Diamond Awataka Watanzania Waache Lawama kwa Serikali

Diamond Awataka Watanzania Waache Lawama kwa Serikali

Mwanamuziki nyota wa Bongo Fleva, Diamond Platnumz, ameibua gumzo baada ya kuwatolea uvivu watu wanaoendelea kulalamikia serikali kuhusu hali ya maisha. Kupitia ujumbe wake, Diamond amesisitiza kuwa wananchi wanapaswa kuongeza bidii kwenye kazi zao badala ya kuishia kuilaumu serikali kila mara. Hitmaker huyo wa Mtasubiri ameongeza kuwa changamoto za maisha ni za kawaida, na anayejituma hupata matunda yake bila kujali nani yupo madarakani. Diamond, ambaye mara nyingi hujitokeza kuzungumzia masuala ya kijamii, amesema ataendelea kuwatia moyo vijana kufanya kazi kwa bidii na kutumia vipaji vyao ipasavyo ili kuondokana na utegemezi. Kauli hiyo imezua mjadala mitandaoni, baadhi ya mashabiki wakimuunga mkono kwa kusema ujumbe huo ni wa kuhamasisha, huku wengine wakihisi amewabeza wananchi wanaopitia ugumu wa maisha.

Read More
 Diamond Platnumz Asema Maumivu ya Mapenzi Yalimjengea Ustaa

Diamond Platnumz Asema Maumivu ya Mapenzi Yalimjengea Ustaa

Mwanamuziki nguli wa Bongo Fleva, Diamond Platnumz, amefunguka kwa uchungu kuhusu changamoto alizopitia kabla ya kutamba kwenye muziki, akisimulia namna alivyoachwa na mpenzi wake kwa madai ya kutokuwa na uwezo wa kumuhudumia kifedha. Akipiga stori na podcast ya Telliswift, Diamond amekiri kuwa maumivu ya kuachwa ndiyo yaliyompa msukumo wa kuandika wimbo “Kamwambie”, uliompa umaarufu mkubwa na kufungua rasmi milango ya mafanikio katika muziki wake. Baada ya kuachia wimbo huo, alijipatia mashabiki lukuki na kufanikisha kushinda tuzo mbalimbali zilizomtambulisha rasmi katika tasnia ya muziki wa Bongo Fleva. Staa huyo amekiri kuwa safari yake haikuwa rahisi, kwani familia yake ilitoka kwenye hali ya umasikini mkubwa na ili kuendeleza ndoto zake, alilazimika kufanya kazi za mikono ili kujikimu kimaisha. Amefichua kwamba aliwahi kuuza nguo za mitumba, kufanya kazi katika kituo cha mafuta, na hata kujihusisha na upigaji picha, kazi ambayo wakati huo ilidharaulika sana. Hata hivyo, Diamond anasema hajawahi kusahau maumivu yaliyompa motisha ya kuandika wimbo wa “Kamwambie.” uliompa jina. Leo hii, Diamond Platnumz anahesabika kama moja ya wasanii wenye ushawishi mkubwa barani Afrika, lakini safari yake ya kufika hapo imetokana na maumivu, uvumilivu na bidii ya miaka mingi.

Read More
 Diamond Platnumz Aingilia Mzozo Kati ya Babalevo na Mbosso

Diamond Platnumz Aingilia Mzozo Kati ya Babalevo na Mbosso

Mzozo ulioshika kasi mitandaoni kati ya Babalevo na Mbosso kuhusu wimbo ‘Pawa’ umechukua mwelekeo mpya baada ya Diamond Platnumz kuingilia kati na kutoa msimamo wake. Babalevo na Mbosso walikuwa wakijibizana mitandaoni huku jina la Diamond likihusishwa kwenye malumbano hayo. Hata hivyo, kupitia ukurasa wake wa Instagram, Diamond ametoa kauli ya kutaka pande zote mbili kumheshimu, akisisitiza kuwa amekuwa akiwaheshimu na hana sababu ya kuhusishwa na migogoro yao. Diamond alimueleza Babalevo kuwa licha ya kumheshimu kama kijana mwenzake, maneno na mienendo yake yameanza kumpa hisia za kutilia shaka, hali inayoweza kupelekea kutojihusisha naye. Aidha, alimkumbusha Mbosso kuwa ana haki ya kukasirika au kujibu pale anapojisikia amekosewa, lakini akamtaka asiingize jina lake katika malumbano hayo, jambo ambalo amesema wameshazungumzia mara kadhaa huko nyuma. Hitimisho la ujumbe wake lilikuwa wito wa kuheshimiana, akieleza kwamba ikiwa wawili hao wana ajenda tofauti wanazopanga kupitia kivuli chake, basi waendelee, ila yeye hatashiriki.

Read More
 Diamond Platnumz Asema Hana Msemaji Rasmi

Diamond Platnumz Asema Hana Msemaji Rasmi

Mwanamuziki nyota kutoka Tanzania, Naseeb Abdul Juma, maarufu kama Diamond Platnumz, ametoa tamko rasmi akieleza kuwa hajawahi na hajateua mtu yeyote kuwa msemaji wa maisha yake binafsi au kazi zake za muziki. Kupitia taarifa hiyo, Diamond amesisitiza kuwa taarifa yoyote inayotolewa na mtu mwingine kwa niaba yake haina uhalali wowote na haitakiwi kuchukuliwa kama ya kweli. Ameeleza kuwa iwapo mtu yeyote ataamua kuamini taarifa hizo zisizo rasmi, basi matokeo ya imani hiyo yatakuwa juu ya mhusika mwenyewe, na yeye hatalaumiwa kwa lolote linalotokana na hilo. Ameweka wazi kuwa endapo kutakuwa na jambo lolote muhimu la kuzungumza, atazungumza mwenyewe kupitia njia rasmi bila kumtuma mtu yeyote kumwakilisha. Mashabiki na vyombo vya habari wanahimizwa kufuatilia vyanzo rasmi vya mwanamuziki huyo kwa taarifa sahihi na kuepuka upotoshaji. Tamko hili limekuja kufuatia hali ya sintofahamu iliyojitokeza kwa muda sasa, ambapo Baba Levo amekuwa akizungumza mara kwa mara kuhusu maisha ya ndani ya Diamond na kazi zake, hali iliyowafanya baadhi ya watu kumchukulia kama msemaji wake wa karibu.

Read More
 Diamond Apuuzilia Madai ya Wasanii wa Bongo Kukosa Dili za Kimataifa

Diamond Apuuzilia Madai ya Wasanii wa Bongo Kukosa Dili za Kimataifa

Staa wa muziki wa Bongo Fleva, Diamond Platnumz, ameonesha kutoridhishwa na hatua ya jina na picha yake kutumiwa na ukurasa maarufu wa mitandaoni nchini kwao, katika mjadala kuhusu kwa nini wasanii wa Tanzania hushindwa kusainiwa na lebo kubwa za kimataifa. Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Diamond amejibu vikali mada hiyo, akieleza kuwa amekuwa na mafanikio makubwa katika anga za kimataifa. Amesema amewahi kupokea ofa kutoka kwa lebo kubwa duniani kama Universal Music Group na Roc Nation, na hatimaye alisaini mkataba rasmi na Warner Music, unaokadiriwa kuwa na thamani ya shilingi bilioni 13.5 za Kitanzania. Msanii huyo ambaye pia ni mkurugenzi wa lebo ya WCB Wasafi, amesema mafanikio yake hayakuja kwa bahati bali ni matokeo ya bidii, maadili ya kazi na kujituma kwake. Ametaja kuwa amewahi kushirikiana na mastaa wa kimataifa kama Alicia Keys, Rick Ross, Ne-Yo, Omarion na wengine wengi, ishara kuwa anaheshimiwa na kutambuliwa hata nje ya mipaka ya Afrika. Kauli hiyo imeibua mjadala mpana mitandaoni, huku mashabiki wake wakimtetea vikali, wakisisitiza kuwa Diamond ni miongoni mwa wasanii wachache barani Afrika walioweza kuvuka mipaka ya bara na kupata nafasi katika jukwaa la kimataifa.

Read More
 Victoria Kimani Akanusha Kumlenga Diamond Katika Kauli Yake ya Rolls Royce

Victoria Kimani Akanusha Kumlenga Diamond Katika Kauli Yake ya Rolls Royce

Msanii wa muziki wa R&B kutoka Kenya, Victoria Kimani, hatimaye amejibu ukosoaji ulioibuka baada ya mahojiano yake kwenye Mic Cheque Podcast, ambako alitoa kauli iliyotafsiriwa na wengi kuwa ni dongo kwa msanii nyota wa Tanzania, Diamond Platnumz. Katika mahojiano hayo, Kimani alidai kuwa kuna Rolls Royce ya rangi ya buluu inayodaiwa kuwa ya bandia, kauli ambayo iliwafanya mashabiki wengi kuamini kuwa alikuwa akimlenga Diamond, ambaye hivi majuzi alijivunia kumiliki gari hilo la kifahari. Hata hivyo, akizungumza katika mahojiano na mtangazaji Milard Ayo, Victoria Kimani alikanusha madai hayo kwa kusisitiza kuwa hakuwa amemtaja mtu yeyote kwa jina. “Sikutaja jina la mtu yeyote… acheni. Nilisema nilichosema, haikuwa maana ya ndani,” alisema Kimani kwa msisitizo. Kauli hiyo ya Kimani imeibua mjadala mkali mitandaoni, huku baadhi ya mashabiki wakimtetea kwa kusema ana uhuru wa kutoa maoni yake, na wengine wakimtaka awe makini na matamshi yake, hasa inapohusiana na wasanii wengine wakubwa wa Afrika Mashariki. Diamond Platnumz hajatoa tamko rasmi kuhusiana na madai hayo, huku baadhi ya mashabiki wake wakimtetea vikali kwenye mitandao ya kijamii. Mashabiki sasa wanasubiri kuona iwapo kutakuwa na mwendelezo wa mvutano huu au kama pande zote zitapuuza na kuendelea na kazi zao za kisanaa.

Read More
 Victoria Kimani Amrushia Dongo Diamond Platnumz: Adai Rolls Royce ya Buluu Ni ya Bandia

Victoria Kimani Amrushia Dongo Diamond Platnumz: Adai Rolls Royce ya Buluu Ni ya Bandia

Mwanamuziki na mtunzi mashuhuri Victoria Kimani amezua gumzo mitandaoni baada ya kudokeza kuhusu gari la kifahari aina ya Rolls Royce linalodaiwa kuwa la bandia, ambalo linapigiwa debe katika ukanda wa Afrika Mashariki. Kwenye mahojiano yake hivi karibuni, Victoria alirusha dongo la chinichini kwa mtu mashuhuri ambaye hakumtaja moja kwa moja, akidai kuwa anajigamba na gari la kifahari lisilo halisi. “Si kila Rolls Royce ya buluu unayoiona mitaani ni halisi. Wengine wanapenda kuishi kwa kiki kuliko uhalisia,” alisema Kimani. Ingawa hakumtaja jina mhusika, mashabiki na wachambuzi wa mitandao walihisi kuwa ujumbe huo umeelekezwa kwa kwa staa wa Bongo Fleva, Diamond Platnumz ambaye hivi karibuni ameonekana mara kwa mara akipiga picha na gari la kifahari la rangi ya buluu katika hafla mbalimbali. Kauli ya Kimani imezua maoni mseto, baadhi wakimpongeza kwa kusema ukweli huku wengine wakimshutumu kwa kuanzisha mzozo usio na msingi. Wafuasi wa Diamond wamemkingia kifua msanii wao, wakisisitiza kuwa gari hilo ni halisi na lilinunuliwa kihalali. Diamond Platnumz bado hajajibu hadharani kuhusu suala hilo, lakini mijadala inaendelea kushika kasi mitandaoni huku mashabiki wakingoja kuona iwapo atatoa majibu au kulipuuza kabisa.

Read More
 Diamond Athibitisha Kuachia Albamu Mpya Mwezi Septemba 2025

Diamond Athibitisha Kuachia Albamu Mpya Mwezi Septemba 2025

Mwanamuziki nguli kutoka Tanzania, Diamond Platnumz, ametangaza rasmi kuwa albamu yake mpya inatarajiwa kutoka mwezi Septemba mwaka 2025. Akizungumza katika mahojiano maalum na jarida maarufu la Billboard, Diamond amesema maandalizi ya albamu hiyo yako katika hatua za mwisho. Diamond Platnumz, ambaye ameendelea kuwa mmoja wa wasanii wakubwa barani Afrika, amesema sababu ya kuchelewa kutoa albamu mpya ni uhitaji wa ubora wa hali ya juu katika kila wimbo utakaokuwemo ndani ya Albamu hiyo. Ameeleza kuwa analenga kuhakikisha kila ngoma kwenye albamu hiyo ni hit, jambo linalohitaji muda mwingi wa kufanya utafiti, uandishi wa mashairi na utayarishaji wa muziki. Kupitia mahojiano hayo, Diamond ameweka wazi kuwa hana haraka linapokuja suala la kutoa kazi ya muziki, kwani anaamini katika ubora kuliko haraka. Mashabiki wake wamepokea habari hizo kwa hamasa kubwa, wakisubiri kwa shauku ujio wa albamu hiyo ambayo inatarajiwa kuwa na ushirikiano wa kimataifa. Albamu hiyo ya Septemba 2025 inatarajiwa kuwa moja ya kazi kubwa zaidi kutoka kwa Diamond Platnumz, na kuongeza mchango wake katika kukuza muziki wa Bongo Flava kwenye jukwaa la kimataifa.

Read More
 Diamond Aonyesha Heshima kwa Jose Chameleone, Ataka Ushirikiano wa Mwaka

Diamond Aonyesha Heshima kwa Jose Chameleone, Ataka Ushirikiano wa Mwaka

Mwanamuziki nguli kutoka Tanzania, Diamond Platnumz, ametangaza nia yake ya dhati ya kushirikiana na msanii mkongwe wa Uganda, Jose Chameleone, katika wimbo mpya unaotarajiwa kutoka mwaka huu. Akiwa jukwaani katika tamasha la Coffee Marathon huko Ntungamo, Uganda, Diamond aliwajulisha mashabiki kuwa kolabo hiyo ni ndoto aliyokuwa nayo kwa muda mrefu, na sasa anafanya kila juhudi kuhakikisha inatimia. Diamond alisema kuwa licha ya mafanikio yake makubwa katika bara la Afrika, hajawahi kusahau mchango wa Jose Chameleone katika muziki wa Afrika Mashariki. Alimuelezea kama msanii aliyeathiri kizazi kizima na kumvutia hata yeye kuingia kwenye tasnia ya muziki. “Mwaka huu nataka kuhakikisha ninafanya wimbo na Jose Chameleone. Tunamshukuru Mungu kuwa anaendelea vizuri kiafya na tunamshukuru kwa mchango wake mkubwa kwenye muziki,” alisema Diamond mbele ya mashabiki. Kwa upande wake, Jose Chameleone, ambaye ametamba kwa zaidi ya miaka 20 na kubaki kuwa moja ya nguzo za muziki wa Afrika Mashariki, bado anaheshimika kwa nyimbo zake zenye ujumbe mzito na sauti ya kipekee. Kolabo kati ya Chameleone na Diamond inatarajiwa kuwa ya kihistoria, na tayari mashabiki kote kanda ya Afrika Mashariki wanasubiri kwa hamu kusikia kazi yao ya pamoja.

Read More
 Msanii Diamond Afunguka Kuhusu Kipaji Chake cha Kuandika Mashairi

Msanii Diamond Afunguka Kuhusu Kipaji Chake cha Kuandika Mashairi

Msanii nguli wa muziki wa Bongo Fleva, Diamond Platnumz, amefunguka wazi kuhusu kipaji chake cha kipekee katika uandishi wa nyimbo, akieleza kuwa hiyo ndiyo silaha yake kubwa katika mafanikio ya muziki wake. Kupitia mahojiano ya hivi karibuni, Diamond amesema ubora wake unajengwa zaidi na uwezo wake wa kuandika mashairi yenye hisia na ujumbe mzito, jambo ambalo limechangia kwa kiasi kikubwa kupendwa na mashabiki ndani na nje ya Tanzania. “Watu wengi wanajua tu napiga shoo, naimba, lakini ukweli ni kwamba uandishi wa mashairi ndiyo silaha yangu kubwa. Hapo ndipo nguvu yangu ipo,” amesema Diamond. Ameeleza kuwa mbali na nyimbo zake binafsi, amekuwa akiandika pia nyimbo kwa wasanii wengine, hususan wale walioko chini ya lebo yake ya WCB Wasafi, lakini pia amewahi kusaidia wasanii wa nje ya lebo hiyo. Hata hivyo, hakutaja majina ya wasanii au nyimbo alizohusika nazo, lakini amesisitiza kwamba mchango wake katika uandishi wa nyimbo umechangia mafanikio ya wengi kwenye tasnia. Kauli hiyo inazidi kuthibitisha nafasi yake kama mmoja wa wasanii waandamizi na wabunifu zaidi katika muziki wa Afrika Mashariki, huku akiendelea kushika nafasi ya juu kwenye chati mbalimbali za muziki barani Afrika.

Read More
 Harmonize amkingia Diamond kwa kukosa show nchini Rwanda

Harmonize amkingia Diamond kwa kukosa show nchini Rwanda

Msanii Harmonize ameonyesha uzalendo kwa kumuombea msamaha msanii mwenzake Diamond Platnumz huko nchini Rwanda kutokana na Diamond kushindwa kufika kwenye show aliyotakiwa aifanye December 23 mwaka jana jijini Kigali, pale BK Arena. Kwenye mahojiano aliyoyafanya na RwandaTV Harmonize mwishoni alikuwa akipewa shukurani ya kufika kwenye kipindi na akatumia nafasi hiyo kuomba msamaha kwa wanyarwanda kwa niaba ya Diamond Platnumz kwa kutokufika kwenye show. Kwenye maelezo yake alisema kuwa hajui tatizo lilikuwa nini lakini kwenye maisha huwezi kujua nini kinatokea hivyo aliwaomba wamsamehe ili tuupeleke muziki wetu wa Afrika Mashariki kwenye hatua inayofuata, japo hakulitaja jina la diamondplatnumz moja kwa moja hali iliyomfanya mtangaazaji kumuuliza ‘Unamaanisha Diamond?” na Harmonize alijibu “yeah yeah”.

Read More
 Diamond Platnumz apewe elimu ya kodi

Diamond Platnumz apewe elimu ya kodi

Staa wa Bongofleva Nasibu Abdul Juma maarufu Diamond Platnumz  amefanya kikao na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) hapo jana katika Ofisi za Makao Makuu ya Mamlaka hiyo Jijini Dar es salaam na kuzungumza kwa kina pamoja na kupata elimu juu ya kodi. Mwimbaji huyo ameandika kuhusu kikao hicho leo kwenye ukurasa wake wa Instagram kama ifuatavyo “Kikao kilienda vyema na nikapewa elimu mbalimbali ambazo zitaongeza ustawi bora wa Kampuni na biashara zetu lakini pia namna sahihi ya kuendelea kuchangia pato la Taifa” “Kipekee nimshukuru Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia kwa kutupa Serikali sikivu lakini pia nimshukuru Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Mwigulu na Kamishna Mkuu TRA Alphayo J. Kidata kwa kuendelea kuwa mstari wa mbele kwenye kuhakikisha kwamba TRA inaendelea kuwa Mlezi bora kwenye ustawi wa biashara na Wafanyabiashara” Kikao hiki kimetokana na mahojiano ya Diamond Platnumz Desemba 30, mwaka 2022 ambayo alilalamikia akaunti za Kampuni na zake binafsi kuzuiliwa kutokana na madeni ambayo TRA walisema wanamdai huku akisisitiza kuwa hakupenda jinsi alivyofuatwa kwenye Ofisi za Wasafi kitendo kilichomfanya ajione kama ni Mkimbizi ndani ya Nchi yake.

Read More