CHRIS BROWN AACHIA RASMI ALBUM YAKE MPYA

CHRIS BROWN AACHIA RASMI ALBUM YAKE MPYA

Nyota wa Pop na RnB kutoka Marekani, msanii Chris Brown tayari ameachia album yake mpya iitwayo “Breezy” yenye jumla ya ngoma 24. Album hii mpya inakuwa ni album ya 10 kwa Chris Brown ikiifuata Indigo iliyotoka mwaka 2019. “Breezy” imewashirikisha wasanii kama Wizkid, Ella Mai, H.E.R., Lil Wayne, Blxst, Anderson .Paak, Jack Harlow, Tory Lanez na wengine.

Read More
 CHRIS BROWN ADAI DIDDY ALIKATAA KUMSAINI KWENYE LEBO YAKE YA MUZIKI

CHRIS BROWN ADAI DIDDY ALIKATAA KUMSAINI KWENYE LEBO YAKE YA MUZIKI

Mwanamuziki nyota kutoka Marekani Chris Brown kwenye mahojiano na Drink Champs ameweka wazi kwamba rapa mkongwe Diddy alikataa kumsaini kwenye Label yake ya “Bad Boy”, kipindi ambacho alikuwa na umri wa miaka 12. Breezy amesema kwa kipindi kile miaka ya 1993 na kuendelea, record label kubwa ilikua ya rapa Diddy, hivyo kukataliwa kwake hakukuweza kumkatisha tamaa kufikia ndoto zake. Chris brown kwa sasa yupo kwenye media tour kwa ajili kutangaza album yake mpya “Breezy”, pamoja na ziara yake ya muziki ambayo itazunguka kwenye miji 27 ya Kaskazini mwa Marekani, itaanza Julai 15 mwaka huu.

Read More
 ZIARA YA ONE OF THEM ONES YAMNYIMA USINGIZI CHRIS BROWN

ZIARA YA ONE OF THEM ONES YAMNYIMA USINGIZI CHRIS BROWN

Staa wa muziki kutoka Marekani Chris Brown ana zaidi ya miaka 17 kwenye huu muziki, amefanya matamasha mengi katika kipindi cha miaka yote hiyo lakini bado haijamfanya kulizoea Jukwaa. Breezy amefunguka kupitia Big Boy TV kwamba ziara yake ijayo pamoja na Lil Baby “One Of Them Ones” inamtia wasiwasi na kumnyima usingizi kabisa kwenye kuhakikisha anawapa furaha mashabiki ambao wamelipa pesa zao kuja kumtazama. Ziara hiyo ya muziki ambayo itazunguka kwenye miji 27 ya Kaskazini mwa Marekani, itaanza Julai 15 mwaka huu

Read More
 CHRIS BROWN AKIRI KUREKODI NYIMBO 250 KWA AJILI YA ALBUM YAKE MPYA

CHRIS BROWN AKIRI KUREKODI NYIMBO 250 KWA AJILI YA ALBUM YAKE MPYA

Staa wa muziki kutoka Marekani Chris Brown amefunguka kwamba alirekodi nyimbo 250 katika kipindi cha miaka mitatu ambayo alikuwa akiitayarisha Album yake mpya “Breezy” ambayo itaachiwa June 24 mwaka huu. Katika nyimbo hizo 250 ilibidi zipunguzwe na kupatikana 23 ambazo zimetokea kwenye Tracklist ya Album hiyo. Kwenye mahojiano na Big Boy TV, Breezy ameelezea mchakato wa kupunguza ngoma hizo ambapo amesema nyimbo nyingi zilikuwa zinafanana ‘sound’ hivyo ilimchukua muda kuchagua na kupata hizo 23 kwa ajili ya masikio ya mashabiki zake. Album yake ya mwisho “Indigo” ya mwaka 2019 ilikuwa na Jumla ya nyimbo 32 na baadaye ziliongezwa nyimbo zingine na kufikia 42. Chris Brown anafahamika kwa kuwa na maktaba ya  nyimbo nyingi, mwaka 2017 wakati aki-promote Album yake ‘Heartbreak on a Full Moon’ alimwambia Mtangazaji Ebro kwamba ana nyimbo 800 kwenye simu yake

Read More
 CHRIS BROWN AMPONGEZA RIHANNA NA MPENZI WAKE ASAP ROCKY KWA KUPATA MTOTO WA KIUME

CHRIS BROWN AMPONGEZA RIHANNA NA MPENZI WAKE ASAP ROCKY KWA KUPATA MTOTO WA KIUME

Moyo wa Chris Brown bado upo kwa Rihanna, hii ni baada ya kumpongeza Ex wake huyo kwa kupata mtoto wa Kiume pamoja na mpenzi wake Asap Rocky. Kupitia instastory yake kwenye mtandao wa Instagram Breezy ameandika ujumbe unaosomeka “Congratulations,” akiambatanisha na emoji za kushukuru huku pia akisindikiza na emoji ya mama mjamzito. Rihanna ambaye amejifungua mtoto wake wa kwanza wa kiume akiwa na umri wa miaka 34, Mei 13 mwaka huu, ripoti mbalimbali zinaeleza kwamba mtoto wake anaendelea vizuri ijapokuwa jina la mtoto huyo halijawekwa wazi. Mwaka 2009 Chris Brown alimpiga mwanadada Rihanna wakiwa kwenye gari na kumsababishia michubuko usoni kiasi cha kupelekea wawili hao kuvunja uhusiano wao wa kimapenzi. Hata hivyo Breezy alihukumiwa kifungo cha nje miaka 5 huku akiwa chini ya uangalizi pamoja na kufanya kazi za Kijamii.

Read More
 CHRIS BROWN MBIONI KUACHIA ALBUM YAKE MPYA

CHRIS BROWN MBIONI KUACHIA ALBUM YAKE MPYA

Staa wa muziki kutoka Marekani Chris Brown ametupasha juu ya ujio wa Album yake mpya “Breezy”. Kupitia ukurasa wake wa Instagram ameandika Album hiyo itatoka mwezi Juni mwaka huu. Hitmaker huyo wa ngoma ya “Go Crazy” hajaweka wazi orodha ya nyimbo wala wasanii walioshiriki kwenye album yake hiyo. Hii itakuwa Album yake ya 10 ikiifuata Indigo iliyotoka mwaka 2019.

Read More
 ASAP ROCKY AMTOLEA UVIVU CHRIS BROWN KUPITIA WIMBO WAKE MPYA D.M.B

ASAP ROCKY AMTOLEA UVIVU CHRIS BROWN KUPITIA WIMBO WAKE MPYA D.M.B

Rapa kutoka Marekani Asap Rocky amemchana Chris Brown kwenye wimbo wake mpya (D.M.B) ambao umetoka Mei 5 Mwaka huu. Kwenye moja ya verse katika ngoma hiyo, A$AP Rocky amesema “I don’t beat my b*tch, I need my b*tch.” akihusisha na tukio la Chris Brown kumpiga Rihanna mwaka 2009. Jina la wimbo huo limefupishwa kuwa (D.M.B) ikiwa na maana ya “DAT$ MAH B!*$H.” Utakumbuka mwaka 2009 Chris Brown alimpiga Rihanna wakiwa kwenye gari na kumsababishia michubuko usoni kiasi cha kupelekea wawili hao kuachana. Chris Brown alihukumiwa kifungo cha nje miaka 5 huku akiwa chini ya uangalizi pamoja na kufanya kazi za Kijamii.

Read More
 LIL BABY NA CHRIS BROWN MBIONI KUJA NA TAMASHA LIITWALO ONE OF THEM ONES

LIL BABY NA CHRIS BROWN MBIONI KUJA NA TAMASHA LIITWALO ONE OF THEM ONES

Wasanii kutoka marekani Chris Brown na Lil Baby wametangaza kuja na ziara ya pamoja ambayo wameipa jina la “One Of Them Ones”. Ziara hiyo itapita kwenye miji 27 nchini Marekani na imepangwa kuanza Julai 15 na kumalizika Agosti 27 mwaka huu. Kwa upande wa Chris Brown, ziara hii inakuja huku kukiwa na tetesi za ujio wa Album yake mpya iitwayo “Breezy” ambapo tayari ameachia mkwaju mmoja uitao ‘WE (Warm Embrace)’ na hajafanya ziara tangu mwaka 2019 alipofanya Indigo Tour. Kwa Lil Baby vile vile naye anatarajiwa kuachia Album mpya kwani tayari amedondosha ngoma mbili; ambazo ni  “Right On” na “In a Minute.”

Read More
 EX WA CHRIS BROWN, KARRUECHE TRAN AKANUSHA UVUMI WA KUTOKA KIMAPENZI NA QUAVO WA KUNDI LA MIGOS

EX WA CHRIS BROWN, KARRUECHE TRAN AKANUSHA UVUMI WA KUTOKA KIMAPENZI NA QUAVO WA KUNDI LA MIGOS

Mwiigizaji maarufu kutoka Marekani Karrueche Tran amepuzilia mbali uvumi wa muda mrefu kuwa anatoka kimapenzi na rapa Quavo wa kundi la Migos. Akiwa Mbele ya kamera za TMZ, Karrueche amekanusha madai hayo kwa kusema kwamba uhusiano wake na rapa huyo ni wa kirafiki tu na kwa sasa anafurahia maisha yake akiwa hana mpenzi yaani single! Uvumi wa Karrueche Tran kutoka kimapenzi na Quavo ulianza tangu mwaka 2017 baada ya kuwa na muendelezo wa kuonekana wakiwa pamoja mara kwa mara kwenye viwanja mbali mbali vya kukulia bata.

Read More
 MWANASHERIA WA KESI YA UBAKAJI INAYOMKABILI CHRIS BROWN AJITOA

MWANASHERIA WA KESI YA UBAKAJI INAYOMKABILI CHRIS BROWN AJITOA

Mwanasheria wa kesi ya ubakaji ambayo inamkabili Chris Brown ametangaza kujitoa kwenye shauri hilo. Ariel Mitchell amesema amejitoa kufuatia ushahidi wa sauti (voice note) pamoja na ujumbe mfupi ambazo chris brown alizianika hadharani zikionesha hakuwa na hatia. Ushahidi uliotolewa na Breezy ulimuanika wazi mwanamke huyo kuwa ndiye alikuwa akimuhitaji mwimbaji huyo wa R&B tofauti na madai yake. Mwanasheria huyo amesema mteja wake hakumueleza ukweli kabla ya kumfungulia mashtaka Chris brown kwani angefuta kesi dhidi ya msanii huyo. Chris Brown ameendelea kudai aombwe msamaha hadharani, lakini pia ameendelea kuvitaka vyombo habari kuripoti habari hii kama ambavyo waliripoti tuhuma zake.

Read More
 CHRIS ROWN AANIKA USHAHIDI DHIDI YA TUHUMA ZA UBAKAJI

CHRIS ROWN AANIKA USHAHIDI DHIDI YA TUHUMA ZA UBAKAJI

Staa wa muziki kutoka nchini Marekani Chris Brown ameamua kuanika ushahidi wa sauti ya mwanamke aliyemfungulia mashtaka ya ubakaji anayefahamika kwa jina la Jane Doe Mwanamke huyo alichukua headlines kwenye mitandao ya kijamii alipomtaka mwanamuziki huyo amlipe dolla milioni 20 kwa kile alichodai kuwa Chris Brown alimbaka kwenye Boti mwaka wa 2020. Sasa Chris Brown Ameweka wazi sauti ya Mwanadada huyo kupitia insta story yake kwenye mtandao wa Instagram akimlalamikia kuwa kwanini hajibu text zake huku akimtaka waonane naye, kitu ambacho Breezy anaamini ni mchongo wa kutaka kumuharibia jina na sio kitu kingine. “Unasoma SMS zangu na Bado hujaniblock nahisi Hunichukii Nataka tu kuonana na wewe tu tena ,Nijulishe kama unataka nikuache pekeako pia nitafanya,ila natamani tu kufanya mapenzi na wewe tena”..Sauti ya mwanamke huyo anasikika kwenye voice note aliyoshare Chris Brown kupitia Instagram Page yake.

Read More
 CHRIS BROWN AKANUSHA TUHUMA ZA UBAKAJI ZILIZOIBULIWA NA MWANAMKE MMOJA HUKO MAREKANI

CHRIS BROWN AKANUSHA TUHUMA ZA UBAKAJI ZILIZOIBULIWA NA MWANAMKE MMOJA HUKO MAREKANI

Mwanamuziki maarufu kutoka nchini Marekani Chris Brown ameibuka na kukanusha Taarifa  za kumbaka mwanamke mmoja huko Miami nchini Marekani Desemba 30 mwaka 2020. Kupitia instastory kwenye mtandao wa Instagram Breezy amepuuzilia mbali tuhuma hizo kwa kudai kuwa kila mara anapoachia kazi mpya watu hutengeneza mazingira ya kumchafulia jina. “I hope y’all see this pattern of [cap]. Whenever I’m releasing music or projects, ‘THEY’ try to pull some real b***t”. Ameandika Chris Brown. Kauli ya Breezy imekuja mara baada ya mwanamke ambaye hakutaka jina lake lifahamike kufungulia mashtaka ya ubakaji huku akidai fidia ya zaidi ya Bilioni 2.3 za Kenya kwani kitendo hicho kilimfanya apate matatizo ikiwemo mfadhaiko wa kihisia.

Read More