Iyanii Aahidi Kutoa Mapato Yake ya Muziki Kwa Wafungwa
Msanii wa muziki nchini Kenya, Iyanii, amewagusa wengi baada ya kutangaza uamuzi wake wa kusaidia wafungwa kupitia mapato ya muziki wake. Kupitia podcast ya Mic Check, Iyanii amesema ameahidi kutenga asilimia 20 ya mapato yote atakayopata kutokana na muziki wake ili kuwasaidia watu walioko magerezani. Msanii huyo amesema hatua hiyo inalenga kuwapa wafungwa matumaini na kuwasaidia kuboresha maisha yao wakiwa kifungoni, akisisitiza kuwa kila mtu anastahili nafasi ya pili maishani. Iyanii ameendelea kusisitiza kuwa muziki kwake si burudani pekee, bali ni njia ya kurudisha kwa jamii na kugusa maisha ya watu wanaohitaji msaada.
Read More