfundisha funzo kubwa kwamba watu wengi hawafurahii mafanikio ya wengine, hasa pale mtu anapofanikiwa kwa kasi. Ameeleza kuwa badala ya kuonea fahari hatua alizofikia, baadhi ya watu wamekuwa wakisubiri anguko lake ili wapate jambo la kucheka. Chief Godlove ameenda mbali zaidi kwa kuwashambulia waliomcheka, akiwaita maskini, akisema kejeli zao zinatokana na chuki na wivu. Amehitimisha ujumbe wake kwa kusisitiza kuwa ataendelea kusonga mbele, kufanya kazi na kufanikisha malengo yake bila kujali maneno ya watu.

Read More
 Chief Godlove Akerwa na Kejeli Baada ya Gari zake Kudaiwa Kupigwa Mnada

Chief Godlove Akerwa na Kejeli Baada ya Gari zake Kudaiwa Kupigwa Mnada

Bilionea maarufu mitandaoni, Chief Godlove, ameshindwa kujiuzuia baada ya kukumbwa na wimbi la kejeli kutoka kwa mashabiki kufuatia taarifa za magari yake ya kifahari kupigwa mnada kutokana na madeni. Kupitia taarifa aliyotoa mtandaoni, Godlove amesema licha ya changamoto anazopitia kwa sasa, tayari ameishi maisha ya utajiri ambayo wengi wanaomkejeli hawajawahi kuyaonja.Amejigamba kuwa aliwahi kuendesha magari makubwa na ya kifahari, akisisitiza kuwa uzoefu huo hauwezi kufutwa na anguko la muda. Tajiri huyo mwenye majigambo, ameenda mbali zaidi na kujinadi kuwa yeye ndiye kijana mwenye ushawishi mkubwa zaidi barani Afrika, akisema ana ushawishi na uwezo wa kifedha unaomzidi hata staa wa kimataifa IShowSpeed. Godlove pia amewashambulia wanaume wanaofurahia anguko lake kiuchumi, akiwataka waache uvivu na badala yake wajikite katika kuwahudumia wapenzi wao na kujitafutia maisha bora. Katika kauli iliyozua taharuki zaidi, bilionea huyo amewatuhumu mashabiki wake kwa kuwaita maskini, huku akiahidi kuwa atakaporejea katika hali nzuri ya kifedha, yuko tayari kuwapa pesa za bure kama ishara ya kuthibitisha uwezo wake.

Read More
 Chiefgod Love Atoa Onyo Kali kwa Wanaume Wazembe

Chiefgod Love Atoa Onyo Kali kwa Wanaume Wazembe

Mwanamitandao anayefahamika kwa jina la Chief Godlove amezua mjadala mkubwa mitandaoni baada ya kutoa kauli tata akiwalenga wanaume anaodai hawawajibiki kwa wake zao wala kutimiza mahitaji ya msingi ya kifamilia. Kupitia ujumbe alioutoa kwenye mitandao ya kijamii, Chiefgod Love amesema amechoshwa na wanaume anaowataja kuwa wazembe na wasiojua kuwajibika, akidai kuwa endapo wataendelea kupuuza majukumu yao, yuko tayari kuwaingilia kimapenzi wake zao. Chief Godlove amejinadi kuwa ana mali nyingi ikiwemo pesa na magari, akisisitiza kuwa itakuwa ni jambo la aibu kwa wanaume hao kumuacha kijana mdogo kama yeye achukue nafasi yao kwa sababu ya uzembe wao wenyewe. Kauli hiyo imekuja siku chache baada ya Chief Godlove kunukuliwa akidai kuwa anatumia nguvu ya jicho la tatu, na kwamba mizimu imemruhusu kushiriki masuala ya kimapenzi nje ya mipaka ya kawaida. Aidha, alidai kuwa kuanzia mwakani ataanza kuishi maisha hayo kwa mujibu wa imani zake za kiroho.

Read More
 Chief Godlove Akanusha Kutoka Kimapenzi na Pipi Jojo

Chief Godlove Akanusha Kutoka Kimapenzi na Pipi Jojo

Mwanamitandao maarufu Chief Godlove amejitokeza kukemea madai yanayoenezwa mtandaoni yakidai kuwa ana uhusiano wa kimapenzi na msanii wake mchanga, Pipi Jojo. Katika video aliyoipakia Instagram, Chief Godlove ameonyesha kukerwa na taarifa hizo, akieleza kuwa zinamkosea heshima na msanii huyo ambaye ni mtoto wa umri wa miaka 16. Chief Godlove amesema kuwa ukaribu wake na msanii huyo unatokana na majukumu yake ya kumlea kimuziki na kumsaidia kukua katika tasnia, na si kutokana na sababu za kimapenzi kama inavyodaiwa mtandaoni. Chief Godlove pia amethibitisha kuwa siku ikifika, atatambulisha mke wake ili kuzima uvumi huo, akionyesha kuwa anahitaji kulinda faragha ya Pipi Jojo kutokana na umri wake mdogo. Tuhuma hizi zilianza kusambaa baada ya Chief Godlove kumpeleka Pipi Jojo kwenye sherehe ya yacht iliyolenga kusherehekea mafanikio yake mapya tangu alipotambulishwa rasmi kwenye muziki.

Read More
 Chief Godlove Awaponda Wanaouliza Chanzo cha Utajiri Wake

Chief Godlove Awaponda Wanaouliza Chanzo cha Utajiri Wake

Mshawishi wa mitandao ya kijamii, anayejulikana kama Billionaire Chief Godlove, ameibua ghadhabu na mjadala mkali baada ya kuchapisha ujumbe wenye utata uliojaa dharau na kejeli dhidi ya wafuasi wake wanaohoji kuhusu utajiri wake. Katika ujumbe huo uliowekwa kwenye mtandao wa Instagram, mwanamitandao huyo ameonekana kuwadharau wafuasi wake, akijibu maswali ya mara kwa mara kuhusu chanzo cha pesa zake kwa madai kuwa utajiri ni sehemu ya utambulisho wake wa asili na si jambo analolitafuta au kulifanyia kazi mahali pengine. Godlove amewapa tahadhari wanaomkosoa, akiwataka kupunguza wivu, hasira, na mihemko isiyo na msingi. Ameeleza wazi kwamba wengi wanaomkosoa hawana msingi wa kufanya hivyo kutokana na hali zao duni za kiuchumi, kauli ambazo zimewafanya baadhi ya wafuasi kuhisi amewazungumzia kwa dharau kubwa na kuwaita maskini. Sanjari na hilo, amechochea mjadala kwa kuwaambia wafuasi wake waweke akaunti zao ili awape pesa, akionyesha mtazamo wa kuwadhihaki wale anaodai kuwa wanapitia changamoto za kifedha.

Read More
 Chief Godlove Atangaza Kutafuta Mke

Chief Godlove Atangaza Kutafuta Mke

Mwanamitandao maarufu kutoka nchini Tanzania, Chief Godlove, ametangaza harakati zake za kutafuta mke baada ya kumtambulisha binti yake wa pili kutoka Kenya. Kupitia ukurasa wake wa mitandao ya kijamii, Chief Godlove amesema wazi kuwa anahitaji mwanamke mrembo kuliko mabinti zake, akitoa sababu kuwa uzuri huo unapaswa kuendana na uwezo wa kumhudumia na kuwatunza watoto wake. Godlove, amesema kuwa anataka mke atakayekuwa na utu, uvumilivu na sura ya kuvutia, akisisitiza kuwa uzuri kwa upande wake unapaswa kuwa wa hali ya juu kuliko ule wa mabinti zake ili kuendana na hadhi ya familia yake. Chief Godlove, ambaye mara nyingi hujulikana kwa utani na kauli zinazosisimua mijadala, amesisitiza kuwa anachotafuta ni mwanamke mwenye mvuto, upendo na uwezo wa kuleta utulivu katika maisha yake na ya watoto wake. Kwa sasa, mashabiki wake bado wanangoja kuona kama tangazo hili litageuka kuwa safari rasmi ya kumtafuta mke, au kama ni sehemu ya maudhui yake yanayovutia watazamaji mtandaoni.

Read More
 Chief Godlove Achanganyikiwa Baada Ya Msanii Wake Kumkatia Mauno  

Chief Godlove Achanganyikiwa Baada Ya Msanii Wake Kumkatia Mauno  

Msanii chipukizi kutoka Tanzania Pipi Jojo, ameibua mjadala mkubwa mitandaoni baada ya video yake kusambaa ikimuonyesha akicheza kwa mitindo ya kimahaba mbele ya bosi wake Chief Godlove, ambaye alikuwa ameketi sebuleni akitazama runinga. Katika video hiyo, Pipi Jojo alionekana akikata mauno kwa ustadi na hisia kali huku akimuangalia moja kwa moja Chief Godlove, jambo lililowafanya baadhi ya mashabiki kuanza kuhoji aina ya uhusiano uliopo kati yao. Wengi wamehoji kama kweli ni uhusiano wa kazi pekee au kuna ukaribu zaidi, hasa ikizingatiwa kwamba msanii huyo amekuwa akimuita Chief Godlove “baba” kwenye mahojiano na machapisho yake ya mitandaoni. Hata hivyo, baadhi ya mashabiki wamemtetea Pipi Jojo wakisema video hiyo ilirekodiwa kama sehemu ya promo ya “Chakacha Challenge”, iliyoanzishwa na Chief Godlove kuhamasisha watu kucheza wimbo huo ambapo washindi wanatarajiwa kujinyakulia zawadi nono ikiwemo milioni 5 kwa mshindi wa kwanza.

Read More