Dudu Baya Amwaibisha Mwijaku kwa Tuhuma Nzito

Dudu Baya Amwaibisha Mwijaku kwa Tuhuma Nzito

Msanii mkongwe wa Bongofleva, Dudu Baya, amemwaibisha hadharani mtangazaji na mdau wa burudani Mwijaku kwa kuibua madai mazito dhidi yake. Akizungumza katika mahojiano ya hivi karibuni, Dudu Baya amedai kuwa Mwijaku kwa sasa hana makazi ya kudumu baada ya kudaiwa kufurushwa na mke wake kutoka katika nyumba aliyokuwa akiishi, hatua aliyodai ilitokea baada ya ndoa yao kuvunjika. Katika madai mengine mazito, Dudu Baya amedai kuwa kipindi Mwijaku alipokuwa akisoma chuoni aliwahi kuhusishwa na sakata la ushoga, kauli ambayo imezua mjadala mpana mitandaoni. Dudu Baya amejigamba kuwa hana sababu ya kuhangaika na makazi kwani anamiliki majumba mawili ya kifahari. Ameongeza kuwa hata kama mwanamke wake atamuacha, bado hawezi kukosa pa kuishi. Kauli hizi zimekuja siku chache baada ya Mwijaku kudai kuwa Dudu Baya anaishi kwenye lindi la umaskini kutokana na msanii huyo kujiingiza kwenye matumizi ya dawa za kulevya.

Read More
 Dudu Baya Amwonya Mwijaku Kutoingilia Ugomvi wake na Mkubwa Fella

Dudu Baya Amwonya Mwijaku Kutoingilia Ugomvi wake na Mkubwa Fella

Msanii mkongwe wa Bongo Fleva, Dudu Baya, amempa onyo kali mdau wa burudani, Mwijaku, akimtaka ajiondoe mara moja katika kile alichokiita vita ya mapinduzi kati yake na meneja Mkubwa Fella ambaye kwa sasa ni mgonjwa. Akipiga stori na Bongo 24, Dudu amesema Mwijaku anatafuta kiki kwa kuingilia mjadala usiomuhusu, na akasisitiza kuwa akizidi kuingilia ugomvi huo, ataambulia kichapo cha mbwa msikitini Kwa mujibu wa Dudu Baya, wanaopaswa kujibu hoja zinazomhusu Mkubwa Fella ni wasanii wakongwe waliopitia mikononi mwa meneja huyo, na siyo mtoto mdogo kama Mwijaku. Amesema ukimya wa wasanii wakongwe unatokana na ukweli kwamba wengi wao wanafahamu tabia za ukatili na unyanyasaji walizofanyiwa na Mkubwa Fella, ikiwemo kuzimwa kwa vipaji na nyota za wasanii kadhaa. Dudu ameongeza kuwa yuko tayari kuweka wazi maovu anayodai kufanywa na Mkubwa Fella ili jamii ya Watanzania ijue ukweli, akisema muda umefika wa ukweli kuanikwa bila woga. Kauli hiyo ya Dudu Baya imekuja kufuatia Mwijaku kumtaka aonyeshe utu na heshima kwa Mkubwa Fella, hasa ikizingatiwa kuwa meneja huyo anaumwa. Mwijaku alimkosoa Dudu Baya baada ya kauli yake ya awali kwamba endapo Mkubwa Fella atafariki, hatofika kwenye mazishi yake.

Read More
 Dudu Baya Amshambulia Vikali Mkubwa Fella kwa Kumtakia Kifo

Dudu Baya Amshambulia Vikali Mkubwa Fella kwa Kumtakia Kifo

Msanii mkongwe wa muziki wa Bongo Fleva, Dudu Baya, amezua mjadala mkubwa mitandaoni baada ya kutoa kauli nzito dhidi ya meneja wa wasanii Tanzania, Mkubwa Fella, akisema hata akipata taarifa za kifo chake hatahudhuria mazishi yake. Akizungumza na Bongo24, Dudu Baya amemtaja Mkubwa Fella kama mtu mkatili aliyewanyanyasa wasanii wengi na kuzima vipaji vingi ndani ya tasnia ya muziki wa Bongo Fleva. Kwa mujibu wa msanii huyo, mateso na ukandamizaji unaodaiwa kufanywa na meneja huyo uliwaathiri wasanii wengi kiasi cha kuwaacha na maumivu makali. Aidha, Dudu Baya amemkosoa mke wa Mkubwa Fella, akisema hana ufahamu wa kina kuhusu yaliyokuwa yakijiri nyuma ya pazia la tasnia hiyo, na kumtaka aache kuwashutumu wasanii kwa madai ya kukataa kumsaidia meneja huyo katika gharama za matibabu. Kauli za Dudu Baya zimekuja siku chache baada ya taarifa za kuugua kwa Mkubwa Fella, ambapo mke wake alilalamika hadharani kuwa baadhi ya wasanii aliowahi kuwasaidia wamekataa kuchangia matibabu yake.

Read More
 Dudu Baya Awatahadharisha Wanaume Kuhusu Wanawake Wanaotumia Ushirikina

Dudu Baya Awatahadharisha Wanaume Kuhusu Wanawake Wanaotumia Ushirikina

Msanii mkongwe wa muziki wa Hip Hop nchini Tanzania, Dudu Baya, amezua gumzo mitandaoni baada ya kutoa kauli kali inayowalenga wanawake wanaotembelea waganga wa kienyeji kwa masuala ya mahusiano. Kupitia video iliyosambaa kwenye mitandao ya kijamii, Dudu Baya alionya vikali wanaume dhidi ya kuwa katika mahusiano na wanawake wanaotafuta huduma za kishirikina ili kudhibiti au kushikilia wapenzi wao.  “Ogopa sana mwanamke anayeenda kwa waganga (mshirikina), mwanaume ukipata mwanamke wa aina hii ni ngumu kufanikiwa. Utajikuta badala ya kwenda mjini unarudi kijijini,” alisema msanii huyo kwa msisitizo. Kauli hiyo imezua maoni tofauti kutoka kwa mashabiki na watumiaji wa mitandao ya kijamii, baadhi wakimuunga mkono huku wengine wakimtaka kutoa ushahidi au kufafanua zaidi kuhusu madai hayo. Dudu Baya, ambaye amekuwa akijulikana kwa kauli kali na zenye utata, amewahi pia kujihusisha na kampeni dhidi ya matumizi ya dawa za kulevya na pia kuwaasa wasanii wenzake kuzingatia maisha ya kiroho na kimaadili. Kwa sasa, bado haijafahamika ikiwa kauli hiyo ilikuwa ya jumla au imelenga mtu fulani, lakini imezidi kuibua hisia mseto miongoni mwa wafuasi wake na jamii

Read More