Meneja wa Diamond, Sallam SK ajibu disstrack ya Harmonize

Meneja wa Diamond, Sallam SK ajibu disstrack ya Harmonize

Meneja wa mwanamuziki Diamond Platnumz, Sallam SK amemjibu Harmonize kufuatia mashairi yake kwenye wimbo “Champion” alioshirikishwa na rapa Kontawa. Harmonize kwenye sehemu fupi ya wimbo huo aliimba kwamba, kwa sasa Konde Gang ni Jeshi la watu wawili akiwa na maana kwamba ni yeye na Ibraah pekee yaani baada Killy, Cheed na Anjella kujiondoa. Sallam ama Mendez leo Jumanne kupitia ukurasa wake wa Instagram amehoji kwamba, “Kwa hiyo kaua lebo kafungua kundi, wanajiita.. “Wagambo mtu mbili” au nimeelewa vibaya ” ameandika kupitia ukurasa wake. Utakumbuka tangu ameondoka WCB Wasafi, Harmonize hajawa na wakati mzuri na Lebo hiyo hasa Sallam SK ambaye mara kadhaa wameonekana kupisha kauli mtandaoni na hata walipokutana.

Read More
 Diamond Platnumz asema hawezi kumuoa Zuchu

Diamond Platnumz asema hawezi kumuoa Zuchu

Msanii nyota wa Bongofleva Diamond Platnumz ameamua kutoa ya moyoni baada ya meneja wake Babu Tale kumshinikiza amuoe Zuchu kutokana na video aliyoichapisha kwenye ukurasa wake Instagram akibusiana na hitmaker huyo wa “Sukari”. Kulingana na comment yake akimjibu Babu Tale, hawezi kumuoa msanii wake Zuchu kama ambavyo baadhi ya watu wamekuwa wakiamini. “Sasa nitamuoaje wakati ni Msanii wangu Bosi, hilo busu hapo lisiwatishe viongozi, ni salamu tu za Kijerumani” amesema Diamond. Utakumbuka wawili hao wamekuwa na ukaribu sana kiasi cha kuzawadiana zawadi jambo lililofanya baadhi ya watukuamini kuwa Diamond na Zuchu wapo katika mahusiano ya kimapenzi.

Read More
 DIAMOND PLATNUMZ AJIONDOA RASMI KWENYE TUZO ZA BONGO MUSIC AWARDS

DIAMOND PLATNUMZ AJIONDOA RASMI KWENYE TUZO ZA BONGO MUSIC AWARDS

Kampuni ya Millennium Stars Entertainment inayoratibu tuzo za Bongo Music Awards imepokea barua kutoka uongozi wa kampuni ya Wasafi Limited uliopendekeza kuondolewa kwenye mchakato wa Tuzo za Bongo Music Awards kwa msanii Diamond Platnumz kutokana na kuwa na ratiba ngumu itakayomzuia kupata muda wa kutosha kushiriki katika mchakato wa Tuzo za Bongo Music Awards 2022. Pamoja na mambo mengine uongozi wa Wasafi Limited wamepongeza na kushukuru kuona wapenzi wa muziki nchini Tanzania wamempendekeza kwa wingi msanii huyo. Kwa maana hiyo kampuni hiyo itamuondoa msanii Diamond Platnumz kwenye category zote alizokuwa amependekezwa muda wowote kuanzia sasa. Aidha, kampuni ya Millennium Stars Entertainment inaomba radhi kwa changamoto yoyote itakayojitokeza kwa mashabiki wa msanii Diamond Platnumz.

Read More
 LYNN AKIRI KUTOKA KIMAPENZI NA DIAMOND PLATNUMZ

LYNN AKIRI KUTOKA KIMAPENZI NA DIAMOND PLATNUMZ

Video vixen aliyegeukia muziki wa Bongofleva Lynn amemtaja ‘Simba’ kama ndiye Boyfriend wake kwa sasa. Jina la simba limeibua hisia mseto miongoni mwa mashabiki zake ambapo wengi wameenda mbali na kuhoji huenda mrembo huyo ana mahusiano na Diamond Platnumz ambaye amekuwa akitumia jina hilo. Katika hatua nyingine, Lyyn aliyetaja umri wake ni miaka 23, amesema hajawahi kuwa na mahusiano na msanii yeyote yule ingawa amekuwa akitongozwa sana na wasanii hao. Mrembo huyo ambaye kwa wakati mmoja amewahi kuwa kwenye mahusiano ya kimapenzi na msanii Tommy Flavour amefunguka hayo wakati akijibu maswali ya mashabiki wake kupitia mtandao wa Instagram.

Read More
 DIAMOND PLATNUMZ ADOKEZA KUMSAINI ASLAY WBC WASAFI

DIAMOND PLATNUMZ ADOKEZA KUMSAINI ASLAY WBC WASAFI

Moja kati ya vitu ambavyo Diamond Platnumz alivizungumza usiku wa kuamkia leo katika uzinduzi wa album mpya ya Barnaba “Love Sounds Different” ni kuhusiana na uwekezaji katika muziki hapa nchini unavyoyumba. Diamond ameeleza kwa undani namna wawekezaji wanavyosita kuingia katika muziki kwa sababu wakiangalia lebo kama WCB wakati fulani hali wanayoipitia hasa wasanii wake wakitaka kondoka inakua ni mshikemshike kitu ambacho Diamond amekisisitiza mbele ya Basata. Pia Diamond alimuongelea msanii aslayisihaka akisema kwamba ni mtu ambaye anamkubali na ana uwezo mkubwa sana na kama angekuwa chini ya usimamizi wake mwenyewe angefika mbali. “Kila mtu humu ndani anamjua Aslay, ana uwezo mkubwa sana, siongei kwa sababu niko hapa lakini Aslay angekuwa mikononi mwangu, asingekuwa huyu mnayemsikia, angefika mbali zaidi, au angepata mwekezaji mwingine hata kama siyo mimi, angefika mbali sana.” ameeleza Diamond Aidha, Aslay anatajwa kuwa ameshasaini na kampuni ya Sony Music na dili hilo lipo mbioni kutangazwa

Read More
 ZUCHU KULIPA MILLIONI 500 ZA KENYA KUONDOKA WCB

ZUCHU KULIPA MILLIONI 500 ZA KENYA KUONDOKA WCB

C.E.O wa WCB Wasafi, Diamond Platnumz ameweka wazi kuwa Zuchu kuondoka katika Lebo hiyo atalipa takriban shilingi milllioni 500 za Kenya. Kauli ya Diamond inakuja muda mfupi baada ya Babu Tale kutangaza Lebo hiyo itasaini wasanii wapya hivi karibuni. Kupitia ukurasa wake wa Instagram Babu Tale ameandika “Hivi karibuni tutasaini wasanii wawili kujiunga lebo ya Wasafi ila safari hii tumeamua msanii atakua na mashaidi wawili kutoka COSOTA na BASATA” “Music ni biashara yetu na ni jukumu letu kukuza na kusimamia hii kazi, hatuwezi kuacha hata iwe vipi” amesema Tale. Hadi sasa WCB iliyoanza kusaini wasanii tangu mwaka 2015, ina wasanii kama Diamond Platnumz, Queen Darleen, Lava Lava, Mbosso na Zuchu. Utakumbuka WCB Wasafi haijasaini msanii mpya tangu Aprili 2020 walipomtangaza Zuchu ambaye alikuwa msanii wa pili wa Kike ndani ya lebo hiyo.

Read More
 DIAMOND PLATNUMZ ATHIBITISHA KUNUNUA PRIVATE JET

DIAMOND PLATNUMZ ATHIBITISHA KUNUNUA PRIVATE JET

Staa wa muziki wa Bongofleva Diamond Platnumz amethibitisha kuwa tayari ameshanunua ndege yake binafsi, “Private Jet”. Diamond amethibitisha hilo kwenye mahojiano yake na DW nchini Ujerumani, akiwa na mtangazaji Josey Mahachie, ambapo alikuwa anamueleza namna staa anavyotakiwa kuishi ili kupata heshima anayostahili. Diamond amesema yeye ametoka mtaani, ameshanunua magari yenye thamani hadi Shilingi Bilioni 2.3 (Rolls Royce, Black Bedge), anasema inabidi ufanye hivyo, usipofanya hivyo hawatakuona wewe ni wa thamani na sasa tayari ana ndege binafsi. Itakumbukwa, kwa mara ya kwanza Diamond kueleza mpango wake wa kununua ndege yake binafsi ilikuwa ni miezi miwili iliyopita akizungumza na wanahabari nchini Ivory Coast alipoenda kwenye show yake, ambapo alisema ndege yake hiyo itatua nchini kabla ya mwezi Oktoba.

Read More
 DIAMOND PLATNUMZ ATAJWA KUWANIA TUZO ZA MUZIKI NCHINI GHANA

DIAMOND PLATNUMZ ATAJWA KUWANIA TUZO ZA MUZIKI NCHINI GHANA

Staa wa muziki wa Bongofleva Diamond Platnumz ametajwa kuwania tuzo za muziki kutoka Ghana, ziitwazo Ghana Entertainment Awards USA. Majina ya wanaowania tuzo hizo yalianza kutangazwa, Mei 13 mwaka huu ambapo hadi sasa Diamond anashindania kipengele kimoja kwenye tuzo hizo. Katika tuzo za Ghana Entertainment Awards USA kwenye msimu wake huu wa nne, Diamond Platnumz anang’ang’ania kipengele cha Best African Entertainer ambacho ni maalum kwa wasanii wote Afrika. Wanamuziki na watu wengine wanaoshindania kipengele hicho ni Davido, Wizkid, Burna Boy, Tems, Focalistic, na wengine wengi. Tuzo za Ghana Entertainment Awards USA kwa mwaka huu zinafanyika kwa mara ya nne, na zinatarajiwa kutolewa Julai 8, mwaka 2022 huko jijini New York, nchini Marekani.

Read More
 VIDEO YA WIMBO WA MTASUBIRI WA DIAMOND PLATINUMZ YAPIGWA MARUFUKU TANZANIA

VIDEO YA WIMBO WA MTASUBIRI WA DIAMOND PLATINUMZ YAPIGWA MARUFUKU TANZANIA

Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), imeagiza kusitishwa kwa video ya wimbo wa msanii Diamond Platnumz aliyomnshirikisha Zuchu “Mtasubiri” kutokana na kipande kinachomuonesha Zuchu akiimba kwaya kanisani na baadaye akaacha baada ya kupigiwa simu. TCRA imesema kipande hicho kimeibua ukakasi na hisia za dharau juu ya dini/madhehebu fulani, hivyo vyombo vyote vya utangazaji na mitandao ya kijamii nchini Tanzania vinatakiwa kutorusha video ya wimbo huo hadi pale Diamond Platnumz atakapo rekebisha sehemu hiyo ya video. Video ya wimbo “Mtasubiri” ilipandishwa kwenye mtandao wa Youtube Machi 29, mwaka huu

Read More
 SWIZZ BEATS KUHUSIKA KWENYE ALBUM MPYA YA DIAMOND PLATNUMZ

SWIZZ BEATS KUHUSIKA KWENYE ALBUM MPYA YA DIAMOND PLATNUMZ

Staa wa muziki a Bongofleva Diamond Platnumz anatarajia kuachia album yake ya nne katika maisha yake ya muziki baada ya kupata mafanikio makubwa na album ya ‘A Boy From Tandale’ mwaka wa 2017. Akizungumzia ujio wa album hiyo, amemtaja producer mkubwa wa muziki kutoka Marekani Swizz Beatz kuwa ndio mtayarishaji mkuu wa album yake ijayo (executive producer). Diamond ameeleza hayo akiwa nchini Uingereza kupitia Podcast ya Afrobeats inayoongozwa na Adesope. Huu unakuwa ni muendelezo wa Swizz Beatz kufanya kazi pamoja na Diamond, hivyo kumfanya mkali huyo wa wonder kuwa msanii wa kwanza Afrika kutayarishiwa album na Swizz Beatz. Mwaka 2020 Diamond Platnumz alishirikishwa kwenye album ya Alicia Keys, ‘ALICIA’ na kusikika kwenye wimbo uitwao Wasted Energy. Album hiyo ya Alicia ilitayarishwa na mumewe Swizz Beatz.

Read More
 AKAUNTI YA YOUTUBE YA DIAMOND PLATUMZ YAREJESHWA HEWANI

AKAUNTI YA YOUTUBE YA DIAMOND PLATUMZ YAREJESHWA HEWANI

Hatimaye youtube channel ya mwanamuziki wa Bongofleva Diamond Platnumz imerejea tena hewani katika mtandao wa youtube baada ya kufutwa na mtandao huo. Channel hiyo ambayo ina siku mbili tangu idukuliwe (hacked), mapema aprili 25 ilikuwa imeondolewa na youtube (terminated) kufuatia kukiuka masharti na kuvunja sheria zilizowekwa na youtube. Baada ya Akaunti yake ya Youtube kurejeshwa, Diamond platnumz amewashukuru wote walio hakikisha Akaunti hiyo inarudi hewani na kuwataka mashabiki zake kuendelea Kuitazama video yake mpya  Wonder Ambayo imerudi kwenye Trending namba 1 youtube kwa kuandika  “Thank you my Beloved my Youtube channel is back, Enjoy my brand new video #WONDER ” Akaunti hiyo imerudi kama ilivyokuwa hapo awali hakuna mabadiliko yoyote ikiwa na zaidi ya Subscribers milioni 6.5 na jumla ya watazamaji Bilioni 1.5. Ilikuwa na zaidi ya video 700.

Read More
 DIAMOND PLATINUMZ KUWASAJILI WASANII WAPYA WCB

DIAMOND PLATINUMZ KUWASAJILI WASANII WAPYA WCB

Mwanamuziki wa Bongofleva kutoka Diamond Platnumz ameweka wazi kwamba Mwaka huu kuna wasanii wapya ambao watatambulishwa ndani ya record label yaWCB. Katika mahojiano na kituo cha BBC Swahili nchini Uingereza Diamond amesema kwamba Mwaka huu kuna baadhi ya wasanii wataondoka katika lebo hiyo na kwenda kujiendeleza wenyewe. Hitmaker huyo wa ngoma ya “Mtasubiri” amedai kwamba atakuwa nao bega kwa bega mara baada ya kutoka katika Lebo hiyo na akaongezea kusema kuwa wcb haiwezi kuwa na wasanii wale wale kila siku. Tayari kauli yake hii inahusishwa na kitendo cha mwanamuziki Rayvanny siku chache zilizopita kufuta utambulisho wa kuwa mwanamuziki aliye chini ya usimamizi wa record label ya WcB katika ukurasa wake wa instagram.

Read More