VIDEO YA WIMBO WA MTASUBIRI WA DIAMOND PLATINUMZ YAPIGWA MARUFUKU TANZANIA

VIDEO YA WIMBO WA MTASUBIRI WA DIAMOND PLATINUMZ YAPIGWA MARUFUKU TANZANIA

Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), imeagiza kusitishwa kwa video ya wimbo wa msanii Diamond Platnumz aliyomnshirikisha Zuchu “Mtasubiri” kutokana na kipande kinachomuonesha Zuchu akiimba kwaya kanisani na baadaye akaacha baada ya kupigiwa simu. TCRA imesema kipande hicho kimeibua ukakasi na hisia za dharau juu ya dini/madhehebu fulani, hivyo vyombo vyote vya utangazaji na mitandao ya kijamii nchini Tanzania vinatakiwa kutorusha video ya wimbo huo hadi pale Diamond Platnumz atakapo rekebisha sehemu hiyo ya video. Video ya wimbo “Mtasubiri” ilipandishwa kwenye mtandao wa Youtube Machi 29, mwaka huu

Read More
 SWIZZ BEATS KUHUSIKA KWENYE ALBUM MPYA YA DIAMOND PLATNUMZ

SWIZZ BEATS KUHUSIKA KWENYE ALBUM MPYA YA DIAMOND PLATNUMZ

Staa wa muziki a Bongofleva Diamond Platnumz anatarajia kuachia album yake ya nne katika maisha yake ya muziki baada ya kupata mafanikio makubwa na album ya ‘A Boy From Tandale’ mwaka wa 2017. Akizungumzia ujio wa album hiyo, amemtaja producer mkubwa wa muziki kutoka Marekani Swizz Beatz kuwa ndio mtayarishaji mkuu wa album yake ijayo (executive producer). Diamond ameeleza hayo akiwa nchini Uingereza kupitia Podcast ya Afrobeats inayoongozwa na Adesope. Huu unakuwa ni muendelezo wa Swizz Beatz kufanya kazi pamoja na Diamond, hivyo kumfanya mkali huyo wa wonder kuwa msanii wa kwanza Afrika kutayarishiwa album na Swizz Beatz. Mwaka 2020 Diamond Platnumz alishirikishwa kwenye album ya Alicia Keys, ‘ALICIA’ na kusikika kwenye wimbo uitwao Wasted Energy. Album hiyo ya Alicia ilitayarishwa na mumewe Swizz Beatz.

Read More
 AKAUNTI YA YOUTUBE YA DIAMOND PLATUMZ YAREJESHWA HEWANI

AKAUNTI YA YOUTUBE YA DIAMOND PLATUMZ YAREJESHWA HEWANI

Hatimaye youtube channel ya mwanamuziki wa Bongofleva Diamond Platnumz imerejea tena hewani katika mtandao wa youtube baada ya kufutwa na mtandao huo. Channel hiyo ambayo ina siku mbili tangu idukuliwe (hacked), mapema aprili 25 ilikuwa imeondolewa na youtube (terminated) kufuatia kukiuka masharti na kuvunja sheria zilizowekwa na youtube. Baada ya Akaunti yake ya Youtube kurejeshwa, Diamond platnumz amewashukuru wote walio hakikisha Akaunti hiyo inarudi hewani na kuwataka mashabiki zake kuendelea Kuitazama video yake mpya  Wonder Ambayo imerudi kwenye Trending namba 1 youtube kwa kuandika  “Thank you my Beloved my Youtube channel is back, Enjoy my brand new video #WONDER ” Akaunti hiyo imerudi kama ilivyokuwa hapo awali hakuna mabadiliko yoyote ikiwa na zaidi ya Subscribers milioni 6.5 na jumla ya watazamaji Bilioni 1.5. Ilikuwa na zaidi ya video 700.

Read More
 DIAMOND PLATINUMZ KUWASAJILI WASANII WAPYA WCB

DIAMOND PLATINUMZ KUWASAJILI WASANII WAPYA WCB

Mwanamuziki wa Bongofleva kutoka Diamond Platnumz ameweka wazi kwamba Mwaka huu kuna wasanii wapya ambao watatambulishwa ndani ya record label yaWCB. Katika mahojiano na kituo cha BBC Swahili nchini Uingereza Diamond amesema kwamba Mwaka huu kuna baadhi ya wasanii wataondoka katika lebo hiyo na kwenda kujiendeleza wenyewe. Hitmaker huyo wa ngoma ya “Mtasubiri” amedai kwamba atakuwa nao bega kwa bega mara baada ya kutoka katika Lebo hiyo na akaongezea kusema kuwa wcb haiwezi kuwa na wasanii wale wale kila siku. Tayari kauli yake hii inahusishwa na kitendo cha mwanamuziki Rayvanny siku chache zilizopita kufuta utambulisho wa kuwa mwanamuziki aliye chini ya usimamizi wa record label ya WcB katika ukurasa wake wa instagram.

Read More
 DIAMOND MBIONI KUFANYA KOLABO NA RIHANNA

DIAMOND MBIONI KUFANYA KOLABO NA RIHANNA

Mwanamuziki wa Bongofleva Diamond Platnumz ametangaza kushirikiana na Rihanna kwenye Album yake ijayo. Akizungumza na BBC akiwa huko nchini Uingereza Diamond Platnumz amesema kuwa tayari ameshaweka mambo sawa kukamilisha kolabo na staa huyo mkubwa wa muziki duniani na anaamini itakuwa ni moja kati ya nyimbo kubwa kuwahi kutokea. “Napenda kufanya kazi na Rihanna, naona itakuwa nyimbo kali sana. Natumaini kama sio kwenye album yangu hii ijayo au nyingine tunaweza kushirikiana. Tumeshafanya mazungumzo toka mwaka jana kama sikosei. Anaweza kukosekana kwenye album hii kwasababu ya hali aliyonayo lakini kwa album inayofuata naamini tutakuwa pamoja”, amesema Diamond Diamond kwa sasa yupo nchini Uingereza kwa ajili ya kui-promote EP yake mpya FOA ambayo ameiachia wiki chache zilizopita.

Read More
 DIAMOND PLATNUMZ ADOKEZA UJIO WA ZIARA YA DUNIA YA EP YAKE FOA

DIAMOND PLATNUMZ ADOKEZA UJIO WA ZIARA YA DUNIA YA EP YAKE FOA

Staa wa Bongo Fleva, Diamond Platnumz ametangaza ujio wa ziara ya dunia kwa ajili ya kuitamgaza EP yake ya First Of All katika mataifa mbali mbali. Diamond amethibitisha hilo kupitia ukurasa wake wa Instagram ambapo ameipa ziara hiyo jina la FOA World Tour na inatarajiwa kuanza rasmi mwezi Mei’ mpaka Novemba mwaka huu. mahsusi kwa ajili ya FOA The EP pekee. Tour hiyo itaanza Mei 7, huko Ethiopia na kumalizika Novemba 26, mwaka 2022 nchini Sierra Leone. Katika taarifa yake Diamond Platnumz ameongeza kuwa ataendelea kutangaza tarehe za Ziara yake hiyo katika nchi Zingine. Ikumbukwe Diamond aliachia rasmi EP hiyo Machi 11, mwaka 2022 na mpaka sasa imefikisha streams zaidi ya milioni 30 kwenye platforms tofauti za kusikilizia muziki.

Read More
 DIAMOND PLATINUMZ ATANGAZA UZINDUZI WA VIDEO ZA FOA EP JUMATANO HII

DIAMOND PLATINUMZ ATANGAZA UZINDUZI WA VIDEO ZA FOA EP JUMATANO HII

Staa wa muziki wa Bongofleva Diamond Platnumz ametangaza rasmi uwepo wa tukio la uzinduzi wa video za nyimbo zote kumi zinazopatikana kwenye EP yake ya “First Of All” Diamond kupitia ukurasa wake wa Instagram ameeleza kuwa uzinduzi huo AMBAO NI kwa waalikwa tu utafanyika Machi 23,, Mlimani City jijini Dar es salaam “23. 03. 2022 #FOA VIDEOS PREMIERE! Cinemax Mlimani City, Invitees Only! Everything is Different in #FOAtheEP” – ameandika Diamond Platnumz Kando na hayo, ukiachilia mbali rekodi mbalimbali alizowahi kuweka Diamond, EP hiyo yenye mafanikio makubwa imeweza kuingiza nyimbo zake zote 10 zilizopo kwenye trending Youtube. Ikumbukwe Diamond aliachia rasmi EP hiyo Machi 11, mwaka 2022 na mpaka sasa imefikisha streams zaidi ya milioni 30 kwenye platforms tofauti za kusikilizia muziki mtandaoni.

Read More
 DIAMOND PLATINUMZ ATANGAZA UJIO MPYA WA QUEEN DARLEEN MWAKA 2022

DIAMOND PLATINUMZ ATANGAZA UJIO MPYA WA QUEEN DARLEEN MWAKA 2022

Baada ya kimya cha muda mrefu na stori za hapa na pale kuhusu uwepo wake ndani ya record label ya WcB , hatimae boss wa label hiyo Diamond Platnumz ameamua kuweka wazi juu ya ujio mpya wa first lady wa WCB Queen Darleen Kupitia insta story yake Diamond Platnumz ameshare sehemu ya video clip ikimuonesha Queen Darleen akiwa studio tayari kwa ajili ya maandalizi ya kazi mpya. Hitmaker huyo wa “Bachelor” ndiye msanii wa kwanza kwa kike kusainiwa na lebo ya WCB kisha baada ya miaka kadhaa ndipo akaja Zuchu. Utakumbuka hadi sasa Queen Darleen ndiye msanii pekee ambaye hajatoa albamu wala EP chini ya WCB Wasafi.

Read More
 DIAMOND AINGIA STUDIO NA MOHAMMED RAMADAN KUANDAA WIMBO WA PAMOJA

DIAMOND AINGIA STUDIO NA MOHAMMED RAMADAN KUANDAA WIMBO WA PAMOJA

Mwanamuzi kutoka Tanzania,Diamond Platnumz ameingia studio kurekodi wimbo na staa wa muziki kutoka nchini Misri, Mohamed Ramadan. Diamond ameingia studio na staa huyo ambaye ni mbabe wa youtube afrika kwa upande wa wasanii kwani anazaidi ya subscribers zaidi ya milioni 13.3 kwenye mtandao huo huku akiwa amevuna jumla ya watazamaji zaidi ya bilioni 4.3 kwenye mtandao huo wa youtube. Diamond na Mohamed wamekutana jijini Dubai ambapo wote walikuwa wamealikwa kwenye tamasha la All Africa Festival lililofanyika usiku wa kuamkia October 22,mwaka wa 2021. Ikumbukwe Diamond Platnumz ndiye alikuwa msanii wa kwanza Afrika Mashariki na kati kufikisha jumla ya watazamaji bilioni 1 kwenye mtandao wa youtube lakini pia ndiye msanii mwenye subscribers wengi kwa wasanii wa wanaopatikana kusini mwa Jangwa la Sahara.

Read More