Mwanamitandao anayefahamika kwa jina la Chief Godlove amezua mjadala mkubwa mitandaoni baada ya kutoa kauli tata akiwalenga wanaume anaodai hawawajibiki kwa wake zao wala kutimiza mahitaji ya msingi ya kifamilia.
Kupitia ujumbe alioutoa kwenye mitandao ya kijamii, Chiefgod Love amesema amechoshwa na wanaume anaowataja kuwa wazembe na wasiojua kuwajibika, akidai kuwa endapo wataendelea kupuuza majukumu yao, yuko tayari kuwaingilia kimapenzi wake zao.
Chief Godlove amejinadi kuwa ana mali nyingi ikiwemo pesa na magari, akisisitiza kuwa itakuwa ni jambo la aibu kwa wanaume hao kumuacha kijana mdogo kama yeye achukue nafasi yao kwa sababu ya uzembe wao wenyewe.
Kauli hiyo imekuja siku chache baada ya Chief Godlove kunukuliwa akidai kuwa anatumia nguvu ya jicho la tatu, na kwamba mizimu imemruhusu kushiriki masuala ya kimapenzi nje ya mipaka ya kawaida. Aidha, alidai kuwa kuanzia mwakani ataanza kuishi maisha hayo kwa mujibu wa imani zake za kiroho.