Malkia wa Dancehall Spice Amzimia Drake Hadharani Akiwa Jukwaani Wireless Festival

Malkia wa Dancehall Spice Amzimia Drake Hadharani Akiwa Jukwaani Wireless Festival

Msanii maarufu wa dancehall kutoka Jamaica, Spice, amezua gumzo baada ya kumtamkia hadharani mwanamuziki wa Kanada, Drake, kuwa ni “crush” wake wa muda mrefu. Tukio hilo lilijiri wakati wa onyesho lake la kusisimua katika tamasha la Wireless Festival, ambapo alikonga nyoyo za mashabiki kwa miondoko ya nguvu na burudani ya kiwango cha juu. Spice, anayefahamika kama Queen of Dancehall, alichukua fursa hiyo kuonyesha mapenzi yake ya wazi kwa Drake kupitia remix ya kibabe ya wimbo wake maarufu One Dance. Katika mdundo huo uliopigwa kwa mtindo wa Karibea, Spice aliongeza ladha ya Jamaica kwa sauti na mahaba kwa kucheza kwa weledi, hali iliyowafanya mashabiki kulipuka kwa shangwe na kushangilia kwa nguvu. Wakati akiimba na kucheza kwa miondoko ya kuvutia, Spice alisema, “Wacha niseme ukweli, nimekuwa na hisia kwa Drake kwa miaka”! Kauli hiyo ilitawala mitandao ya kijamii huku mashabiki wengi wakionekana kuvutiwa na ujasiri wake. Tamasha la Wireless Festival ambalo hufanyika Uingereza, limeendelea kuwa jukwaa la kusisimua kwa wasanii wa kimataifa, na onyesho la Spice mwaka huu limeongeza moto kwa jinsi alivyochanganya muziki, mahaba, na ucheshi wa jukwaani, kwa mtindo wa kipekee wa Caribbean. Wengi sasa wanangojea kuona iwapo Drake atajibu hisia hizo au hata kufanya kazi ya pamoja na Malkia huyo wa Dancehall

Read More
 Drake Awakodishia Private Jet Waandishi wa Habari

Drake Awakodishia Private Jet Waandishi wa Habari

Rapa maarufu Drake ameonesha tena kiwango chake cha juu cha ukarimu na ushawishi kwenye muziki baada ya kukodi ndege binafsi (Private Jet) yenye thamani ya Dola Milioni 80, kwa ajili ya kuwachukua Bloggers, Waandishi wa Habari na Streamers maalum kwenda jijini London kuhudhuria tamasha kubwa la Wireless Festival. Drake, ambaye ndiye mtumbuizaji mkuu (Headliner) wa tamasha hilo, ameandaa safari hiyo kama sehemu ya kuwatambua na kuwahusisha watu muhimu katika tasnia ya burudani na mitandao ya kijamii nchini Marekani. Tamasha hilo litafanyika kwa siku tatu kuanzia leo Julai 11 hadi Julai 13, likitarajiwa kuvutia maelfu ya mashabiki kutoka sehemu mbalimbali za dunia. Hatua hii inaonyesha namna Drake anavyothamini vyombo vya habari na majukwaa ya kidijitali katika kuendeleza na kusambaza muziki wake kimataifa.

Read More
 Mtoto wa Lil Wayne Asema Baba Yake Ndiyo Msingi wa Mafanikio ya Drake

Mtoto wa Lil Wayne Asema Baba Yake Ndiyo Msingi wa Mafanikio ya Drake

Mtoto wa rapa maarufu Lil Wayne, anayefahamika kwa jina la kisanii Lil Novi, amezua gumzo mitandaoni baada ya kudai kuwa mafanikio ya rapa Drake yalichangiwa pakubwa na mchango wa baba yake katika uandishi wa nyimbo. Akizungumza katika mahojiano maalum yaliyopeperushwa hivi majuzi, Lil Novi alisema kuwa Lil Wayne hakuhusika tu kumtambulisha Drake kwa dunia ya muziki, bali pia alihusika moja kwa moja katika kuandika nyimbo zake nyingi zilizomletea umaarufu mkubwa.  “Baba yangu ndiye aliyeweka msingi mzuri kwa Drake. Yeye ndiye aliyemsaidia kuandika nyimbo nyingi za Drake ambazo zimepata mafanikio makubwa,” alisema Lil Novi kwa msisitizo. Kauli hiyo imeibua mijadala mikali miongoni mwa mashabiki wa hip hop, huku baadhi wakisema kwamba si jambo la kushangaza ikizingatiwa kuwa Lil Wayne ndiye aliyemsaini Drake chini ya lebo yake ya Young Money mwaka 2009, kipindi ambacho Drake alikuwa bado hajajijengea jina kimataifa. Uhusiano kati ya Lil Wayne na Drake umeendelea kuvutia hisia za wengi, hasa kutokana na ushirikiano wao wa muda mrefu na mafanikio ya pamoja katika muziki. Hata hivyo, madai ya Lil Novi yanaweza kufungua ukurasa mpya wa mjadala kuhusu mchango wa Lil Wayne katika mafanikio ya Drake, ambao kwa sasa ni miongoni mwa wasanii wa hip hop wanaosikilizwa zaidi duniani. Wakati mashabiki wakingoja kauli ya Drake au Lil Wayne kuhusu suala hilo, ukweli mmoja unabaki palepale, ushawishi wa Lil Wayne katika muziki wa kizazi hiki hauwezi kupuuzwa.

Read More
 Rick Ross Aonyesha Nia ya Kumaliza Bifu au Mzozo Wake na Drake

Rick Ross Aonyesha Nia ya Kumaliza Bifu au Mzozo Wake na Drake

Rapa maarufu Rick Ross amejitokeza hadharani na kuonyesha wazi nia ya kumaliza mzozo wake wa zamani na rapa mwenzake maarufu, Drake. Mzozo huu umekuwa ukivuma kwa muda mrefu katika tasnia ya muziki wa rap, huku mashabiki wakisubiri kwa hamu kuona kama wawili hawa wataweza kusuluhisha tofauti zao. Katika mazungumzo na wanahabari hivi karibuni, Rick Ross alionyesha kuwa yuko tayari kuweka tofauti zao nyuma na kuanzisha upya uhusiano mzuri na Drake. “Hujui kamwe… Nitumie chupa ya Belaire nyeupe, nitachukua picha pamoja nawe.”, Rozzay alisema akijibu juu ya mpango wa kusuluhisha mzozo huo. Kauli hii imepokelewa kwa mshangao na furaha na mashabiki wa muziki wa hip hop, ambao wamekuwa wakisubiri alama zozote za amani kati ya wawili hao. Chupa ya Belaire ni kivutio maarufu katika tamaduni za hip hop na inaashiria ishara ya urafiki na mazungumzo ya amani. Mzozo kati ya Rick Ross na Drake ulikuwa umeanza kwa njia mbalimbali, ikiwa ni pamoja na kuachishwa kwa nyimbo, matusi ya hadharani, na mashindano ya moja kwa moja kupitia muziki. Hata hivyo, hivi karibuni kuna dalili za marekebisho, na Rick Ross anahisi kuwa sasa ni wakati mzuri wa kuweka tofauti zao kando. Kufuatia kauli hii, mashabiki na wanamuziki wengine wametoa maoni mbalimbali, wengi wakipongeza hatua hii kama njia ya kuleta mshikamano katika tasnia ya muziki ambayo mara nyingi huathirika na migogoro ya hadharani. Kwa sasa, hakuna taarifa rasmi kutoka kwa Drake kuhusu kauli hii ya Rick Ross, lakini mashabiki wanatarajia majibu mazuri yatakapotolewa na ni matumaini makubwa kwamba wawili hawa wataweza kurejea kuwa marafiki na mshirika wa muziki.

Read More
 Kanye West Aonyesha Furaha Baada ya Larry Hoover Kumpunguzia Kifungo, Atoa Shukrani kwa Drake

Kanye West Aonyesha Furaha Baada ya Larry Hoover Kumpunguzia Kifungo, Atoa Shukrani kwa Drake

Msanii maarufu wa Marekani, Ye (Kanye West), ameonyesha furaha yake baada ya Rais wa sasa wa Marekani, Donald Trump, kupunguza kifungo cha aliyekuwa kiongozi wa genge kutoka Chicago, Larry Hoover. Ye alionyesha shukrani kwa msanii mwenzake Drake kwa mchango wake katika juhudi za kumkomboa Hoover, akitambua ushirikiano wao kama sehemu muhimu ya mafanikio haya. “THANK YOU DRAKE FOR HELPING TO BRING LARRY HOOVER HOME.”, Aliandika X Ye na Drake waliweka tofauti zao kando na kuungana kwa tamasha la pamoja mnamo mwaka 2021, likiwa ni sehemu ya kampeni ya kumtetea Hoover na kushinikiza kuachiliwa kwake. Tamasha hilo liliitwa Free Larry Hoover Benefit Concert na lilileta msukumo mkubwa kwa umma na viongozi kuhusu kesi ya Hoover. Larry Hoover alikuwa akitumikia kifungo cha maisha kwa makosa ya uhalifu wa genge, lakini amekuwa akihusishwa na mabadiliko chanya akiwa gerezani. Uamuzi wa kupunguziwa kifungo wake umetajwa na baadhi ya watu kama hatua ya kihistoria katika juhudi za mageuzi ya mfumo wa haki nchini Marekani. Kwa Ye, huu ni ushindi mkubwa kwa familia ya Hoover na kwa wale wanaoamini katika nafasi ya pili na msamaha wa kweli.

Read More
 Drake Athibitisha Kurejea kwa OVO Fest 2025 Wakati wa Onyesho la Central Cee

Drake Athibitisha Kurejea kwa OVO Fest 2025 Wakati wa Onyesho la Central Cee

Msanii maarufu wa muziki wa hip hop na R&B, Drake, ametangaza kurejea kwa tamasha lake maarufu la OVO Fest msimu wa joto wa mwaka 2025. Tangazo hilo liliwekwa wazi wakati wa onyesho la rapa wa Uingereza Central Cee lililofanyika katika uwanja wa Nokia Arena, ambapo Drake pia alishangiliwa kwa kupanda jukwaani kwa kushtukiza. Drake alidokeza kuwa Central Cee atakuwa miongoni mwa wasanii watakaotumbuiza kwenye OVO Fest jijini Toronto msimu huu wa kiangazi. Tangazo hili limepokewa kwa shangwe mitandaoni, huku mashabiki wakijawa na matarajio makubwa ya kile kinachoonekana kuwa mojawapo ya matamasha makubwa ya mwaka. Kwa mujibu wa vyanzo vya karibu na OVO Sound, tamasha hilo litafanyika kati ya mwezi Julai na Agosti, likiwa ni sehemu ya ratiba ya kiangazi yenye shughuli nyingi kwa Drake. Msimu huu wa joto unaonekana kuwa wa kazi nyingi kwa Drake, kwani baada ya tangazo hilo, atapanda jukwaani kama msanii kinara kwa siku tatu mfululizo kwenye Wireless Festival nchini Uingereza mwezi  mwezi Julai, akiungana na majina makubwa kama Vybz Kartel, Burna Boy, na wengine wengi. Tamasha la OVO Fest ni mojawapo ya matukio makubwa zaidi ya muziki kila msimu wa joto jijini Toronto, likijulikana kwa kuwaalika wasanii wa kimataifa na kushuhudia maonyesho ya kipekee.

Read More
 Mfululizo wa Picha za Drake Mtandaoni Wazua Tetesi za Albamu Mpya Iitwayo Ice Man

Mfululizo wa Picha za Drake Mtandaoni Wazua Tetesi za Albamu Mpya Iitwayo Ice Man

Rapa nyota wa Canada, Drake, amezua gumzo mitandaoni baada ya kuchapisha mfululizo wa picha kwenye ukurasa wake wa Instagram, ambazo mashabiki na wachambuzi wa muziki wanazitafsiri kama uthibitisho wa albamu yake mpya kwa jina la ICEMAN. Katika chapisho lake kwenye akaunti rasmi ya Instagram (@champagnepapi), Drake alionekana kuweka picha ya mandhari ya theluji yenye mlima uliofunikwa na barafu, na chini yake akaandika kwa herufi kubwa; ICEMAN. Chapisho hilo limepokea zaidi ya likes milioni moja na maelfu ya maoni kutoka kwa mashabiki waliotafsiri ujumbe huo kama tangazo la jina la albamu mpya. Drizzy pia alichapisha picha za watu mbalimbali mashuhuri wanaohusiana na jina hilo, ikiwa ni pamoja na Bobby Drake, mhusika wa Marvel Comics, Kimi Räikkönen, dereva wa zamani wa Formula 1 na Val Kilmer, ambaye aliigiza kama Iceman katika filamu ya Top Gun. Hata hivyo, Drake hajatoa tamko rasmi kuthibitisha jina la albamu hiyo, lakini machapisho hayo yameongeza matarajio makubwa miongoni mwa mashabiki wake duniani kote. Albamu hii itakuwa kazi yake ya kwanza ya solo tangu kutolewa kwa For All The Dogs mwaka 2023. Kwa sasa, wapenzi wa muziki wanasubiri kwa hamu taarifa rasmi kutoka kwa rapa huyo anayejulikana kwa ubunifu wa hali ya juu na mbinu za kipekee za kusisimua kwenye mitandao ya kijamii

Read More
 Dr. Dre afunguka sababu za kumtetea Kendrick Lamar kwenye bifu na Drake

Dr. Dre afunguka sababu za kumtetea Kendrick Lamar kwenye bifu na Drake

Mtayarishi mkongwe wa muziki nchini Marekani Dr. Dre, amefunguka sababu za kuchagua upande kwenye bifu ya Drake na Kendrick Lamar iliyotikisa ulimwengu wa muziki wa Hiphop duniani. Akizungumza kwenye podcast ya The Unusual Suspects With Kenya Barris and Malcolm Gladwell, Dr. Dre ameeleza kuwa hakuvutiwa na hatua ya Drake kumshambulia Kendrick Lamar pamoja na familia yake. “Ninapenda wimbo wa  ‘Not Like Us’. Lakini niliposikia Drake akisema mambo mabaya kuhusu mke wa Kendrick na watoto wake, nikasema ‘Ah, adios!’”, Alisema Dre. Kauli ya Dr. Dre inakuja muda mfupi baada ya Drake kufungua kesi dhidi ya Universal Music Group kuhusu wimbo ‘Not Like Us’, ambao una mashambulizi makali dhidi yake. Hii si mara ya kwanza Dre kuzungumzia ‘Not Like Us’. Novemba mwaka jana, aliusifu wimbo huo kwa kusema kuwa umeleta mshikamano mkubwa kwa muziki wa Hiphop nchini Marekani.

Read More
 Jumba la Drake lavamiwa na wahuni

Jumba la Drake lavamiwa na wahuni

Jumba la Rapa Drake lililopo mjini Los Angeles nchini Marekani limevamiwa na mtu mmoja ambaye alivunja na kufanikiwa kuingia ndani. Baada ya muda mfupi, polisi waliwasili kufuatia simu iliyopigwa na walinzi wa nyumba wakidai kumuona mtu mmoja akitokomea akiwa amebeba kitu. Baada ya msako wa nje na maeneo ya Jirani, alipatikana mtu mmoja ambaye alihisiwa kuwa ndiye mwizi. Polisi walimtia mbaroni na kumkuta akiwa amebeba vitu ambavyo vinaaminika alivitoa nyumbani kwa Drizzy ikiwemo picha za michoro. Tovuti ya TMZ inaripoti, Drake hakuwepo nyumbani wakati tukio linatokea.

Read More
 Drake adokeza ujio wa Album mpya

Drake adokeza ujio wa Album mpya

Rapa kutoka nchini Canada Drake huenda akaachia Album nyingine mwaka huu, amedokeza kupitia onesho lake ambalo alitumbuiza jana Jumamosi. Wakati akimalizia onesho hilo, Drizzy aliwaambia mashabiki zake; “I hope I can strike up more emotions for you. Maybe this year. I might get bored and make another one. Who knows.” Mwaka 2022 ulikuwa wa neema kwa mashabiki wa Drake kwani walibarikiwa kumsikia zaidi ya mara moja kupitia Album yake “Honestly, Nevermind” iliyotoka Juni 17 na Album ya pamoja na 21 Savage, “Her Loss” iliyotoka Novemba 4.

Read More
 Drake kutoa ushuhuda wa mauji ya Rapa XXXTentacion mwaka

Drake kutoa ushuhuda wa mauji ya Rapa XXXTentacion mwaka

Rapa Drake ni miongoni mwa watu maarufu sita ambao wameorodheshwa kwa ajili ya kutoa ushuhuda kwenye shtaka la mauaji ya Rapa XXXTentacion mwaka 2018 ambaye aliuawa kwa kupigwa risasi. Mawakili wa utetezi wamewasilisha orodha hiyo yenye jina la Drake, Quavo, Offset, marehemu Takeoff, Tekashi 6ix9ine na Joe Budden ambao wametajwa kama mashahidi kwenye nyaraka hizo za Mahakama. Drizzy ametajwa kwenye shtaka hilo la mauaji ya XXXTentacion kufuatia bifu lao la mwaka 2017 ambapo marehemu XXX aliwahi kuibuka na kudai Drake ameiba midondoko yake (flows) kutoka kwenye wimbo wake wa kwanza “Look At Me” na kuitumia kwenye wimbo wake “KMT” wa mwaka 2017. Baada ya mwaka mmoja wa kutupiana maneno na mvutano, akaunti ya Instagram ya XXXTentacion upande wa insta story yaliandikwa maneno yasemayo “If anyone tries to kill me it was Drake,” akimtaja Drizzy kama mtu ambaye anatishia kuchukua uhai wake. Miezi minne baadaye, rapa huyo aliuawa kwa kupigwa risasi mjini Florida.

Read More
 Drake akuja na mkufu wa Almasi uliotengenezwa kwa Pete za Uchumba 42

Drake akuja na mkufu wa Almasi uliotengenezwa kwa Pete za Uchumba 42

Rapa kutoka Marekani Drake amekuja na mkufu wa Almasi ambao umetengenezwa kwa Pete za Uchumba 42 ambazo aliwahi kutaka kuwavisha wanawake tofauti tofauti kwenye maisha yake lakini akabadili maamuzi. Sonara maarufu Alex Moss ameiambia Tovuti ya TMZ kwamba mkufu huo unaitwa “Previous Engagements” ikiwa ni kumbukumbu kwa wanawake hao ambao Drake alitamani kuwaoa lakini akabadili gia angani. Alex anasema Pete hiyo imetumia miezi 14 kukamilika na ilitengenezwa kwa mkono huko New York, Marekani. Hata hivyo gharama yake bado haijawekwa wazi.

Read More