Drake aongoza kusikilizwa Spotify Marekani mwaka 2022

Drake aongoza kusikilizwa Spotify Marekani mwaka 2022

Rapa Drake ndiye mfalme wa Spotify nchini Marekani kwa mwaka 2022, mtandao huo umetoa takwimu za wasanii na nyimbo zilizosikilizwa zaidi kwa mwaka huu Duniani. Drake anaongoza kwa Marekani akifuatiwa na Taylor Swift pamoja na Bad Bunny. Kanye West na The Weeknd wanaikamilisha Top 5. Kwa upande wa Dunia nzima, Bad Bunny anaongoza kwa kuwa na streams nyingi zaidi (18.5 Billion) kwa mwaka huu pia ikiwa ni miaka mitatu mfululizo kwenye nafasi hiyo.

Read More
 Kanye West amfukuza kazi mfanyakazi wake kisa Drake

Kanye West amfukuza kazi mfanyakazi wake kisa Drake

Rapa Kanye West ameripotiwa kumfukuza kazi mfanyakazi wake kwenye kampuni ya Yeezy kufuatia kupiga wimbo wa Drake ofisini. Hii ni kwa mujibu wa Rolling Stone. Utakumbuka juzi kati Drake alitapika nyongo kwenye “Circo Loco” ngoma ambayo inapatikana kwenye Album ya pamoja na 21 Savage, Her Loss. Drizzy alifunguka ya moyoni kwamba aliamua kupatana na Kanye West na kufanya onesho la pamoja (Free Larry Hoover Concert) Disemba 10, 2021 kwa sababu ya heshima tu ya godfather wake, J. Prince. “Linking with the opps, b*tch, I did that shit for J Prince. B*tch, I did it for the mob ties” – alichana Drizzy.

Read More
 Rapa Drake na 21 Savage washtakiwa na Kampuni ya VOGUE kwa madai ya utapeli

Rapa Drake na 21 Savage washtakiwa na Kampuni ya VOGUE kwa madai ya utapeli

Wanamuziki Drake na 21 Savage wameingia tena kwenye headsline baada ya kushtakiwa na Kampuni ya VOGUE kufuatia kutumia chapisho feki na kisha ku-promote album yao mpya iitwayo “Her Loss” iliyotoka Nov 4, mwaka huu. Kwenye picha hiyo ambayo inaonekana kama jalada halali la Vogue, limepelea taharuki kwa mashabiki kuamini kuwa huenda kampuni hiyo ingetoa toleo maalum hivi karibuni juu ya album hiyo inayozungumziwa kwa sasa. Mwanamama Condé Nast ambaye ni mmiliki wa kampuni ya Vogue, amedai timu ya Drake imeudanganya Umma kufuatia ujumbe wa Drake kuhusu “kusherehekea jalada la Drake kutoka kwenye kampuni yetu Vogue” pamoja na kumpongeza Mhariri mkuu Anna Wintour wa jarida hilo mtandaoni kwa kudai wamepata baraka. Condé Nast amekaririwa na vyombo vya habari akisema, Drake amejichukulia sheria mkononi, hayakuwa makubariano Maalum

Read More
 Drake amchana Kanye West na Megan Thee Stallion kupitia wimbo wa Circo Loco

Drake amchana Kanye West na Megan Thee Stallion kupitia wimbo wa Circo Loco

Rapa kutoka Marekani Drake ameamua kutapika nyongo kwenye “Circo Loco” ngoma ambayo inapatikana kwenye Album ya pamoja na 21 Savage, Her Loss. Drizzy amefunguka ya moyoni kwamba aliamua kupatana na Kanye West na kufanya onesho la pamoja (Free Larry Hoover Concert) Disemba 10, mwaka 2021 kwa sababu ya heshima tu ya godfather wake, J. Prince. “Linking with the opps, b*tch, I did that shit for J Prince. B*tch, I did it for the mob ties” – amechana Drizzy. Utakumbuka Drake pia kupitia hii single amemchana Megan Thee Stallion kufuatia madai yake ya kupigwa risasi na Tory Lanez kwa kusema kuwa alidanganya juu ya tukio hilo. “This b**ch lied about getting shot but she still a stallion. She don’t even get the joke but she still smiling.” amechana Drake.

Read More
 Kanye West amvulia kofi Drake, amuita rapa mkali wa muda wote

Kanye West amvulia kofi Drake, amuita rapa mkali wa muda wote

Rapa Kanye West anataka kila aliye karibu yake afanikiwe, amempa maua yake Drake akiwa hai. Kwenye mahojiano mapya na Drink Champs, Kanye West amefunguka kwamba Drake ni rapa mkubwa na mkali zaidi kwa nyakati zote na hawezi kuomba radhi kwa kauli yake hiyo. Hata hivyo YE amekutana na upinzani mkubwa kutoka kwa watu mbali mbali duniani wakidai kuwa rapa huyo amekosa adabu kabisa kutomtaja Kendrick Lamar, Jay Z na Lil Wayne kama The Greatest Rapper Alive. Licha ya kumwagia misifa Drake, Kanye ametema nyongo tena kwa Drizzy kwa kusema kuwa aliwahi kufanya mapenzi na Kris Jenner, Mama mzazi wa Kim Kardashian.

Read More
 Drake na The Weeknd wagoma kupeleka kazi zao Grammy

Drake na The Weeknd wagoma kupeleka kazi zao Grammy

Wanamuziki Drake na The Weeknd wameendelea kuziwekea mgomo Tuzo za Grammy, taarifa mpya zinasema wakali hao kutoka nchini Canada hawajawasilisha nyimbo zao kwa ajili ya kufikiriwa (Consideration) kwa tuzo za mwaka 2023. Album zao ‘Honestly, Nevermind’ na ‘Dawn FM’ hazijawasilishwa kwenye kipengele chochote cha tuzo hizo kwa mwaka 2023 sambamba na nyimbo zao Hit kama ‘Sticky’ na ‘Out Of Time.’ Kwa upande wa Drizzy, amekuwa kwenye mahusiano mabaya na Waandaaji wa tuzo hizo tangu mwaka 2017 baada ya kutoridhika na kipengele ambacho wimbo wake “Hotline Bling” iliwekwa. Mwaka Jana alitangaza kujitoa kwenye Tuzo hizo baada ya kutajwa kwenye vipengele viwili ambapo alitajwa kuwania Best Rap Album na Best Rap Performance. Si hayo tu, Drake pia alisimimama kumtetea The Weeknd ambaye mwaka Jana alikosekana kwenye kipengele chochote cha Tuzo za Grammy licha ya kuachia Album “After Hours” ambayo ilifanya vizuri sana.

Read More
 Kendrick Lamar ashinda Tuzo ya Msanii Bora wa  Hiphop kwenye BET Hip-Hop Awards 2022

Kendrick Lamar ashinda Tuzo ya Msanii Bora wa Hiphop kwenye BET Hip-Hop Awards 2022

Rapa Kendrick Lamar ameibuka mshindi wa kipengele cha Hip-Hop Artist Of The Year kwenye Tuzo za BET Hip-Hop 2022 ambazo zinatolewa usiku wa kuamki leo nchini Marekani. Kendrick Lamar pia ameondoka na ushindi kwenye vipengele vya Lyricist Of The Year, Best Hip Hop Video “Family Ties”, Best Live Performer na Hip Hop Album Of The Year (Mr. Morale & The Big Steppers) Kwa upande mwingine Rapa 50 Cent ameibuka mshindi wa Tuzo ya ‘Hustler Of The Year’ akiwaangusha DJ Khaled, Drake, Cardi B, Jay-Z, Kanye West na Megan Thee Stallion. Kolabo ya Future, Tems na Drake “Wait For You” imeshinda Tuzo ya Best Collaboration kwenye Tuzo za BET Hip Hop 2022.

Read More
 DRAKE AKANUSHA KUKAMATWA SWEDEN

DRAKE AKANUSHA KUKAMATWA SWEDEN

Usiku wa kuamkia leo hashtag ya Free Drake ilikamata headlines za mitandao ya Kijamii baada ya taarifa kuwa Drake na walinzi wake wamekamatwa nchini Sweden kwa makosa ya kukutwa na Bangi. Taarifa hiyo ilichochewa na video ambayo ilionesha ndege binafsi ya Drizzy ikiwa nchini humo. Sasa baada ya taharuki hiyo, timu yake imeibuka na kukanusha taarifa hizo kwa kusema hazina ukweli wowote.

Read More
 DRAKE AMJIBU PUSHA T KUHUSU KAULI YAKE KUFUNGIWA KUINGIA CANADA

DRAKE AMJIBU PUSHA T KUHUSU KAULI YAKE KUFUNGIWA KUINGIA CANADA

Rapa kutoka marekani Drake ameibuka na kumjibu Pusha T baada ya kauli yake kuwa amepigwa marufuku kuingia nchini Canada kufuatia bifu yao ambayo ilifikia pabaya. Drizzy ametokea kwenye post ya Chubbs view ambaye ni member wa OVO, post iliyoonekana kumlenga Pusha T ikisema hawana haja ya kuwapiga marufuku washkaji zao bali wanawakaribisha kiroho safi kabisa. Comment ya Drake ilifuata ikionekana kumkaribisha Pusha T aingie nchini humo. Kama utakumbuka vyema, Pusha T ndiye aliingia kwenye bifu na drake baada ya kufahamisha dunia kwamba Drake ana mtoto anaitwa Adonis Kupitia freestyle yake ‘The Story of Adidon’  na Hii ilimfanya Drake na baadaye kuthibitisha taarifa hizo kupitia album yake, Scorpion mwaka 2018.

Read More
 DRAKE ANG’AA KWENYE TUZO ZA BILLBOARD MUSIC AWARDS 2022

DRAKE ANG’AA KWENYE TUZO ZA BILLBOARD MUSIC AWARDS 2022

Rapa Drake ameendelea kung’aa kwenye Tuzo za Billboard (Billboard Music Awards) ambapo usiku wa kuamkia leo ametengeneza rekodi ya kuwa msanii aliyeshinda Tuzo nyingi zaidi, akishinda Jumla ya Tuzo 34 kwenye historia ya BBMA’s. Drizzy ameshinda Tuzo ya Top Rap Artist, Top Rap Album kupitia album yake ya Certified Lover Boy na Top Artist. Kwa upande wa muziki wa Injili Rapa Kanye West ametamba kwa kushinda Tuzo Tatu; Top Christian Album kupitia album yake ya DONDA, Top Christian Artist na Top Gospel Artist. Wasanii wengine walioshinda tuzo za billboard ni pamoja na Olivia Rodrigo ambaye alishinda Tuzo ya Msanii Bora Chipukizi huku Justin Bieber akishinda tuzo ya Top Collaboration kupitia ngoma ya STAY aliyomshirikisha The Kid Laroi .

Read More
 DRAKE ASAINI DILI NONO LA SHILLINGI BILLIONI 46 ZA KENYA.

DRAKE ASAINI DILI NONO LA SHILLINGI BILLIONI 46 ZA KENYA.

Rapa kutoka Marekani Drake ameripotiwa kutia saini dili nono na Universal Music Group ambalo linadaiwa kuwa na thamani ya dola milioni 400 sawa na zaidi ya shilingi bilioni 46 za Kenya . Habari hiyo imethibitishwa kupitia simu ya mapato ya UMG (Q1 earnings call), licha ya kuwa kiasi halisi hakikuwekwa wazi lakini wadadisi wa mambo wametaja kuwa ni kiasi cha pesa kisichopungua dola milioni 400, ingawa kinaweza kuwa kikubwa zaidi hicho. Hapo awali Drake aliwahi kusaini dili na Cash Money kupitia ‘Republic Records, inazomilikiwa na Universal Music Group, na amesaini tena na UMG mkataba mpya, ambao makubaliano yatahusisha kurekodi, kusambaza kazi za muziki, bidhaa za mavazi pamoja na miradi mingine. Kwa mujibu wa wakili mmoja katika tasnia ya muziki nchini Marekani, “Drake ana uwezo wa kujadiliana ili kufikia muafaka wa mgawanyiko wa faida kamili

Read More
 DRAKE AWACHEKA FORBES KWA ORODHA YAO YA WASANII WA HIPHOP WALIOINGIZA FEDHA NYINGI 2021

DRAKE AWACHEKA FORBES KWA ORODHA YAO YA WASANII WA HIPHOP WALIOINGIZA FEDHA NYINGI 2021

Rapa kutoka Marekani Drake ameonyesha wazi kuikataa orodha ya wasanii 10 wa Hip Hop walioingiza fedha nyingi kwa mwaka 2021, akitajwa namba 4, Jay-Z akiwa kinara kwenye orodha hiyo. Kwenye orodha hiyo Drake ametajwa kuingiza kiasi cha dola milioni 50 kwa mwaka 2021 kitu ambacho ameonesha hajakubaliana na tathmini hiyo. Drake amewajibu Forbes kwa kuangua kicheko kwa kuweka emoji ya kucheka katika taarifa hiyo kwenye mtandao wa Instagram. Inaelezwa kuwa watoa tathimini walikosea, kwani mapato ya mkali huyo yanadaiwa kuzidi kiasi cha dola milioni 50 walizoziweka. Ikumbukwe, Forbes walitoa orodha hiyo  Jumanne ya wiki iliyopita, ikiwa ni utaratibu wake wa kufanya hivyo kila mwaka.

Read More