ERIC OMONDI AJA NA MASHARTI MAPYA YA MALIPO KWA WASANII WA KENYA

ERIC OMONDI AJA NA MASHARTI MAPYA YA MALIPO KWA WASANII WA KENYA

Mchekeshaji  ambaye hivi karibuni ameibuka na kupigania maslahi ya muziki wa Kenya Eric Omondi ameibuka tena na kuwapa masharti waandaaji wa matamasha ya muziki nchini. Eric Omondi amesema wasaanii wanapaswa kulipwa asilimia 70 ya pesa kabla ya show na inayobaki wapewe wakishafika kwenye eneo ambalo show itafanyika. Lakini pia hajaishia hapo amewataka waandaji wa matamasha kuwalipa vizuri wasanii wa Kenya kwa kuwagawa wasanii katika makundi mawili. Kundi la kwanza la wasanii linapaswa kulipwa si chini ya shilling laki 6 za Kenya huku wasanii kundi la pili likitakiwa kulipwa shilling laki nne. Kupitia ukurasa wake wa Instagram Eric Omondi ameandika “lease be NOTIFIED that this YEAR I will PERSONALLY SCRUTINISE every detail of Every EVENT!!! I want to know how much ARTISTS are paid. I want to ensure that Every ARTIST is paid 70 PERCENT of their money PRIOR and 25 PERCENT on the day of the Event before the EVENT. Every A LIST Artist must be paid not less than Ksh 600,000. By A LIST I mean the following.NADIA MUKAMI – KSH 600,000 OTILE BROWN – KSH 1.5 MILLION NYASHINSKI – KSH 1.5 MILLION SAUTI SOL – KSH 2.8 MILLION All the B LIST Artist must be paid not less than KSH 450,000. i.e Ethic, Trio Mio etc.All EVENTS MUST BE HEADLINED BY A KENYAN ARTIST Whether BEYONCE is performing or not!!! SECURITY MUST Be PROVIDED for all ARTIST. A World CLASS BACKSTAGE FOR All ARTIST is NON NEGOTIABLE”

Read More
 ERIC OMONDI NA BIEN WA SAUTI SOL WARUSHIANA MAKONDE KWENYE ONESHO LA KONSHENS

ERIC OMONDI NA BIEN WA SAUTI SOL WARUSHIANA MAKONDE KWENYE ONESHO LA KONSHENS

Mchekeshaji Eric Omondi ameingia kwenye headlines baada ya kutaka kuzichapa na member wa Sauti Sol, Bien baraza usiku wa kuamkia Januari mosi katika onesho la Konshens Jijini Nairobi. Chanzo cha ugomvi huo ni baada ya Omondi kushinikiza kundi la Sauti Sol watumbuize wa mwisho katika orodha ya wasanii kama njia ya kuwapa heshima. Làkini Pia Bien katika moja ya interview amenukuliwa akisema muda wanaopewa kuperfom kama kundi la Sauti Sol katika tamasha haijawahi kuwa tatizo kwao, iwapo atakuwa wasanii wa kwanza au wa mwisho katika orodha ya wasanii. Ikumbukwe kwa muda  sasa eric omondi amekuwa akipaza sauti juu ya wasanii wa kenya kutotendewa haki na waandaaji wa matamasha ya muziki. Hii ni baada ya wasanii wa mataifa mengine kuonekana kupewa kipau mbele kufanya shows nchini huku wasanii wa Kenya wakiwekwa pembeni.

Read More
 ERIC OMONDI AMJIBU ZUCHU BAADA YA KUPINGA KAULI YAKE KUWA MUZIKI WA BONGOFLEVA UMEKUFA

ERIC OMONDI AMJIBU ZUCHU BAADA YA KUPINGA KAULI YAKE KUWA MUZIKI WA BONGOFLEVA UMEKUFA

Mchekeshaji Erick Omondi amejitokeza na kutetea kauli yake kwamba muziki wa Bongofleva umekufa kufuatia baadhi ya wasanii wake kufanya Amapiano. Kupitia mtandao wake wa Instagram, Omondi amemjibu Zuchu ambaye hakukubaliana na kauli hiyo akidai kwamba wanamuziki wa Tanzania wameamua kukumbatia muziki wa Amapiano ambao utawasaidia kujulikana zaidi. “Bongofleva haiwezi kufa, wasanii wanatoka nje ya eneo lao, kutafuta utofauti wa kujaribu sauti mpya. haijawahi shuhudiwa ikiuua tasnia yoyote, tasnia ya muziki ni kubwa sana, acha msanii ajaribu mambo yake. Hayo ni mabadiliko” alisema Zuchu. Kufuatia kauli hio Eric Omondi amejitokeza na kutetea kauli yake huku akimjibu Zuchu na kumweleza kwamba wanamuziki wa Kenya walianza hivyo na muziki wao ukapotea “Dada yangu mpendwa, hivi ndivyo inavyoanza, huwa tunaanza kwa kupoteza uhalisia na utambulisho wetu na kutoa visingizio vyake. Huku Kenya tulianza vivyo hivyo na Muziki wetu ukapotea” “Bongofleva iko SAWAA kabisa na hakuna haja ya kuwaacha Bongo Fleva ati kwa ajili ya ‘diversify’ Amapiano ni Basi tu linapita ila sisi tundapanda bila kujua linaenda wapi, tutashindwa kurudi nyumbani.tutakuwa tunauza sera zao na kushindwa kurundi nyumbani. tutakuwa tunauza tamaduni zao na kuua zetu za nyumbani” Mchekeshaji Omondi alinakiri” “Unapoimba ‘Sukari’ kwa sauti hiyo tamu ya kweli ya bongo na mdundo . unachofanya kimsingi ni kuinua na taifa na Bendera ya Tanzania”alisema Eric Omondi.

Read More
 ERIC OMONDI AWATOLEA UVIVU WASANII TANZANIA, ADAI MUZIKI WA BONGOFLEVA UMEKUFA

ERIC OMONDI AWATOLEA UVIVU WASANII TANZANIA, ADAI MUZIKI WA BONGOFLEVA UMEKUFA

Baada ya kuuzungumzia sana muziki wa Kenya kiasi cha kukamatwa na polisi , akidai kuwa muziki Kenya unakufa na wasanii wake hawajitumi, mchekeshaji maarufu nchini Eric Omondi ameugeukia muziki wa Bongofleva na wasanii wake akidai muziki wa amapiano unaua utambulisho wa muziki wa Bongofleva kutoka Tanzania. Kupitia ukurasa wake wa Instagram mchekeshaji huyo mwenye zaidi ya wafuasi million 3.7 ameeleza kuwa kwa ukanda wa Afrika Mashariki muziki wa bongofleva ndio ulikuwa kama utambulisho wa Ukanda huu lakini kwa kuiga muziki wa Amapiano ,muziki wa bongo fleva umepotea. Omondi amewataka wasanii wa Tanzania kuamka na kurudi katika utambulisho wao wa Bongofleva huku akidai kuwa wakenya wamelala , na inafaa watanzania warejee kwa upesi kwenye muziki wao kabla ya muda kuisha. EAST AFRICA I am SAD!!! I Weep for my PEOPLE😥😥😥. Nina Huzuni Moyoni😥. Bongo flava has always been East Africa’s PRIDE ila Kwa sasa IMEKUFAA. Kila Tanzania Artist Kwa sasa Anaimba Amapiano. We have lost our CULTURE, Killed our Own!!! Tumekaribisha, tumeiga, tumeichukua Tabia na Mwenendo zake Jirani tukajisahau wenyewe😥😥😥. We are LOSING OUR IDENTITY, OUR PRIDE!!! Naomba ndugu Zangu Wa BONGO Turejee kwa upesi before it’s too late!!! Wakenya WAMELALA, Wa Tanzania WAMEJIPOTEZAA. Mungu TUHURUMIE, TUREHEMU🙏🙏😥😥…aliandika Omondi kupitia Instagram yake

Read More
 NADIA MUKAMI AMCHANA ERIC OMONDI, ADAI ANATUMIA MUZIKI WA KENYA KUJITAFUTIA UMAARUFU

NADIA MUKAMI AMCHANA ERIC OMONDI, ADAI ANATUMIA MUZIKI WA KENYA KUJITAFUTIA UMAARUFU

Staa wa muziki nchini Nadia Mukami ametolea uvivu Eric Omondi baada ya mchekeshaji huyo kudai wasanii wa kenya wataendelea kudharauliwa hadi pale watakapoacha tamaa na uzembe kwenye kazi zao za muziki. Kupitia ukurasa wake wa Instagram amemtaka Omondi aache suala la kujipendekeza katika ishu ya kupigania mabadiliko kwenye muziki wakenya ikizingatiwa kuwa ni suala mtambuka ambalo linahitaji kuzungumziwa kwa kina. Hitmaker huyo “Roho Mbaya” ameenda mbali na kuonyosha maelezo kuhusu ya kufukuzwa na promota kwenye tamasha lilofanyika majuzi huko Mombasa kwa kusema kwamba hakutaka kupishana na waandaji wa tamasha hilo kwani hapendi kutumia nguvu kwenye kazi zake. Kauli ya Nadia Mukami inakuja mara baada ya kudaiwa alitimuliwa na msanii  mwenzake Masauti wakiwa jukwaani kumpisha msanii wa bongofleva mbosso kwenye tamasha la Bright Future lilofanyika mombasa wikiendi hii iliyopita.

Read More