Diamond Platnumz ataja sababu za kushindwa kutimiza ahadi ya kununua ndege
Msanii wa Bongofleva kutoka WCB Wasafi, Diamond Platnumz ametaja sababu za kushindwa kutimiza ahadi yake ya kushusha ndege binafsi pamoja na helikopta yake kabla ya kuisha kwa mwaka huu 2022. Akizungumza na Wasafi FM, Diamond amesema wakala aliyemtumia akimtaja kwa jina ‘Mr T’ ndiye aliyemfanya asitimize ahadi hiyo baada ya wakala huyo kushindwa kuleta ndege hizo licha ya kulipwa kila kitu. Kwa mujibu wake, kwa sasa wameamua kufikishana katika vyombo vya sheria na suala lao litashughulikiwa huko. Mapema mwaka jana, baada ya Diamond maarufu kama Simba kufanikisha ahadi yake ya kununua gari aina ya Rolls Royce Cullinan 2021, aliweka bayana nia yake ya kununua ndege binafsi.
Read More