JOSE CHAMELEONE AWACHANA WANAOPENDA KWENDA GYM, ADAI NI WAVIVU

JOSE CHAMELEONE AWACHANA WANAOPENDA KWENDA GYM, ADAI NI WAVIVU

Mwanamuziki Jose Chameleone amewatolea uvivu watu wanaopenda kufanya mazoezi akiwataja kuwa ni wavivu ambao hawana chochote cha kufanya maishani mwao. Akiwa kwenye moja ya Interview Chameleone anasema aliwahi kwenda gym lakini aligundua kuwa alikuwa anapoteza muda wake mwingi, na hivyo akaamua kuacha. Hitmaker huyo wa β€œBaliwa” amesema alihamua kuwekeza muda wake katika kufanya kazi, na hiyo imemsaidia kupata kipato kizuri ambacho kinamsaidia kufanikisha baadhi mambo yake. Hata hivyo Chameleone anasema anarithika na muonekano wake kimwili ingawa kuna baadhi ya watu wanadai hana mwili wa masupastaa. Kwa upande mwake, msanii Bebe Cool anaamini kuwa mwanamuziki anahitaji kufanya mazoezi ili awe na muonekano mzuri kwa mashabiki wake.

Read More
 JOSE CHAMELEONE MBIONI KUACHIA COLLABO YAKE NA KOFFI OLOMIDE

JOSE CHAMELEONE MBIONI KUACHIA COLLABO YAKE NA KOFFI OLOMIDE

Bosi wa lebo ya muziki ya Leone Island Jose Chameleone amekuwa jamhuri ya demokrasi ya kongo kwa kipindi cha wiki moja sasa. Goods ni kuwa Chameleone ameonekana kuingia studio na nguli wa muziki barani afrika Koffi Olomide jambo linalotafsiri kuwa huenda kukawa na kazi ya pamoja baina ya wawili hao hivi karibuni. Duru za kuaminika zinasema wawili hao walitumbuiza pamoja mapema wiki hii huko Kinshasa ambapo walipiga shoo ya kufa mtu ambayo iliwavutia watu wengi zaidi. Jose chameleone anajiunga na wasanii wa afrika mashariki Diamond platinumz na Nandy ambao tayari wamefanya kazi na Koffi olomide ambaye ni moja kati ya wasanii wakubwa jamhuri ya demokrasia ya congo

Read More
 JOSE CHAMELEONE AMFUTA KAZI MENEJA WAKE BIJOU FORTUNATE KISA UZEMBE KAZINI

JOSE CHAMELEONE AMFUTA KAZI MENEJA WAKE BIJOU FORTUNATE KISA UZEMBE KAZINI

Bosi wa lebo ya leone island Jose Chameleone amemfuta kazi meneja wake Bijou Fortunate. Inadaiwa kuwa Bijou ameshindwa kumleta Chameleone dili kubwa za kimataifa kitu ambacho kimemfanya msanii huyo kutoridhika na utenda kazi wake. Hata hivyo duru za kuaminika zinasema kuwa chameleone anafadhalisha kufanya kazi na meneja wake zamani Robert Mutiima ambaye kipindi cha nyuma alimleta dili nyingi zilizomuingizia kipato. Ingawa hakuna tamko rasmi kutoka kwa Chameleone ila chanzo cha karibu na msanii huyo kinasema Robert Mutiima ameamuriwa kuchukua wadhfa wa umeneja wa kazi za Chameleone. Bijou alitambulishwa kama meneja wa Chameleone mwaka wa 2020 ila wengi walitilia shaka uwezo wake wa kusimamia kazi za msanii huyo ambapo walienda mbali zaidi na kusema kuwa mrembo huyo hawezi kaa mwezi mmoja lakini aliwashangaza wakosoaji wake.

Read More
 JOSE CHAMELEONE: SINA MPANGO WA KUREJEA TENA KWENYE SIASA

JOSE CHAMELEONE: SINA MPANGO WA KUREJEA TENA KWENYE SIASA

Bosi wa lebo ya muziki ya Leone Island msanii Jose Chameleone ameweka wazi kwamba hana mpango tena wa kuingia kwenye siasa. Chameleone amesema siasa inataka pesa nyingi sana na kwa mantiki hiyo itakuwa vigumu kwake kuwania wadhfa wowote wa kisiasa. Hata hivyo amesisitiza kwamba licha ya watu kutompigia kura kwa wingi kwenye uchaguzi mkuu uliopita nchini Uganda, anaamini hana vigezo vya kuwa kiongozi na ndio maana wananchi walimchagua mpinzani wake. Ikumbukwe Jose Chameolene alipoteza kwenye uchaguzi wa umeya wa Jiji la Kampala mapema mwaka huu na mpinzani wake Erias Lukwago.

Read More
 CHAMA CHA UGANDA MUSICIANS FEDERATION CHAANZA ZOEZI LA KUWASAJILI WASANII

CHAMA CHA UGANDA MUSICIANS FEDERATION CHAANZA ZOEZI LA KUWASAJILI WASANII

Msanii nguli kutoka nchini Uganda Jose Chameleone amezindua zoezi la kuwasajili wasanii ambao wanatamani kujiunga na chama chake cha Uganda Musicians Federation. Ni Zoezi ambalo litaandeshwa na timu ya wataalam wa masuala ya muziki nchini Uganda ambao watawachagua  wasanii kutoka maeneo mbali mbali nchini Uganda. Ikumbukwe chama cha Uganda Musician Federation lilizunduliwa na Mwanamuziki Jose Chameleone  mwezi juni mwaka huu. Lengo kuu la kuanzishwa kwa chama hicho lilikuwa ni kuangazia maslahi ya wasanii nchini uganda ambao wamekuwa wakisuasua kimuziki. Chameleone aliweza kuwasajili wasanii kama Pallaso, Weasel, Feffe Buusi na wengine wengi. Chini ya mwongozo wake, walipata fursa ya kukutana na Jenerali Salim Saleh kutafuta msaada wa kifedha lakini wachache wao walipewa pesa taslimu. Wanamuziki waliokosa pesa hizo walihamua kumkimbia chameleone jambo lilomlazimu bosi huyo wa Leone island kuchukua mapumziko mafupi.

Read More