Gravity Omutujju Amaliza Urafiki na King Saha kwa Uchungu Mwingi

Gravity Omutujju Amaliza Urafiki na King Saha kwa Uchungu Mwingi

Msanii wa muziki wa hip-hop nchini Uganda, Gravity Omutujju, amezungumza kwa mara ya kwanza kwa kina kuhusu kuvunjika kwa urafiki wake na mwanamuziki King Saha, akifichua kuwa hana tena uhusiano wowote naye. Wawili hao walikuwa marafiki wa karibu kwa muda mrefu na walishirikiana katika kibao kilichopata umaarufu kiitwacho “Winner”. Hata hivyo, uhusiano wao uliingia doa mwezi Septemba mwaka jana baada ya King Saha kusherehekea hadharani kufeli kwa tamasha la Gravity, kitendo kilichomvunja moyo na kumwacha na maumivu makali. Akizungumza katika mahojiano ya hivi karibuni, Gravity alisema wazi kuwa hana nia ya kurejesha urafiki huo, licha ya kutokuwa na chuki ya moja kwa moja. “Sina ugomvi naye, lakini si rafiki yangu tena. Sitaki kuwa na uhusiano wowote naye. Tulikuwa marafiki wa dhati, lakini niliumia sana kwa alichokifanya. Siwezi kumsamehe, wala kusahau,” alieleza kwa hisia. Kauli hiyo imezua gumzo kwenye mitandao ya kijamii, ambapo mashabiki wameonyesha hisia mseto, wengine wakisikitishwa na kuvunjika kwa urafiki huo, huku baadhi wakimuunga mkono Gravity kwa msimamo wake. Ingawa haijulikani iwapo wawili hao wataweza kusameheana na kurejesha urafiki wao wa zamani, kwa sasa, dalili zote zinaonyesha kuwa mlango huo umefungwa kabisa.

Read More
 Gravity Omutujju Atangaza Mapenzi Hadharani Kwa Mke wa Bebe Cool

Gravity Omutujju Atangaza Mapenzi Hadharani Kwa Mke wa Bebe Cool

Msanii maarufu wa muziki wa Hip Hop nchini Uganda, Gravity Omutujju, amezua gumzo mitandaoni baada ya kukiri wazi kuwa ana hisia za kimapenzi kwa Zuena Kirema, mke wa mwanamuziki mashuhuri Bebe Cool. Katika mahojiano na TikToker mmoja maarufu, Gravity alifunguka kwa mara ya kwanza kuhusu hisia zake kwa Zuena, akieleza kuwa amekuwa na “crush” naye kwa muda mrefu, na licha ya ndoa ya Zuena na Bebe Cool kuwa imara, bado anampenda kisiri. “Sijawahi kumuambia lakini ukweli ni kwamba nina ‘crush’ naye. Ni mwanamke mrembo sana, na hata kama ameolewa, siwezi kuficha hisia zangu,” alisema Gravity kwa ucheshi. Zuena Kirema, ambaye ameolewa na Bebe Cool kwa zaidi ya muongo mmoja na wana watoto pamoja, hajatoa tamko lolote kuhusu kauli hiyo ya Gravity. Bebe Cool pia hajaonekana kuguswa moja kwa moja na taarifa hiyo, ingawa mashabiki wake wengi wameonyesha mshtuko na wengine kuchukulia kama mzaha wa kawaida wa mastaa.

Read More
 Rapa Gravity Omutujju akiri kumchukia Spice Diana na meneja wake Rodger Lubega

Rapa Gravity Omutujju akiri kumchukia Spice Diana na meneja wake Rodger Lubega

Rapa Gravity Omutujju na Spice Diana walikuwa marafiki wakubwa sana kwa muda mrefu hadi alipokosana kutokana na sababu ambazo hawakuweka wazi. Wakati wa mahojiano hivi karibuni, Gravity amefichua kwamba anachukia uongozi wa Spice Diana kiasi kwamba hakutaka kusikia chochote kuhusu tamasha la mrembo huyo lililokamilika hivi karibuni. “Sikusikia kuhusu tamasha lake. Sikujua chochote kuhusu yeye pamoja na meneja wake. Siwapendi,” alisema kwenye mahojiano na Galaxy TV. Rapa huyo ameendelea kumlaani meneja wa Spice Diana, Rodger Lubega kwa madai ya kuwa mtu mbaya ambaye amekuwa akihujumu shughuli za watu.

Read More
 Gravity Omutujju Ajibu Madai ya Bebe Cool Kwamba Haogi

Gravity Omutujju Ajibu Madai ya Bebe Cool Kwamba Haogi

Rapa Gravity Omutujju amejibu madai ya Bebe Cool kuwa anapaswa kuoga kila mara ili aweze kufikia kiwango chake cha maisha. Hii ni baada ya Omutujju kumtaka bosi huyo wa Gagamel kustaafu muziki na kuwapa nafasi vijana wachanga waendeleze gurudumu la kuupeleka muziki wa Uganda kimataifa. Sasa kupitia mitandao yake ya kijamiii rapa huyo amesema kuwa yeye huwa anazingatia sana masuala ya usafi kwa kuoga kila siku, hivyo Bebe Cool hapaswi kutumia suala hilo kuficha ukweli kwamba anatakiwa kustaafu muziki. “Tunaoga na kuvaa vizuri, kwa kweli hata tunanukia vizuri. Unaogopa uhalisia na mabadiliko. #kizazi kipya kinatawala duniani kote,” Gravity alichapisha kwenye mitandao yake ya kijamii.

Read More
 Bebe Cool amjibu Gravity Omutujju kuhusu kustaafu muziki

Bebe Cool amjibu Gravity Omutujju kuhusu kustaafu muziki

Mwanamuziki kutoka nchini Uganda Bebe Cool amemjibu Gravity Omutujju baada ya rapa huyo kumshauri astaafu muziki kwa kuwa ana umri mkubwa. Kwenye mahojiano yake hivi karibuni Bebe Cool amemtaka rapa huyo kumlipa pesa kama anatamani aache muziki. Utakumbuka baada ya Gravity kupata mapokezi kwenye show yake miezi kadhaa huko Cricket Oval, Lugogo aliibuka na kuwachana wasanii bebe cool jose chameleone na Bobi wine akiwashauri wageukia masuala ya kilimo na kuachia wasanii kizazi kipya kuendelea na muziki. Alienda mbali zaidi na kutoa orodha ya wanamuziki bora nchini Uganda na kuwaacha nje wasanii hao watatu.

Read More
 Eddy Kenzo amtabiria mema Gravity Omutujju licha ya watu kumshambulia mtandaoni

Eddy Kenzo amtabiria mema Gravity Omutujju licha ya watu kumshambulia mtandaoni

Mwanamuziki Eddy Kenzo amemtabiria mema rapa Gravitty Omutujju kwa kusema kuwa atapata mafanikio makubwa kwenye muziki wake licha ya watu kumpiga vita kila mara kwenye shughuli zake. Kwemye mahojiano yakw hivi karibuni Kenzo amesema omutujju hatoshushwa kisanaa na baadhi ya watu wanaojaribu kumshambulia mtandaoni kwani ni moja kati ya watu ambao wamepitia maisha ya taabu.. “Nilimtoa Gravity kutoka mitaa ya banda. Alikuwa analala chumba kimoja na mama yake mzazi pamoja na dada yake. Ana ujasiri kwa kile anachokifanya najua atafika mbali, hivyo hakuna mtu ambaye atamshusha kisanaa mapema, ana moyo mugumu wa kupigana na matatizo”, Alisema. Eddy Kenzo ambaye alimtoa kimuziki Rapa Gravityy Omutujju chini ya lebo yake ya muziki ya Big Talent, anatarajiwa kufanya tamasha lake la muziki Novemba 9 mwaka huu huko Kololo Airstrip nchini Uganda.

Read More
 Ykee Benda amkingia kifua Gravity Omutujju kwa kuwavunjia heshima wasanii wakongwe.

Ykee Benda amkingia kifua Gravity Omutujju kwa kuwavunjia heshima wasanii wakongwe.

Bosi wa lebo ya mpaka Records, Ykee Benda amemkingia kifua rapa Gravity Omutujju kutokana na kauli yenye utata aliyotoa juzi kati dhidi ya wasanii Bobi Wine, Bebe Cool na Jose Chameleone. Kwenye mahojiano yake hivi karibuni Ykee amesema hatua ya Omotujju kuwataka wasanii hao kustaafu muziki na kuwaapisha wasanii wajanga ilikuwa njia ya rapa huyo kutengeneza mazingira ya kuzungumzia mtandaoni. Ykee Benda amesema kauli ya hitmaker huyo wa “Enyama” haikulenga kumvunjia heshima msanii yeyote bali alitoa matamashi hayo kwa ajili ya kuteka hisia za mashabiki kabla kuachia wimbo wake mpya. Hata hivyo amewalaumu wasanii wakongwe kwa kuwaaminisha wasanii wajanga kuwa hawezi toboa kisanaa bila kujihusisha na matukio yenye ukakasi. Utakumbuka baada ya Gravity Omutujju kuwataka wasanii Bobi Wine, Bebe Cool na Jose Chameleone alikashifiwa na baadhi ya wasanii pamoja na mashabiki jambo ambalo lilimlazimu kuomba radhi kwa kuwavunjia heshima wasanii hao mbele ya waandishi wa habari.

Read More
 Gravity Omutujju amwaga machozi baada ya familia yake kushambuliwa mtandaoni

Gravity Omutujju amwaga machozi baada ya familia yake kushambuliwa mtandaoni

Rapa Gravity Omutujju amejipata akiangua kilio hadharani kwa kile alichokitaja kuzidiwa na mashambulizi ya walimwengu dhidi ya familia yake kwenye mitandao ya kijamii. Katika kikao na wanahabari Omutujju amesema kauli yake kuhusu wasanii Bobi Wine, Jose Chameleone na Bebe Cool ilikunuliwa vibaya na mitandao mbali mbali ya burudani nchini Uganda, kitendo ambacho amedai kimewafanya watu kumzushia kila aina matusi kiasi cha kuwaingiza watoto na mke wake kwenye purukushani hiyo. Hata hivyo hitmaker huyo “Enyama” ambaye amekuwa akijigamba mtandaoni, amelazimika kuomba radhi kwa matamshi yake ya chuki dhidi ya wasanii hao wakongwe kwani huenda ikachafua brand yake ya muziki ambayo ameipambania kwa miaka mingi. Kwa muda wiki moja sasa Gravity Omutujju amekuwa gumzo mtandaoni alipojaza ukumbi wa Cricket Oval kupitia tamasha lake lakini pia kuhusu kauli tata aliyotoa dhidi ya wasanii Bobi Wine, Jose Chameleone na Bebe Cool ambapo alinukuliwa akiwataka wastaafu muziki na kuwapisha wasanii wapya waendeleza harakati ya kuupeleka muziki wa Uganda kimataifa.

Read More
 Mashabiki waharibu mali ya thamani kubwa baada ya Gravity Omutujju kususia shoo

Mashabiki waharibu mali ya thamani kubwa baada ya Gravity Omutujju kususia shoo

Mwanamuziki kutoka nchini Uganda Gravity Omutujju ameingia tena kwenye headlines mara baada ya kususia moja ya onesho lake huko Lukaaya. Duru za kkuaminika zinasema mashabiki walimsubiri pallaso kwa takriban masaa matatu lakini msanii huyo hakutokea kwenye performance yake, jambo lilowafanya mashabiki kuzua vurugu na kuaharibu kila kitu kwenye ukumbi wa burudani Royal Gardens  na kuacha mapromota wakikadiria hasara ya mamilioni ya pesa. Juhudi za walinzi kuwatuliza mashabiki ziliambulia patupu kwani walionekana wenye hasira zaidi wakiwataka waliondaa onesho hilo kuwaregeshea pesa zao kwa kushindwa kutimiza ahadi ya kumleta Gravity Omutujju jukwaani awape burudani. Hata hivyo Mmiliki wa ukumbi wa Royal Gardens  ametaka usimamizi wa Kev Motors na Humble uliohusika kuandaa tamasha la Gravity Omutujju kulipia mali iliyoharibiwa ambayo thamani yake ni zaidi ya Shillingi 1.2m.

Read More
 Gravity Omutujju kuacha muziki wa Hiphop

Gravity Omutujju kuacha muziki wa Hiphop

Rapa kutoka nchini Uganda Gravity Omutujju anafikiria kuacha kabisa kufanya muziki wa Hiphop na kuhamia kwenye muziki wa RnB.. Kwenye mahojiano yake hivi karibuni Hitmaker huyo wa “Enyama” amesema anabadilisha aina ya muziki wake kutokana na muziki wa Hiphop kukosa ushindani nchini Uganda. “I am tired of rap. I want to try RnB. I have no competition in the rap game and it is now boring,” alisema Gravity Omutujju Kauli yake imekuja mara baada ya kutamba kuwa mwanamuziki bora nchini Uganda kuliko Jose Chameleone, Bobi Wine na Bebe Cool kufuatia hatua ya kuujaza ukumbi wa Cricket Oval, Lugogo kwa mara ya nne mfululizo.

Read More
 Gravity Omutujju mbioni kuwekeza kwenye shughuli ya kuandaa matamasha ya muziki

Gravity Omutujju mbioni kuwekeza kwenye shughuli ya kuandaa matamasha ya muziki

Rapa Gravity Omutujju amedokeza mpango wa kuwekeza biashara ya kuwasimamia wasanii na kuandaa matamasha ya muziki. Kwenye mahojiano yake hivi karibuni amesema amechukua hatua hiyo kwa  sababu mapromota wengi wamekuwa wakiingiza pesa nyingi kupitia matamasha ya muziki. Hitmaker huyo wa “Enyama” amesema ana uwezo wa kufanya muziki sambamba na kuwasimamia kwa wakati mmoja bila changamoto yeyote. “I’m going to start promoting musicians and organizing their events because I have seen there is money. I will take on a musician and have them perform here by January,” alisema kwenye mahojiano yake Utakumbuka tamasha la Gravity Omutujju ambalo lilifanyika huko Cricket oval lugogo lilitayarisha na kampuni ya Balaam marketing and Promotions.

Read More
 Gravity Omutujju aandika Cricket Oval, Lugogo kupitia tamasha la Tusimbudde

Gravity Omutujju aandika Cricket Oval, Lugogo kupitia tamasha la Tusimbudde

Rapa kutoka Uganda Gravity Omutujju ameshindwa kuficha furaha yake baada ya watu zaidi ya 30, 000 kujaza ukumbi wa Cricket Oval Lugogo usiku wa kuamkia leo kwenye tamasha lake la muziki llitwalo “Tusimbudde” Kupitia ukurasa wake wa Instagram Hitmaker huyo wa “Enyama” amemshukuru mwenyezi Mungu na mashabiki zake kwa kumuonyesha upendo kipindi ambacho walimwengu walikuwa wanasubiri anguko lake kwenye muziki. Utakumbuka mwaka 2017 Omutujju alijaza nyomi la mashabiki katika ukumbi wa Cricket Oval Lugogo huko Jijini Kampala ambako alipiga show ya kufa mtu iliyowaacha mashabiki wakiwa na kiu ya kutaka burudani zaidi.

Read More