CHRIS BROWN ABURUZWA MAHAKAMANI KWA TUHUMA ZA UBAKAJI

CHRIS BROWN ABURUZWA MAHAKAMANI KWA TUHUMA ZA UBAKAJI

Mwanamuziki wa RnB kutoka Marekani Chris Brown amefunguliwa mashtaka ya ubakaji na mwanamke mmoja ambaye hakutaka jina lake lifahamike. Tukio hilo linadaiwa kutokea Disemba 30, mwaka 2020 kwenye boti iliyokuwa imepaki nje ya nyumba ya Diddy mjini Miami ambapo kulikuwa na party. Chris Brown anadaiwa kuwa alimualika mwanamke huyo kuja kwenye party kwa kupitia rafiki yake, na baada ya kuwasili, Breezy alianza kumtongoza na kumuuliza kama anataka kinywaji. Alienda jikoni na kumpatia mwanamke huyo kikombe chekundu kikiwa na kinywaji ambacho kimechanganywa na dawa za Kulevya. Baada ya kunywa kinywaji kile, mwanamke huyo alianza kuhisi kuishiwa nguvu na usingizi, ambapo Chris Brown alimtupa kitandani na kuanza kumbaka. Kwenye shtaka hilo mwanamke huyo anadai ($20 million) zaidi ya shillingi billioni 2.3 za Kenya kama fidia kwa matatizo ambayo Chris Brown amemsababishia ikiwemo mfadhaiko wa kihisia.

Read More
 CHRIS BROWN ADAIWA KUPATA MTOTO WA TATU NA MWANAMITINDO DIAMOND BROWN

CHRIS BROWN ADAIWA KUPATA MTOTO WA TATU NA MWANAMITINDO DIAMOND BROWN

Staa wa muziki kutoka nchini Marekani Chris Brown ameripotiwa kuwa amepata mtoto wa tatu na mrembo mwanamitindo aitwaye Diamond Brown ambaye ame-share taarifa hiyo kupitia ukurasa wake wa instagram. Mrembo huyo pia amelitaja jina la mtoto huyo wa Kike kuwa ni Lovely Symphani Brown. Jina la katikati la mtoto ‘Symphani’ limepelekea watu kuhisi Breezy ndio Baba wa mtoto huyo, kwani limefanana na jina la taasisi yake iitwayo Symphonic Love. Chris Brown tayari ana watoto wawili; Aeko Catori Brown mwenye umri wa miaka miwili, pia ana binti mkubwa Royalty mwenye umri wa miaka 8.

Read More
 CHRIS BROWN MBIONI KUPATA MTOTO WA 3 NA EX-GIRLFRIEND WAKE DIAMOND BROWN

CHRIS BROWN MBIONI KUPATA MTOTO WA 3 NA EX-GIRLFRIEND WAKE DIAMOND BROWN

Inatajwa kuwa huenda msanii Chris Brown akawa anatarajia kupata mtoto wake wa tatu, hii ni baada ya ex girlfriend wake mwanamitindo Diamond Brown kuonesha ujauzito wake na kuwa huenda akajifungua siku za hivi karibuni hii ni kwa mujibu wa tovuti ya rapup Bado mwanamitindo huyo hajaweka wazi kama Chris Brown ndiye baba wa mtoto huyo, lakini alithibitisha kuwa ni mjamzito kwa kupost misururu ya picha katika ukurasa wake wa Instagram. Hata hivyo nyota huyo wa RnB Chris Brown hajazungumzia suala hilo mahala popote pale kama ni kweli ama si kweli, lakini kama itakuwa ni kweli basi Breezy atakuwa na jumla ya watoto watatu kutoka kwa wanawake watatu tofauti.

Read More
 CHRIS BROWN AMUUNGA MKONO KYRIE IRVING KUKATAA KUCHANJWA

CHRIS BROWN AMUUNGA MKONO KYRIE IRVING KUKATAA KUCHANJWA

Chris Brown amemuunga mkono mcheza Kikapu Kyrie Irving ambaye amegoma kuchanjwa chanjo ya COVID-19. Kupitia Insta Stories yake kwenye mtandao wa Instagram Chris Brown amesema ana simama na nyota huyo wa Brooklyn Nets na kumuita shujaa wa ukweli. Kyrie Irving anaendelea kuvigusa vichwa vya habari duniani kwa kuigomea chanjo ya COVID-19 ambayo imefanywa kuwa lazima kwa wana michezo wote, hivyo kuweka hatiani mustakabali wake wa kucheza kwenye ligi hiyo hasa michezo ya nyumbani kwa sheria za Jiji la New York. Staa huyo ameitaja sababu ya kugoma kuchanjwa, akisema kuwa mtu hapaswi kulazimishwa kufanya jambo lolote kwenye mwili wake, na anasimama na wote ambao wanaamini kipi ni sahihi.

Read More