EDDY KENZO AFUNGUKA KUHUSU UHUSIANO WAKE NA BOBI WINE

EDDY KENZO AFUNGUKA KUHUSU UHUSIANO WAKE NA BOBI WINE

Staa wa muziki kutoka Uganda Eddy Kenzo amedai hana uhakika kama uhusiano wake na Bobi Wine utawahi kuwa mzuri tena. Katika mahojiano yake hivi karibuni Eddy kenzo amesema licha ya kutozungumza na Bobi wine kwa muda mrefu hana ugomvi wowote na bobi wine huku akisisitiza kwamba ikitokea amempa mwaaliko wa kutumbuiza kwenye onesho lake la muziki atatumbuiza bila kusita. Utakumbuka mwaka wa 2020 uhusiano kati Bobi Wine na Eddy Kenzo iliingiwa na ukungu mara baada ya sauti ya Eddy Kenzo kusambaa mtandaoni ambapo alisikika akimtolea uvivu bobi wine kwa kumtaja kuwa ni mbinafsi na mnafiki alipodai kuwa alimsaidia kimuziki. Eddy kenzo kipindi cha nyuma aliwahi fanya kazi na mdogo wa bobi wine, mikie wine chini ya lebo ya muziki ya firebase entertainment ambapo waliachia wimbo wa pamoja uitwao Yanimba ambao ulimfungulia milango Eddy kenzo kwenye tasnia ya muziki nchini Uganda.

Read More
 EDDY KENZO AMPIGIA UPATU KING SAHA KUTWAA UONGOZI WA CHAMA UMA

EDDY KENZO AMPIGIA UPATU KING SAHA KUTWAA UONGOZI WA CHAMA UMA

Bosi wa Big Talent, Eddy Kenzo ametangaza kumuunga mkono msanii mwenzake King Saha kwenye azma yake kuwania urais wa chama cha wanamuziki nchini uganda UMA. Katika mahojiano yake hivi karibuni Kenzo amethibitisha kuwa atampigia kura King Saha kama Rais ajaye wa Chama cha (UMA) akisema kwamba msanii huyo anaelewa matatizo ya yanayokumba tasnia ya muziki nchini uganda, kwani atawatumikia wanamuziki vyema. “King Saha alinipigia simu na kuniomba nimpigie kura ya kuwa rais wa UMA, pia nilianza muziki na King Saha, nakumbuka enzi zile tulikuwa studio tukishauriana, kipindi hicho hakuna aliyemfahamu, hivyo namuelewa sana. Siwezi kumsaliti, “alisema. Hata hivyo King Saha amemshukuru Mfalme Eddy Kenzo kwa kubali wito wake wa kuwasimamia wasanii wa uganda kupitia cha UMA.

Read More
 EDDY KENZO AKASHIFU VIKALI MUUNGANO WA WASANII NCHINI UGANDA

EDDY KENZO AKASHIFU VIKALI MUUNGANO WA WASANII NCHINI UGANDA

Mwanamuziki Eddy Kenzo amekashifu uongozi wa Muungano wa Wanamuziki nchini Uganda (UMA), akiwataja kuwa matapeli. Katika mahojiano yake ya hivi karibuni Kenzo ambaye anafanya vizuri na singo yake mpya “Nsimbudde” amedai kuwa viongozi wa Muungano Wanamuziki chini Uganda wamekwenda kinyume na malengo ya kubuniwa kwake kwani wamegeuza muungano huo kuwa kitega uchumi ya kuwanufahisha watu wachache huku wasanii wakiendelea kuishi maishi ya uchochole. “Nilikuwa miongoni mwa watu ambao walikuwa na imani kubwa na UMA lakini walipoteza mweelekeo. Sasa inahusu pesa, sio tasnia ya muziki tena,” alifafanua Eddy Kenzo. Bosi huyo wa Big Talent ameongeza kuwa hana tena kadi ya uanachama wa UMA na hatashiriki katika uchaguzi ujao wa muungano huo. Kauli ya Eddy Kenzo imekuja mara baada ya rais wa sasa wa muungano huo Cindy Sanyu kudai kuwa uchaguzi wa kuwachagua viongozi  wapya utafanywa kwa njia ya mtandao kutokana na ukosefu wa fedha za kutosha. Utakumbuka muungano wa wanamuziki nchini uganda unatarajiwa kuundaa uchaguzi wa kuwateua viongozi wapya wa muungano huo mwezi Mei mwaka huu na tayari tumeona wasanii kama Cindy Sanyu, King Saha na Maurice Kirya wamejitoza kuwania wadhfa wa urais huku Daddy Andre na Kalifah Aganaga wakitarajiwa kuchuana kwenye wadhfa wa Unaibu wa rais.

Read More
 EDDY KENZO AMWAGIA SIFA MARTHA MUKISA, ADAI ANAMPA MOYO WA KUWASAIDIA WASANII CHIPUKIZI NCHINI UGANDA

EDDY KENZO AMWAGIA SIFA MARTHA MUKISA, ADAI ANAMPA MOYO WA KUWASAIDIA WASANII CHIPUKIZI NCHINI UGANDA

Msanii nyota kutoka nchini Uganda Eddy Kenzo anataka kila aliye karibu yake afanikiwe, amehamua kumpa maua yake Martha Mukisa akiwa hai. Hitmaker huyo wa ngoma ya “Weekend” kwenye mahojiano yake ya hivi karibuni amemsifia Martha Mukisa kwa kusema kwamba anapenda jinsi anavyofikiri lakini pia ubunifu wake kwenye muziki. Eddy Kenzo amesema Martha Mukisa amemempa moyo wa kuwasaidia wasanii chipukizii nchini uganda kupitia lebo yake ya muziki ya Big Talent Entertaintment. Martha Mukisa amekuwa akisuasua kimuziki kwa kipindi cha miaka mitano iliyopita lakini nyota yake ilikuja ikang’aa mwaka wa 2021 alipofanya wimbo wa pamoja na Eddy Kenzo uitwao Sango. Utakumbuka Eddy Kenzo na Martha Mukisa wana ukaribu sana jambo ambalo limewafanya walimwengu kwenye mitandao ya kijamii kuhoji kuwa ni wapenzi.

Read More
 EDDY KENZO AKOSOA JANZI AWARDS, ATAKA UWAZI KWENYE TUZO ZA MUZIKI UGANDA

EDDY KENZO AKOSOA JANZI AWARDS, ATAKA UWAZI KWENYE TUZO ZA MUZIKI UGANDA

Nyota wa muziki nchini Uganda Eddy Kenzo amejiunga na orodha ya mastaa ambao wanakosoa mchakato uliotumika kuaandaa tuzo za Janzi Awards zilizokamilika majuzi nchini humo. Katika mkao na wanahabari Eddy kenzo  amewataka wanahabari kuwaweka waandaji wa tuzo za muziki nchini uganda kwenye mizani kama njia ya kutatua baadhi ya changamoto zinazoikabili tasnia ya muziki nchini humo. Hitmaker huyo wa “Leero Party” amewatolea uvivu wanaotilia shaka ushindi wake kwenye tuzo za Afrimma mwaka 2021 kwa kusema kwamba hatotishia na maneno yao kwenye mitandao ya kijamii kwani anafahamu fika alistahili kupewa tuzo ya msanii bora wa kiume kutokana na kazi zake za muziki. Ikumbukwe kwa wiki kadhaa sasa baadhi ya wasanii nchini uganda wakiongozwa na Spice Diana wamekuwa wakiwarushia lawama waandaji wa tuzo za Janzi Awards kwa kutokuwa na uwazi kwenye tuzo hizo.

Read More