Chris Brown Akana Mashtaka ya Kumpiga Mtu kwa Chupa Klabuni London

Chris Brown Akana Mashtaka ya Kumpiga Mtu kwa Chupa Klabuni London

Msanii maarufu wa muziki wa R&B kutoka Marekani, Chris Brown, amekana mashtaka ya jaribio la kushambulia kwa kutumia chupa yaliyowasilishwa dhidi yake katika mahakama ya Uingereza. Brown alifika mbele ya mahakama jijini London, na kujitetea kuwa hana hatia katika tukio linalodaiwa kutokea kwenye klabu ya Tape iliyoko Mayfair, Februari 19, 2023. Kwa mujibu wa taarifa za vyombo vya habari, Brown anatuhumiwa kumshambulia mtayarishaji wa muziki, Abraham Diaw, kwa kutumia chupa ya kileo aina ya tequila. Mashtaka hayo yanajumuisha kosa la kujaribu kusababisha madhara makubwa kwa mwili pamoja na kumiliki silaha hatari ambayo katika kesi hii ni chupa yenyewe. Chris Brown, mwenye miaka 35, alikamatwa mwezi Mei 2025 huko Manchester alipokuwa nchini Uingereza kwa shughuli za muziki. Alizuiliwa kwa muda wa wiki moja kabla ya kupewa dhamana ya pauni milioni tano (£5m) huku akizuiwa kusafiri nje ya Uingereza isipokuwa kwa ruhusa maalum kutoka mahakama. Mshtakiwa mwenzake katika kesi hiyo, rapa Omololu Akinlolu anayefahamika pia kama HoodyBaby, naye amekana mashtaka dhidi yake. Kesi yao imeahirishwa hadi Mei 2026 kwa kusikilizwa tena, huku tarehe rasmi ya kusikilizwa kwa kesi kamili ikipangwa kuwa Oktoba 26, 2026. Mashahidi wanatarajiwa kutoa ushahidi wakitumia picha za kamera za usalama zilizorekodi matukio ndani ya klabu. Aidha, Abraham Diaw amewasilisha kesi ya madai akitaka fidia ya pauni milioni 12 kwa majeraha na madhara aliyoyapata. Chris Brown, ambaye tayari ana historia ya kesi za ukatili na ghasia ikiwemo ile ya mwaka 2009 dhidi ya mwimbaji Rihanna, anajikuta tena katika mzozo wa kisheria unaoweza kuathiri sana kazi yake ya muziki na sifa yake ya kimataifa. Kwa sasa, Brown yuko nje kwa dhamana na ameahidi kushirikiana na vyombo vya sheria ili kuthibitisha kuwa hakuhusika katika tukio hilo.

Read More
 Chris Brown Aahidi Kurejea Kwa Kishindo Kwenye Breezy Bowl Tour

Chris Brown Aahidi Kurejea Kwa Kishindo Kwenye Breezy Bowl Tour

Mwanamuziki nyota kutoka Marekani, Chris Brown, amevunja ukimya kwa mara ya kwanza baada ya kuachiwa kwa dhamana mapema leo, akieleza kuwa yuko tayari kuendelea na ratiba ya onyesho lake kubwa la Breezy Bowl linalotarajiwa kuanza Juni 13 jijini Manchester, Uingereza. Kupitia ujumbe aliouweka kwenye mitandao ya kijamii, Chris Brown aliandika:  “Kutoka kifungoni mpaka kwenye Jukwaa la Breezy Bowl,” kauli iliyowasisimua mashabiki wake duniani kote. Taarifa za awali zilieleza kuwa msanii huyo alikumbwa na mkasa wa kuwekwa rumande kwa muda, hali iliyozua sintofahamu kuhusu mustakabali wa ziara yake ya kimuziki barani Ulaya. Hata hivyo, kwa mujibu wa ujumbe wake, Brown ameweka wazi kuwa yuko huru na amejipanga vilivyo kwa ajili ya tamasha hilo ambalo limekuwa likisubiriwa kwa hamu kubwa na mashabiki. Chris Brown, anayefahamika kwa uwezo wake wa kipekee wa kuimba, kucheza na kutumbuiza jukwaani, anatarajiwa kufanya maonyesho katika miji kadhaa barani Ulaya kupitia ziara ya Breezy Bowl, ambayo ni sehemu ya kampeni ya kuendeleza album yake ya hivi karibuni na kusherehekea mafanikio yake ya kimuziki. Mashabiki nchini Uingereza na sehemu nyingine za dunia sasa wana kila sababu ya kuwa na matumaini kuwa tamasha hilo litaendelea kama ilivyopangwa, huku Chris Brown akiahidi kuwaletea burudani ya hali ya juu licha ya changamoto zilizojitokeza.

Read More
 Chris Brown Aachiliwa kwa Dhamana ya Dola Milioni 6.7 London

Chris Brown Aachiliwa kwa Dhamana ya Dola Milioni 6.7 London

Msanii mashuhuri wa R&B kutoka Marekani, Chris Brown, ameachiwa kwa dhamana ya dola milioni 6.7 (takriban Shilingi bilioni 1) na mahakama mjini London baada ya kufunguliwa mashtaka ya kushambulia mtu bila sababu katika kilabu usiku mnamo mwaka 2023. Chris Brown mwenye umri wa miaka 36, ambaye ameshawahi kushinda tuzo ya Grammy, bado hajaombwa kutoa ombi la kukiri au kukataa shtaka hilo. Hata hivyo, masharti ya dhamana yake yanamruhusu kuanza ziara yake ya kimataifa mwezi ujao kama ilivyopangwa awali. Msanii huyo alikamatwa wiki iliyopita na baadaye kushtakiwa kwa kosa la kujeruhi kwa makusudi, kufuatia tukio ambalo inadaiwa alimshambulia mtayarishaji wa muziki kwa chupa ya kileo aina ya tequila. Jaji Tony Baumgartner alisema kuwa Brown anaruhusiwa kuendelea na ziara yake, ikijumuisha maonesho kadhaa nchini Uingereza, lakini lazima alipe dhamana hiyo ili kuhakikisha atahudhuria kesi yake mahakamani. Tukio hilo limezua mjadala mkubwa miongoni mwa mashabiki na wanamuziki wenzake, huku wengi wakisubiri kwa hamu kuona hatima ya kesi hiyo inayomkabili mmoja wa wasanii wenye ushawishi mkubwa duniani.

Read More
 Chris Brown Ashikiliwa Rumande Hadi Juni 13 kwa Tuhuma za Kujaribu Kumdhuru Mtayarishaji wa Muziki

Chris Brown Ashikiliwa Rumande Hadi Juni 13 kwa Tuhuma za Kujaribu Kumdhuru Mtayarishaji wa Muziki

Msanii maarufu wa muziki wa R&B kutoka Marekani, Chris Brown, ataendelea kushikiliwa rumande hadi tarehe 13 Juni 2025, akisubiri kufikishwa tena mahakamani kufuatia tuhuma za kushambulia kwa makusudi. Chris Brown anadaiwa kumshambulia mtayarishaji wa muziki Abraham Diaw kwa kutumia chupa katika kilabu cha usiku jijini London mnamo Februari 2023.Tuhuma hizo zinahusiana na kosa la kusababisha madhara makubwa ya mwili kwa nia ovu (grievous bodily harm with intent), ambalo ni miongoni mwa makosa makubwa kisheria nchini Uingereza. Hadi sasa, Brezzy hajatoa tamko rasmi kuhusu tukio hilo, huku wakili wake akisisitiza kuwa msanii huyo ataendelea kushirikiana na vyombo vya sheria hadi ukweli utakapobainika. Mashabiki na wadau wa muziki duniani kote wanafuatilia kwa karibu maendeleo ya kesi hii, ambayo huenda ikaathiri ratiba na kazi za kisanii za Brown kwa kiasi kikubwa.

Read More
 Chris Brown Akamatwa Jijini Manchester kwa Tukio la Mwaka 2023

Chris Brown Akamatwa Jijini Manchester kwa Tukio la Mwaka 2023

Msanii nyota wa muziki wa R&B kutoka Marekani, Chris Brown, ameripotiwa kukamatwa jijini Manchester, Uingereza, muda mfupi baada ya kutua nchini humo kwa ndege binafsi (private jet). Kwa mujibu wa taarifa kutoka vyombo vya usalama, maafisa wa Metropolitan Police (Met) walimkamata msanii huyo mara baada ya kubaini uwepo wake jijini humo. Kukamatwa kwake kunahusishwa na tukio la mwaka 2023, ambapo alidaiwa kumpiga kwa chupa ya mvinyo mtayarishaji wa muziki wa London aitwaye Abe Diaw, kitendo kilichosababisha majeraha makubwa hadi kusababisha kupoteza fahamu kwa muda. Chris Brown kwa sasa anazuiliwa katika kituo cha polisi kwa ajili ya mahojiano ya kina, huku uchunguzi ukiendelea kubaini mazingira kamili ya tukio hilo. Baada ya tukio hilo la mwaka jana, Abe Diaw alimfungulia Chris Brown kesi ya madai, akitaka alipwe fidia ya takribani dola milioni 16 za Marekani (zaidi ya shilingi bilioni 2.1 za Kenya), kwa madai ya majeraha ya kudumu, usumbufu wa kisaikolojia na kupoteza mapato kutokana na kushindwa kuendelea na kazi ya muziki kwa muda. Mpaka sasa, Chris Brown bado hajatoa taarifa rasmi kupitia timu yake ya mawakili wala mitandao yake ya kijamii kuhusu kukamatwa kwake. Hii si mara ya kwanza kwa Chris Brown kukumbwa na matatizo ya kisheria. Licha ya mafanikio makubwa katika muziki, amewahi kujikuta matatani mara kadhaa kutokana na matukio ya fujo au unyanyasaji. Tukio hili jipya linaongeza orodha ndefu ya changamoto za kisheria zinazomwandama nyota huyo.

Read More
 Chris Brown Amkingia Kifua Tory Lanez, Wadau Wahoji Nia Yake Halisi

Chris Brown Amkingia Kifua Tory Lanez, Wadau Wahoji Nia Yake Halisi

Staa wa muziki kutoka Marekani Chris Brown ameendelea na juhudi zake za kumtetea msanii Tory Lanez, ambaye anahusishwa na tukio la kupigwa risasi mguu wa rapa Megan Thee Stallion. Katika hatua ya hivi karibuni, Kupitia ujumbe aliouandika kwenye Insta-stori, Chris alisisitiza kuwa Tory Lanez anapaswa kuachiliwa kutokana na kile alichokiita udhalimu wa kifungo kisichostahili. Hatua hii imezua maswali na mjadala miongoni mwa mashabiki na wadadisi wa tasnia ya muziki, huku wengine wakijiuliza ikiwa Chris anafanya hivi kwa nia ya kumsaidia Tory au kama ni hatua ya kurejesha heshima yake mwenyewe. Katika ujumbe wake, Chris alikiri kumsaidia Tory Lanez kifedha wakati alikumbwa na changamoto za kiuchumi, jambo ambalo lilizua maswali kuhusu uhusiano wa kifamilia na mshikamano kati ya wanamuziki hawa wawili. Katika muktadha huu, baadhi ya watu wanaona hatua ya Chris Brown kama njia ya kuonyesha uaminifu kwa Tory, ambaye anahusishwa na mashitaka ya kumpiga risasi Megan Thee Stallion miaka miwili iliyopita. Hata hivyo, kuna wengi wanaopinga msimamo wa Chris, wakisema kwamba hatua hii inakosa muktadha wa kijamii na kisheria, na kwamba kumtetea Tory Lanez kunashindwa kuzingatia athari za matendo hayo kwa Megan, ambaye alikumbwa na jeraha kubwa katika tukio hilo. Mashabiki na wadadisi wengi wanaona kuwa Chris anajikuta akikwepa dhamira ya maadili ya kijamii kwa kumtetea msanii ambaye, kwa kiasi kikubwa, ameonyesha kuwa na matatizo makubwa ya kijamii. Kwa sasa, msimamo wa Chris Brown unaendelea kuwa na maoni mseto miongoni mwa mashabiki na waandishi wa habari, huku mashabiki wa Megan Thee Stallion na wanaharakati wakionyesha hasira dhidi ya mtu yeyote anayeonekana kupuuza athari za unyanyasaji wa kijinsia. Hii ni kwa sababu mzozo huu wa kisheria umekuja wakati ambapo jamii inazidi kujikita katika kulinda haki za waathirika wa unyanyasaji na kupinga vitendo vya aina hii.

Read More
 Chris Brown hawakataza mashabiki zake kuvaa bandana ya nyekundu

Chris Brown hawakataza mashabiki zake kuvaa bandana ya nyekundu

Mwanamuziki Chris Brown amesema na mashabiki zake ambao wanatarajia kuja kwenye ziara yake ya muziki ambayo ametangaza itaanza baadaye mwaka huu. Hakutaka kueleweka vibaya, hivyo akautumia ukurasa wake wa instagram kufafanua jambo kwamba, hataki mashabiki zake waje wakiwa wamevalia vitambaa vyekundu maarufu kama “Red Bandannas” kama ambavyo wanapeana hamasa ya kuvaa hivyo. Breezy amewakataza mashabiki zake kufanya hivyo na kusema ni bora wavae Bandana za rangi ya Brown ili kutojiingiza kwenye matatizo. Kwa historia, Kitambaa hicho chekundu kinaashiria upande wa “Bloods” kikundi maarufu nchini Marekani ambacho kinahusishwa na matukio ya uhalifu, dawa za kulevya, wizi wa magari, mauaji na mambo yote ya kihalifu

Read More
 Chris Brown kufikishiwa kortini kwa tuhuma za kukwepa kodi

Chris Brown kufikishiwa kortini kwa tuhuma za kukwepa kodi

Mwanamuziki kutoka nchini Marekani Chris Brown anadaiwa kodi na mamlaka ya mapato nchini Marekani, ambapo inatajwa kuwa anadaiwa kiasi cha (USD 4 million) zaidi ya KSh. milioni 497 ambacho ni kiwango cha kodi ambayo hakulipa tangu mwaka 2022. Mamlaka hiyo ya mapato (IRS) inamtaka Breezy alipe deni hilo haraka iwezekanavyo, nyaraka za madai hayo zinaonesha tayari serikali imeorodhesha baadhi ya mali ikiwemo nyumba na biashara zake kuwa itazichukua ikiwa atashindwa kulipa kwa muda unaofaa

Read More
 Ngoma ya Chris Brown “Call Me Every Day” yafakisha mauzo ya GOLD Marekani

Ngoma ya Chris Brown “Call Me Every Day” yafakisha mauzo ya GOLD Marekani

Ngoma ya mwimbaji nyota duniani, Chris Brown “Call Me Every Day” ambayo amemshirikisha Wizkid imefanikiwa kuuza nakala zaidi ya 500,000 nchini Marekani na hivyo kufikia kiwango cha mauzo ya “GOLD”. Kwa mujibu wa Recording Industry Association of America (RIAA), Chris Brown yupo nafasi ya 11 kwenye orodha ya wanamuziki waliouza zaidi nyimbo zao kwenye majukwaa ya kidijitali nchini Marekani (Best selling digital singles artist) akiwa na jumla ya mauzo milioni 92. Mafanikio hayo yamemfanya Chris Brown kuwa mwimbaji wa kiume aliyetunukiwa Plaque nyingi za hadhi ya Gold kwenye nyimbo zake akimpiku marehemu Elvis Presley.

Read More
 Kelly Rowland amkingia kifua Chris Brown kwenye Tuzo za American Music Awards

Kelly Rowland amkingia kifua Chris Brown kwenye Tuzo za American Music Awards

Mwanamuziki Kelly Rowland amemkingia kifua Chris Brown mbele ya mashabiki ambao walianza kumzomea kwenye utoaji wa Tuzo za (American Music Awards) usiku wa kuamkia leo. Baada ya kumtangaza kama mshindi wa kipengele cha Msanii Bora wa R&B, Breezy hakuwepo ukumbini na Kelly alilazimika kumchukulia Tuzo hiyo, lakini wakati akizungumza, mashabiki walianza kumzomea. Kelly Rowland aliwakatisha na kuyasema mazuri ya Chris Brown. Utakumbuka siku chache kuelekea utolewaji wa Tuzo za American Music Awards, Waandaaji wa tuzo hizo waliifuta performance ya Chris Brown ambayo ilikuwa maalum kwa ajili ya kutoa heshima kwa Michael Jackson.

Read More
 CHRIS BROWN AKUBALI  JINA ALILOPEWA NA WANAIGERIA

CHRIS BROWN AKUBALI JINA ALILOPEWA NA WANAIGERIA

Mwanamuziki kutoka Marekani Chris Brown amelipokea kwa mikono miwili Jina la Ki-Nigeria ambalo amepewa na raia wa Taifa hilo “Oluwa Gbenga Breezy” baada ya kukubali kushiriki kwenye nyimbo nyingi za wasanii wa Nigeria lakini pia kutumia lafudhi yao kwenye verse zake. Kupitia insta story yake, Breezy amelipokea Jina hilo na kuonesha upendo kwa kuweka vikopa na emoji za kucheka. Hivi karibuni Breezy amekuwa akifanya Kolabo na wasanii wa Nigeria ikiwemo Lojay X Sarz (Monalisa REMIX), Fireboy DML (Diana) lakini pia Wizkid na Davido ambao amekuwa akishirikiana nao kila uchao.

Read More
 CHRIS BROWN MATATANI KWA KUKWEPA SHOW YAKE

CHRIS BROWN MATATANI KWA KUKWEPA SHOW YAKE

Taarifa zinanazidi kusambaa zikimuhusisha Msanii Chris brown kukimbia na pesa baada ya kughairi kutumbuiza huko Houston muda mchache baada ya kufanya Soundcheck. The shade room imeripoti kuwa, Mwanaharakati na Mfanya biashara kutokea Houston Bi.LeJuan Bailey yupo mbioni kumchukulia Breezy hatua za Kisheria iwapo atashindwa kurejesha Mkwanja alio kimbia nao ($1.1M) ambapo March,19 Brown alitakiwa kutumbuiza katika tambasha lililoandaliwa ili kuhamasisha uchangiaji fedha kwa ajili ya wakazi ambao nyumba zao ziliharibiwa wakati wa Kimbunga Ida. Mwanamama huyo Anasema alitimiza kila kitu ambacho CB alihitaji ikiwa ni pamoja na Kumkodishia ndege binafsi na kumpa kiasi cha Dolla za kimarekani 1.1M, lakini mzee baba baada tu ya kufanya Soundcheck likabaki vumbi lake.

Read More