CHAMELEONE ACHUKUA MAPUMZIKO MAFUPI KWENYE MUZIKI WAKE

CHAMELEONE ACHUKUA MAPUMZIKO MAFUPI KWENYE MUZIKI WAKE

Nguli wa muziki kutoka nchini Uganda Jose Chameleone amekuwa akifanya kazi ya muziki kwa takriban miongo mitatu bila kupoa. Baada ya kuachia nyimbo kali zilizokonga nyoyo za wapenzi wa muziki mzuri Afrika Mashariki, mkali huyo wa ngoma ya “Mama Mia” ametangaza kuchukua mapumziko ya miezi mitatu kwenye muziki wake. Vyanzo vya karibu na Jose Chameleone,vimedai kuwa msanii huyo amechukua hatua hiyo kwa ajili ya kusafiri nchini Marekani kuonana na familia yake kwani mara ya mwisho kutua nchini humo ilikuwa mwaka wa 2019. Taarifa hii inakuja mara baada ya bosi huyo wa Leone Island kupata VISA ya kwenda nchini Marekani wiki kadhaa zilizopita.

Read More
 CHAMELEONE AWAPA SOMO MASHABIKI

CHAMELEONE AWAPA SOMO MASHABIKI

Lejendari wa muziki kutoka nchini Uganda Jose Chameleone amewapa somo mashabiki wanaomkosoa kwa kufanya kazi na serikali ya rais Yoweri Museveni. Katika performance yake katika kumbukiza ya General. Muhoozi huko Cricket Oval, Lugogo chameleone amedai kuwa hatokubali kuvunjiwa heshima na mashabiki wanaomtaka afuate wanachokisema mtandaoni kwa kusema kwamba yeye ni mtu mzima na hawezi kupangiwa maisha. Hitmaker huyo wa ngoma ya “Bei Kali” amesema hajali tena namna watu wanavyomchukulia kwenye mitandao ya kijamii kwa kuwa tayari ameshastaafu siasa. Inaripotiwa kuwa Chameleone na Bebe Cool ndio wasanii waliolipwa mkwanja mrefu kwenye hafla ya kumbukizi ya General. Muhoozi ambaye ni mwanawe Yoweri Museveni.

Read More
 CHAMELEONE AFUNGUKA CHANZO CHA UGOMVI WAKE NA BOBI WINE

CHAMELEONE AFUNGUKA CHANZO CHA UGOMVI WAKE NA BOBI WINE

Msanii mkongwe kwenye muziki nchini Uganda Jose Chameleone amekiri hadharani kwamba hana uhusiano mzuri na msanii mwenzake Bobi Wine ambaye aligeukia siasa. Akiwa kwenye moja ya onesho lake huko Kyengera Chameleone amedai kuwa Bobi wine alimnyima tiketi ya kugombea wadhfa wa umeya wa jiji la kampala kupitia chama chake cha NUP kwenye uchaguzi mkuu uliopita nchini uganda. Hitmaker huyo wa ngoma ya “Forever” amesema jambo hilo lilimfanya apoteze imani kwenye siasa na sasa ameamua kuelekeza nguvu zake zote kwenye muziki kwani ni kitu anachokifahamu kwa undani. “Sitaki kumzungumzia alininyima tiketi ya chama chake. Nimepoteza imani kwenye wadhfa wa umeya. Kwa sasa nimelekeza nguvu zangu kwenye muziki kitu ninachokifahamu kwa undani,” Alisema. Chameleone ambaye ni bosi wa Lebo ya muziki ya Leone Island amesema anajihisi mwenye furaha zaidi akiwa karibu na wasanii kama Bebe Cool, Eddy Kenzo na David Lutalo na wengine wengi.

Read More
 JOSE CHAMELEONE AKIRI KUSHINDWA NA MASUALA YA SIASA

JOSE CHAMELEONE AKIRI KUSHINDWA NA MASUALA YA SIASA

Msanii nguli kutoka Uganda Jose Chameleone amekiri kutokuwa na bahati kwenye masuala ya siasa ikiwa ni mwaka mmoja tangu apoteze kiti cha umeya wa jiji la kampala kwa mpinzani wake Erias Lukwago katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2021. Akizungumza kwenye moja ya show huko Mukono Chameleone amesema amekubali hatma yake kwenye siasa huku akidai bado ana ari ya kutaka kujua kiini cha watu kutompigia kura kwenye wadhfa wa umeya licha ya kuwa na mashabiki wengi katika muziki wake. Bosi huyo wa Leone amethibitisha kutorudi tena kwenye masuala ya siasa na badala yake ataelekeza nguvu zake kufanya muziki ambao umekuwa ukimuingizia kipato kwa miaka nyingi. Hata hivyo amedokeza ujio wa show kubwa kati yake  na bebe  cool baada ya show yao iitwayo The Battle of champions iliyokuwa ikiwashindanisha huko Mukono nchini Uganda kupata mapokezi mazuri kutoka kwa mashabiki zao.

Read More
 CHAMELEONE: KOLABO ZA KIMATAIFA HAZINA MAANA KWA WASANII CHIPUKIZI

CHAMELEONE: KOLABO ZA KIMATAIFA HAZINA MAANA KWA WASANII CHIPUKIZI

Lejendari wa muziki kutoka nchini Uganda Jose Chameleone amedai kwamba kufanya kolabo na mastaa wa kubwa duniani haina faida yeyote kwa msanii. Katika mahojiano yake hivi karibuni Chameleone amesema haamini katika suala la kufanya kolabo na wasanii wakubwa duniani ili kupenya kwenye soko la kimataifa. Hitmaker huyo wa ngoma ya “Forever” amesema kolabo hizo hazina maana kwa sababu mastaa hao hushindwa kuitangaza kolabo zenyewe kwenye nchini zao na badala yake mzigo wa kuitangaza project husika ubaki upande mmoja. Chameleone ni moja kati ya wasanii nchini uganda waliofanya kazi ya pamoja na mastaa kubwa duniani kama vile Beenie Man, Davido, Sizzla,Koffi Olomide na wengine wengi.

Read More
 JOSE CHAMELEONE AMWAGIA SIFA MSANII CHIPUKIZI ALLAN HENDRICK, AAHIDI KUSIMAMIA MUZIKI WAKE

JOSE CHAMELEONE AMWAGIA SIFA MSANII CHIPUKIZI ALLAN HENDRICK, AAHIDI KUSIMAMIA MUZIKI WAKE

Mkongwe wa muziki nchini uganda Jose Chameleone amehapa kukuza muziki wa msanii Allan Hendrick kwani ni kijana ambaye ana ari ya kutaka kufanya makubwa kwenye muziki wake. Katika mahojiano yake hivi karibuni Bosi huyo wa leone island amemwagia sifa msanii huyo chipukizi kwa kumtabiria mema kuwa atakuja kuwa msanii mkubwa kwenye kiwanda cha muziki nchini uganda kutokana na kipaji chake cha kipekee katika muziki wake. Kauli ya Chameleone imekuja mara baada ya kuonekana katika siku za hivi karibuni akitumia muda wake mwingi kukaa na Allan Hendrick ambaye ni kijana wa msanii mwenzake Bebe Cool. Utakumbuka msanii Bebe cool amekuwa akikosolewa na watu kwa kutompa support kijana wake Allan Hendrick  kutokana na hatua yake ya kumuacha akipambana mwenyewe kwenye muziki wake licha ya bebe cool kumiliki lebo ya muziki ya Gagamel ambayo ina uwezo wa kukuza kipaji cha msanii huyo.

Read More
 JOSE CHAMELEONE AKIRI BIFU LAKE NA WASANII GOODLYFE CREW LILIMSAIDI KUKUA KIMUZIKI

JOSE CHAMELEONE AKIRI BIFU LAKE NA WASANII GOODLYFE CREW LILIMSAIDI KUKUA KIMUZIKI

Msanii mkongwe kwenye muziki nchini Uganda Jose Chameleone amekiri kuwa bifu yake na wasanii wa Goodlyfe Crew Mozey Radio na  Weasel Manizo lilimsaidia kukua kimuziki. Katika mahojiano yake ya hivi karibuni Chameleone amesema kuwa bifu zinasaidia kukuza muziki kwani kipindi cha nyuma alipokuwa anajibu diss tracks za wasanii hao kwa kuachia ngoma alizungumziwa sana kwenye tasnia ya muziki nchini Uganda. Lakini pia ugomvi wake  na wasanii wa Goodlife Entertainmet uliwatengenezea wasanii hao brand yao ya muziki. Utakumbuka mwaka wa 2005 wasanii wa Goodlyf Crew walikuwa kwenye ugomvi mkali na chameleone jambo lilowafanya kuachia nyimbo za kumshambulia chameleone wakimtaja kama shetani lakini pia msanii wa mashinani. Hata hivyo walikuja baadae wakaweka kando tofauti zao kwa faidi ya wapenzi wa muziki mzuri nchini Uganda ambao waliingia kati na kuwataka wasanii hao waache ishu ya kuendekeza chuki na badala yake washirikiane kwenye shughuli zao za kimuziki.

Read More
 JOSE CHAMELEONE AFUNGUKA SABABU ZA KUTOACHA MUZIKI

JOSE CHAMELEONE AFUNGUKA SABABU ZA KUTOACHA MUZIKI

Msanii mkongwe kwenye muziki nchini Uganda Jose Chameleone amefunguka sababu za kutostaafu kwenye muziki licha ya kufanya kazi hiyo kwa zaidi ya miaka 20. Katika mahojiano yake ya hivi karibuni Chameleone amesema muziki upo ndani damu yake na hivyo haoni kabisa akiacha kuimba. Bosi huyo wa lebo ya Leone Island amesema hafanyi tena muziki kwa shinikizo za kupata pesa kama miaka ya hapo nyuma kwa sababu ana mali nyingi. “Sasa natoa muziki ninapojisikia kwa sababu sifanyi kwa ajili ya kujinufaisha kifedha. Tayari nina mali,” alisema katika mahojiano na runinga moja nchini Uganda. Ikumbukwe Jose Chameleone amejipatia mali nyingi kupitia muziki wake na anaendelea pia kuwekeza kwenye biashara mbali mbali. Hitmaker huyo wa ngoma ya “Forever” ana mjengo wa kifahari huko Seguku nchini Uganda lakini pia inasemekana kuwa ana nyumba mbili nchini Marekani.

Read More
 JOSE CHAMELEONE AWACHANA WANAOPENDA KWENDA GYM, ADAI NI WAVIVU

JOSE CHAMELEONE AWACHANA WANAOPENDA KWENDA GYM, ADAI NI WAVIVU

Mwanamuziki Jose Chameleone amewatolea uvivu watu wanaopenda kufanya mazoezi akiwataja kuwa ni wavivu ambao hawana chochote cha kufanya maishani mwao. Akiwa kwenye moja ya Interview Chameleone anasema aliwahi kwenda gym lakini aligundua kuwa alikuwa anapoteza muda wake mwingi, na hivyo akaamua kuacha. Hitmaker huyo wa “Baliwa” amesema alihamua kuwekeza muda wake katika kufanya kazi, na hiyo imemsaidia kupata kipato kizuri ambacho kinamsaidia kufanikisha baadhi mambo yake. Hata hivyo Chameleone anasema anarithika na muonekano wake kimwili ingawa kuna baadhi ya watu wanadai hana mwili wa masupastaa. Kwa upande mwake, msanii Bebe Cool anaamini kuwa mwanamuziki anahitaji kufanya mazoezi ili awe na muonekano mzuri kwa mashabiki wake.

Read More
 JOSE CHAMELEONE MBIONI KUACHIA COLLABO YAKE NA KOFFI OLOMIDE

JOSE CHAMELEONE MBIONI KUACHIA COLLABO YAKE NA KOFFI OLOMIDE

Bosi wa lebo ya muziki ya Leone Island Jose Chameleone amekuwa jamhuri ya demokrasi ya kongo kwa kipindi cha wiki moja sasa. Goods ni kuwa Chameleone ameonekana kuingia studio na nguli wa muziki barani afrika Koffi Olomide jambo linalotafsiri kuwa huenda kukawa na kazi ya pamoja baina ya wawili hao hivi karibuni. Duru za kuaminika zinasema wawili hao walitumbuiza pamoja mapema wiki hii huko Kinshasa ambapo walipiga shoo ya kufa mtu ambayo iliwavutia watu wengi zaidi. Jose chameleone anajiunga na wasanii wa afrika mashariki Diamond platinumz na Nandy ambao tayari wamefanya kazi na Koffi olomide ambaye ni moja kati ya wasanii wakubwa jamhuri ya demokrasia ya congo

Read More
 JOSE CHAMELEONE AMFUTA KAZI MENEJA WAKE BIJOU FORTUNATE KISA UZEMBE KAZINI

JOSE CHAMELEONE AMFUTA KAZI MENEJA WAKE BIJOU FORTUNATE KISA UZEMBE KAZINI

Bosi wa lebo ya leone island Jose Chameleone amemfuta kazi meneja wake Bijou Fortunate. Inadaiwa kuwa Bijou ameshindwa kumleta Chameleone dili kubwa za kimataifa kitu ambacho kimemfanya msanii huyo kutoridhika na utenda kazi wake. Hata hivyo duru za kuaminika zinasema kuwa chameleone anafadhalisha kufanya kazi na meneja wake zamani Robert Mutiima ambaye kipindi cha nyuma alimleta dili nyingi zilizomuingizia kipato. Ingawa hakuna tamko rasmi kutoka kwa Chameleone ila chanzo cha karibu na msanii huyo kinasema Robert Mutiima ameamuriwa kuchukua wadhfa wa umeneja wa kazi za Chameleone. Bijou alitambulishwa kama meneja wa Chameleone mwaka wa 2020 ila wengi walitilia shaka uwezo wake wa kusimamia kazi za msanii huyo ambapo walienda mbali zaidi na kusema kuwa mrembo huyo hawezi kaa mwezi mmoja lakini aliwashangaza wakosoaji wake.

Read More
 JOSE CHAMELEONE: SINA MPANGO WA KUREJEA TENA KWENYE SIASA

JOSE CHAMELEONE: SINA MPANGO WA KUREJEA TENA KWENYE SIASA

Bosi wa lebo ya muziki ya Leone Island msanii Jose Chameleone ameweka wazi kwamba hana mpango tena wa kuingia kwenye siasa. Chameleone amesema siasa inataka pesa nyingi sana na kwa mantiki hiyo itakuwa vigumu kwake kuwania wadhfa wowote wa kisiasa. Hata hivyo amesisitiza kwamba licha ya watu kutompigia kura kwa wingi kwenye uchaguzi mkuu uliopita nchini Uganda, anaamini hana vigezo vya kuwa kiongozi na ndio maana wananchi walimchagua mpinzani wake. Ikumbukwe Jose Chameolene alipoteza kwenye uchaguzi wa umeya wa Jiji la Kampala mapema mwaka huu na mpinzani wake Erias Lukwago.

Read More