DIAMOND PLATINUMZ AZIKATAA TUZO ZA TANZANIA, ADAI ZINA UPENDELEO

DIAMOND PLATINUMZ AZIKATAA TUZO ZA TANZANIA, ADAI ZINA UPENDELEO

Mwanamuziki wa Bongofleva Diamond Platnumz ameweka wazi kwamba hatoshiriki kwenye tuzo za Tanzania zilizoandaliwa na Baraza La Sanaa nchini humo BASATA, akihoji kuwa kama wasimamizi wa tuzo hizo wameshindwa kumpatia Mirabaha ni vipi wataweza kumpatia tuzo. Kwenye mahojiano na The Switch ya Wasafi FM Diamond Platnumz ameeleza kuwa tuzo pekee anazozitaka na kuzikubali ni tuzo za upande wa digital platforms kwa kuwa tuzo hizo hazisemi uwongo. “Kimsingi Rais wetu Mh. Samia Suluhu ana nia njema sana ya kuwasaidia wasanii . Lakini kama kuna watu wamepewa nafasi huku chini kushughulikia mirabaha inabidi waangaliwe wasije kuitia Doa serikali na nia yao njema . Kwa mfano kama mrabaha tu huwezi kunipa je , tuzo utanipa ? “  Amesema Diamond Platnumz. Mbali na hayo Diamond amedai kuwa hakuzisikia tuhuma zilizotolewa na Harmonize kuwa amekuwa na tabia ya kumshusha kila msanii anayefanya vizuri kwa kusema kwamba hilo halina ukweli wowote kwani kila msanii ana nafasi ya kupata mafanikio yake na yeye haamini katika kuwafanyia figisu vijana wenzake. “Sikufuatilia kusikiliza, mimi kuna vitu huwa sitaki kufuatilia kusikiliza ila kama aliongea hivyo, unajua huwezi kumkataza mtu kuongea anachota kuongea, lakini WCB hatuna mkataba au system ya kumshusha mtu au kumnyonya mtu  Amesema Diamond. Hitmaker huyo wa ngoma ya Gidi ameendelea kwa kusema kuwa “Ikitokea mtu akinizungumzia vibaya zamani nilikuwa naumia sana ila sasa hivi nimekuwa napuuza, kwangu ni Baraka kwa sababu unaponizungumzia vibaya kwenye kitu ambacho sijakifanya unafanya Mwenyenzi Mungu anibariki zaidi, so sikutaka kufuatilia lakini mwisho wa siku kilichozungumzwa watu watajua ukweli upi na kwenye uongo watajua” . “Halafu mimi kufikia kwenye hatua ya kutaka kumzulumu mtu, kumshusha mtu, ni kwamba huamini katika wewe, mimi naami katika mimi sana ndio maana unaoka katika hii EP kuna kolabo chache sana.

Read More
 EP YA DIAMOND YAWEKA REKODI APPLE MUSIC TANZANIA

EP YA DIAMOND YAWEKA REKODI APPLE MUSIC TANZANIA

EP mpya ya msanii wa Bongofleva Diamond Platnumz, “First of All” inaendelea kufanya vizuri kupitia digital platforms mbalimbali. Good news kwa upande wa Apple Music ni kwamba EP hiyo yenye jumla ya ngoma 10, ngoma zake zote zinashika nafasi ya kwanza hadi ya kumi katika orodha ya Top Songs Tanzania. Nafasi ya kwanza imekamata wimbo uitwao “Melody” aliomshirikisha Jay Willz huku nafasi ya kumi ikishika kolabo yake na Mbosso, wimbo uitwao “Oka”. Ikumbukwe EP hiyo ambayo haijamaliza siku tatu tangu iachiwe, imefanikiwa kupata mapokezi makubwa zaidi ndani ya saa chache.

Read More
 DIAMOND PLATINUMZ AACHIA RASMI FIRST OF ALL EP

DIAMOND PLATINUMZ AACHIA RASMI FIRST OF ALL EP

Mwanamuziki wa Bongofleva Diamond Platinumz ameachia rasmi EP yake ya First Of All iliyokuwa ikisubiriwa kwa hamu na mashabiki zake. First Of All Ep ina jumla ya nyimbo 10′ ya moto ikiwa na kolabo 5 ambazo mbili kati ya hizo amefanya na wasanii wake kutoka WcB mbosso na zuchu ,huku akitoa shavu kwa mwanamuziki wa nigeria adekunle gold katika track namba 5 , track namba 10 akiwashirikisha wakali kutoka Afrika kusini na track namba 1 akimshirikisha msanii Jay Willz. Ep hiyo ambayo ni kwanza kwa mtu mzima Diamond Platinumz ina nyimbo kama Somebody, Fine, Melody, Sona, Loyal, Wonder, Mtasubiri, Fresh na Inapatikana Exclusive kupitia digital platforms mbali mbali za kupakua na kusikiliza muziki mtandaoni.

Read More
 DIAMOND PLATINUMZ AZUA GUMZO MTANDAONI KUPITIA VIDEO YA WIMBO WAKE WA GIDI

DIAMOND PLATINUMZ AZUA GUMZO MTANDAONI KUPITIA VIDEO YA WIMBO WAKE WA GIDI

Mwanamuziki kutoka nchini Tanzania Diamond Platnumz amekosolewa mitandaoni kwa kutumia bendera yenye utata katika video ya wimbo wake mpya wa Gidi. Moja ya kipande cha video katika wimbo wa Gidi kina bendera mbili za kibaguzi wa rangi zinazoonyeshwa wakati  Diamond akicheza huku nyingine akiwa na muonkeano wa Cowboy. Bendera hiyo ni ya kundi la Shirikisho la majimbo ya kusini ya Marekani ambayo yalipigania kudumisha utumwa wa watu weusi kati ya mwaka wa 1960 na 1961 na  inaonekana kama ishara ya mivutano ya ubaguzi wa rangi nchini Marekani. Jambo hilo limezua gumzo mtandaoni ambapo watumiaji wengi kwenye mitandao ya kijamii hasa wafrika wameshambulia Diamond Platinumz kwa hatua ya kutumia bendera hiyo ya kibaguzi kwenye video ya wimbo wake Gidi kwa sababu ina tafsiri ya moja kwa moja kwamba ameungana na wazungu katika kuwapiga vita ndugu zake Weusi. Hata hivyo wamemshauri msanii Diamond pamoja na uongozi wake kuhariri upya video hiyo na kutoa sehemu ambazo zina muonekano wa bendera hiyo kwani hili litakuwa jambo zuri tena la busara kwa msanii kama yeye ambaye analenga kupenya katika soko la muziki la Marekani.

Read More
 DIAMOND PLATINUMZ KUWABARIKI MASHABIKI ZAKE NA EP MPYA MWEZI MACHI MWAKA HUU

DIAMOND PLATINUMZ KUWABARIKI MASHABIKI ZAKE NA EP MPYA MWEZI MACHI MWAKA HUU

Mwanamuziki nyota wa BongoFleva Diamond Platnumz ametangaza kuachia EP yake ya kwanza tangu aanze muziki. Kupitia ukurasa wake wa instagram Diamond amesema kwamba EP hiyo ambayo hajaipa jina, itatoka March 4 mwaka huu. Hata hivyo hitmaker huyo wa ngoma ya “Gidi” bado haijaweka wazi idadi ya nyimbo zitakazopatikana kwenye EP hiyo ila ni jambo la kusubiriwa. Mwishoni mwa mwaka jana Diamond alisema albamu yake mpya ipo mbioni kutoka na itakuwa na nyimbo 12 ingawa atalazimika kuachia Extended Playlist (EP) kwanza kwa sababu tayari ana nyimbo 51 zilizokamika. Ikumbukwe kuwa EP hiyo pia itaachiwa siku moja kabla ya Tamasha la mwanamuziki Harmonize , Afro East Carnival linalo tarajiwa kufanyika March 5, 2022

Read More
 DIAMOND NA ZARI KUONEKANA NETFLIX MWEZI MACHI MWAKA 2022

DIAMOND NA ZARI KUONEKANA NETFLIX MWEZI MACHI MWAKA 2022

Msanii wa Bongofleva, Diamond Platnumz na baby mama wake, Zari The Bosslady ni miongoni mwa Mastaa wa Afrika watakaonekana katika mtandao wa Netfflix Machi 18, mwaka wa 2022. Netflix tawi la Afrika Kusini limetangaza Mastaa hao wataonekana katika documentary waliyoipa jina la Young, Famous & African. Ikumbukwe Diamond atakuwa Mtanzania mwingine kuonekana Netflix baada ya Idris Sultan ambaye Machi 26, mwaka 2021 alionekana kwenye mtandao huo kupitia filamu iitwayo ‘Slay’ iliyokutanisha Mastaa wa Afrika kama Ramsey Noah, Fabian Adeoye Lojede, na wengine wengi.

Read More
 DIAMOND PLATINUMZ AWEKA REKODI YA KUTUMBUIZA KWENYE SHOW MAALUM ILIYOANDALIWA NA GRAMMY

DIAMOND PLATINUMZ AWEKA REKODI YA KUTUMBUIZA KWENYE SHOW MAALUM ILIYOANDALIWA NA GRAMMY

Mwanamuziki wa Bongofleva Diamond Platnumz ameweka rekodi ya kuwa msanii wa kwanza kutoka Afrika Mashariki kutumbuiza kwenye show maalum iliyoandaliwa na waandaaji wa tuzo za Grammy Recording Academy inayokwenda kwa jina la Global Spin Show hiyo ambayo iliruka kwa njia ya mtandao kupitia akaunti za YouTube, Twitter, Facebook za recording academy ilianzishwa mwaka 2021 mwishoni kwa lengo la kuuibua na kuutangaza zaidi muziki wa Afro Beat K-Pop na Latin Music. Kwenye show yake hiyo Diamond Platnumz ameimba wimbo wake mpya kwa mara ya kwanza Gidi. Wimbo huo una maadhi ya AfroBeat huko Diamond akichanganya vionjo vya nyimbo mbalimbali kama Show You The Money ya Wizkid.

Read More
 ZUCHU AKANUSHA KUTOKA KIMAPENZI NA BOSI WAKE DIAMOND PLATINUMZ

ZUCHU AKANUSHA KUTOKA KIMAPENZI NA BOSI WAKE DIAMOND PLATINUMZ

Msanii wa Bongofleva Zuchu amekanusha fununu za kuwa amevalishwa pete ya uchumba na Familia ya Diamond Platnumz imepeleka barua ya uchumba kwenye familia yake. Akipiga na Wasafi FM  Zuchu pia Amekanusha madai ya kuishi nyumba moja na Boss wake Diamond Platnumz kwa kusema kuwa kila mtu anaishi nyumbani kwake. Sanjari na hilo amethibitisha kuwa yupo kwenye mahusiano na mwanaume ambaye hajamtaja jina lakini amemtaja kwa mwonekano kwa kusema kwamba ni mrefu ,ana rangi ya maji ya kunde,ni mfanya mazoezi,na mfanyabiashara. Sifa ambazo walimwengu kwenye mitandao ya kijamii wamejaribu kuziunganisha na mwonekano wa Diamond Platnumz ambaye  amekuwa akifanya sana mazoezi siku za hivi karibuni.

Read More
 DIAMOND PLATINUMZ AFIKISHA JUMLA YA SUBSCRIBERS MILLIONI 6 YOUTUBE

DIAMOND PLATINUMZ AFIKISHA JUMLA YA SUBSCRIBERS MILLIONI 6 YOUTUBE

Mwanamuziki wa Bongofleva Diamond Platnumz anazidi kujiwekea rekodi zake za kipekee kusini mwa Jangwa laSahara mara baada ya kufikisha jumla ya subscribers million 6 katika YouTube channel yake. Diamond platnumz ambaye amejiunga na mtando huo Jun 12, mwaka wa 2011 anaendelea kuwa msanii wa kwanza kutoka Kusini mwa Jangwa la Sahaara mwenye idadi kubwa ya subscribers, huku pia akiwa na rekodi ya watazamaji wa jumla yaani total view billioni 1.6. Lakini pia Diamond Platinumz anashikilia rekodi ya kuwa mwanamuziki mwenye wafuasi wengi katika mtandao wa Instagram Afrika Mashariki.

Read More
 DIAMOND ATAJWA KWENYE TUZO ZA MTV EUROPE MUSIC 2021

DIAMOND ATAJWA KWENYE TUZO ZA MTV EUROPE MUSIC 2021

Majina ya mastaa mbalimbali yametajwa kuwania tuzo za  Mtv Europe Music mwaka wa 2021 ambazo zitafanyika nchini Hungury mwishoni mwa mwaka huu. Kwenye orodha hiyo staa wa muziki kutoka Tanzania diamond platnumz ndiye msanii anayeiwakilisha Afrika Mashariki na kati. Diamond Platnumz ametajwa kwenye kipengele cha Best African Act ambapo atachuana na wakali wengine kutoka Afrika kama wizkid, tems, focalistic na amaarae kutoka nchini Ghana. Tuzo hizo zinatarajiwa kutolewa November 14,mwaka wa 2021 huko nchini Hungury. Justine Bieber ameongozwa kwa kutajwa kwenye vipengele vingi ambapo ametajwa kwenye vipengele nane.

Read More
 DIAMOND AONYESHA SAA YAKE MPYA YA ROLEX YENYE THAMANI YA SHILLINGI MILLIONI 2.8

DIAMOND AONYESHA SAA YAKE MPYA YA ROLEX YENYE THAMANI YA SHILLINGI MILLIONI 2.8

Staa wa bongofleva Diamond Platnumz ameamua kuzitumia ipasavyo pesa anazozitolea jasho. Mkali huyo wa Naanzaje ametumia kiasi cha dolla 25,000 ambazo ni zaidi ya shilling milioni 2.8  kwa pesa ya Kenya kununua saa mpya aina ya Rolex. Hii ni kwa mujibu wa risiti ya ununuzi wa saa hiyo ambayo aliishare kwenye insta story yake kwenye mtandao wa Instagram. Diamond Platnumz ambaye kwa sasa yupo nchini Marekani kwenye ziara yake ya kimuziki, alitembelea duka maarufu la Watch Empire huko Los Angeles na kujipatia saa hiyo yenye warantii ya miaka miwili. Diamond anaungana na mastaa kama Davido, Drake, Jay Z, Kanye West  ambao hupendelea kuvaa saa za aina ya Rolex.

Read More