DRAKE ALIPITA NA MREMBO JULIA FOX KABLA YA KANYE WEST
Kumbe Rapa Kanye West kutoka nchini Marekani amepita sehemu ambayo rapa mwenzake Drake alipita kitambo. Taarifa mpya mjini zinadai kwamba Drake aliwahi kuwa na mahusiano na mrembo Julia Fox ambaye kwa sasa yupo penzini na Kanye West. Kwa mujibu wa tovuti ya Page Six, penzi lao lilianza mwaka 2020 kufuatia ukaribu ulioanza mwaka 2019 baada ya Drizzy kumtelezea DM mrembo huyo na kumsifia kuhusu ushiriki wake kwenye filamu ya Uncut Gems. Julia Fox aliachana na mumewe Artemiev na Drake ndiye akawa tulizo lake la muda mfupi. Kumbuka kuwa kipindi cha nyuma kabla ya wawili hawa kuzika tofauti zao walikuwa kwenye bifu zito huku sababu kubwa ikitajwa kuwa Drake aliwahi kusema kuwa yupo kwenye mahusiano na Ex wa rapa Kanye West ambaye ni Kim Kardashian na kwa kuthibitisha hilo alim-follow Instagram pamoja na kutoa ngoma yake ya “In My Feeling” akimuimba “Kiki” ambalo ni jina lingine la mrembo huyo.
Read More