OTILE BROWN ASIFIA UWEZO WA HARMONIZE KWENYE NGOMA YAO YA KWANZA

OTILE BROWN ASIFIA UWEZO WA HARMONIZE KWENYE NGOMA YAO YA KWANZA

Mkali wa muziki nchini Otile Brown amesifia uwezo wa msanii wa Bongofleva Harmonize katika verse ya wimbo wao wa pamoja waliofanya kwa mara ya kwanza. Otile Brown ametumia insta story yake kwenye mtandao wa Instagram  kuelezea hilo, ambapo amesema Harmonize amefanya vizuri katika ngoma hiyo huku akieleza fahari yake kwa mashabiki wa Tanzania na Kenya ambao watakua tayari kusikia kazi hiyo. Hivi karibuni Harmonize  akiwa nchini katika ziara yake ya kimuziki alitangaza wazi kuja na ‘EP’ itakayo kuwa na nyimbo 5 za pamoja kati yake na Otile Brown.

Read More
 HARMONIZE & OTILE BROWN KUJA NA EP YA PAMOJA YENYE NYIMBO 5

HARMONIZE & OTILE BROWN KUJA NA EP YA PAMOJA YENYE NYIMBO 5

Nyota wa muziki wa Bongofleva Harmonize ametangaza ujio wa EP ya pamoja mkali wa muziki nchini Otile Brown. Harmonize ameweka wazi hilo akiwa jukwaani kwenye tamasha la Afro Vasha Disemba 12 mwaka huu huko Naivasha ambapo amesema EP hiyo itakuwa na Jumla ya mikwaju 5 ya moto. Hajabainika kama EP hiyo ni ile Harmonize alituahidi atawashirikisha wasanii 5 wa Kenya wenye vipaji bila kuangalia ukubwa wa msanii ila ni jambo la kusubiriwa. Ikumbukwe kabla ya Hitmaker huyo wa Teacher kutua nchini Kenya alidokeza mpango wa kufanya ziara ya kimuziki kwenye miji kumi za Kenya ambapo aliwapa nafasi mashabiki wapendekeze majina ya miji ambayo wangependa afanye tamasha lake la muziki.

Read More
 20 PERCENT AMJIBU HARMONIZE

20 PERCENT AMJIBU HARMONIZE

Hatimaye ahadi ya Harmonize ya kuingia studio na kufanya kolabo na 20 percent pindi tu akitua Tanzania kutoka nchini Marekani imepokelewa kwa mikono miwili na mkali huyo wa zamani. 20 Percent ametumia insta story yake kwenye mtandao wa Instagram kumjibu Harmonize kuwa “Promise is like a debt”  kwa maana yupo tayari hivyo Harmonize atimize alichokiahidi. 20 percent ambaye ni mshindi wa tuzo tano za Kili Music Awards mwaka wa 2010, aliwahi kutamba na ngoma kama Maisha ya Bongo, Mama Neema, Money Money, Tamaa Mbaya na nyingine kibao. Haya yanajiri baada ya usiku wa kuamkia Oktoba 25 kuwa mrefu sana kwa harmonize ambaye alionekana akiburudika na midundo ya 20 Percent na kupelekea kutoa ahadi ya kufanya nae kolabo, sambamba na kueleza kuwa ni ndoto yake ya muda mrefu.

Read More
 HARMONIZE ATANGAZA TAREHE YA KUACHIA ALBUM YAKE MPYA

HARMONIZE ATANGAZA TAREHE YA KUACHIA ALBUM YAKE MPYA

Msanii wa Bongofleva Harmonize hatimaye ameiweka wazi tarehe ya kuiachia album yake mpya iitwayo “High School”. Album hiyo ambayo ilipaswa itoke mwezi huu wa haitotoka kutokana na sababu mbalimbali hivyo imesogezwa mbele hadi Novemba 5 mwaka huu. Hii ni habari njema kwa mashabiki wa mkali huyo wa “Teacher” ambao wanaisubiri “High School album” kwa hamu kubwa. Ikumbukwe, hii inaenda kuwa album ya pili kwa mtu mzima Harmonize baada ya “Afro East” iliyotoka mwezi Machi mwaka wa 2020.

Read More
 AFRO EAST ALBUM YA HARMONIZE YAFIKISHA ZAIDI YA STREAMS MILLIONI 2.5 BOOMPLAY

AFRO EAST ALBUM YA HARMONIZE YAFIKISHA ZAIDI YA STREAMS MILLIONI 2.5 BOOMPLAY

Album ya Mwanamuziki harmonize iliyotika Machi 14 mwaka wa 2020 Afro East yenye nyimbo 17 imefanikiwa kufikisha jumla ya streams Million 2.5 katika mtandao wa boom play music.   Kwa upande wa Album, album yenye streams nyingi katika mtandao huo kwa wanamuziki wa tanzania ni album ya Mwanamuziki rayvanny Sound From Africa ambayo ina jumla ya streams millioni 15.5 katika mtandao huo maarufu wa kusimamia na kuuza kazi za muziki.   Sound From Africa album ya mtu mzima Rayvanny iliingia sokoni Rasmi februari mosi mwaka huu ikiwa na jumla ya mikwaju 23 ya moto            

Read More