PENZI LA KANYE WEST NA CHANEY JONES LAVUNJIKA RASMI

PENZI LA KANYE WEST NA CHANEY JONES LAVUNJIKA RASMI

Rapper Kanye West (YE) na mpenzi wake mpya Chaney Jones wameachana. Tovuti ya TMZ imethibitisha taarifa hiyo kwa kusema kwamba wawili hao wamefikia ukomo wa penzi lao baada ya ziara ndefu nchini Japan. Hakuna taarifa za yupi aliyempiga chini mwenzie lakini taarifa hizi zinakuja ikiwa ni siku chache baada ya kuonekana picha ya Kanye West akicheki movie na mwanamke mwingine. Kanye West (YE) na Chaney walianza kuonekana hadharani mwezi Februari mwaka huu na tayari mwanadada huyo alishachora Tattoo yenye jina ‘YE’ mkononi.

Read More
 KANYE WEST MBIONI KUJA NA FILAMU YA MAISHA YAKE

KANYE WEST MBIONI KUJA NA FILAMU YA MAISHA YAKE

Rapper Kanye West amedokeza mpango wa kuja na filamu ya maisha yake. Kanye amemuomba mwigizaji Danny McBride kuvaa uhusika wake na kucheza filamu hiyo. McBride amethibitisha taarifa hiyo kwenye podcast ya Jimmy Kimmel Live kwenye mtandao wa Youtube kwa kusema kwamba YE alimpigia simu na kumpa ombi hilo. Mwigizaji huyo ambaye pia ni mchekeshaji wa nchini Marekani amesema alilipokea kwa mikono miwili wazo hilo la Kanye West. Utakumbuka Danny McBride alipatia umaarufu mkubwa kwenye Dunia ya filamu kwa kazi zake kali ikiwemo; Eastbound & Down, Good Vibes, The Righteous Gemstones, The Heartbreak Kid, Tropic Thunder, 30 Minutes or Less na nyingine kibao.

Read More
 TIMU YA KAMPEINI YA KANYE WEST YAKIRI KUIBIWA MAELFU YA FEDHA

TIMU YA KAMPEINI YA KANYE WEST YAKIRI KUIBIWA MAELFU YA FEDHA

Timu ya kampeni ya Kanye West imetoa madai ya kuibiwa kiasi kikubwa cha pesa wakati wa kampeni za uchaguzi mkuu wa Marekani mwaka 2020, kwa njia za ulaghai. Kiasi cha pesa kilichoibiwa na mtu ambaye hakuwa kwenye team hiyo ya kampeni ya kanye west kimetajwa ni zaidi ya shilingi laki 4 za Kenya. Fedha hizo zilikuwa zikiibwa kuanzia Disemba mwaka wa 2020 hadi Februari mwaka wa 2021 katika akaunti ya Kanye West iliyopo katika First Bank of  Wyoming. Kanye West ambaye alikuwa akiwania kiti cha urais katika uchaguzi mkuu mwaka wa 2020  nchini Marekani alishindwa lakini hivi karibuni kwenye moja ya mahojiano yake ameahidi kuwania tena kiti hicho cha urais mwaka wa 2024.

Read More
 KANYE WEST AMFANANISHA KIM KARDASHIAN NA KATUNI  MARGE SIMPSON

KANYE WEST AMFANANISHA KIM KARDASHIAN NA KATUNI MARGE SIMPSON

Mwanamama Kim Kardashian amefunguka kwamba baada ya kumalizika kwa Tuzo za Wall Street Journal’s Innovator Awards (WSJ), Kanye West alimuita pembeni na kumwambia kwamba amefanana na katuni “Marge Simpson” ambaye ni mhusika kwenye animation maarufu nchini Marekani, The Simpsons. Kanye West hakuishia hapo, alienda mbali zaidi na kumwambia Kim kuwa amekwisha, jambo ambalo walimwengu kwenye mitandao ya kijamii wamehoji kuwa huenda Kanye ametoa maneno hayo kutokana na namna ambavyo baby mama wake kim amekuwa akivalia kwenye matukio mbali mbali Kauli ya Kim Kardashian imekuja siku chache baada ya kuweka wazi kuwa siku hizi amekuwa akipaniki hasa linapokuja suala la kupangilia mavazi tangu aachane na Kanye West. Kama unakumbuka, Kanye West ndio alikuwa stylist wa Kim Kardashian na mara ya mwisho kumvalisha ilikuwa ni kwenye kipindi cha Saturday Night Live (SNL)

Read More
 KANYE WEST ASHTAKIWA KWA WIZI WA AUDIO

KANYE WEST ASHTAKIWA KWA WIZI WA AUDIO

Rappa kutoka Marekani Kanye West ameripotiwa kushtakiwa na Askofu David Paul Moten kutoka Texas kwa madai ya ku-sample moja kati ya audio ya mahubiri yake na kuitumia katika ngoma yake ya “Come To Life” inayopatikana kwenye album ya Donda bila ya ridhaa yake. Katika nyaraka zilizodakwa na TMZ, Askofu Paul Moten anadai kuwa mahubiri yake yalitumika kwa muda wa sekunde 70 katika ngoma hiyo yenye dakika 5 na sekunde 10, ambayo ni zaidi ya asilimia 20 ya wimbo huo. Askofu David Paul Moten pia amezishtaki , lebo za Universal Music Group, Def Jam pamoja na Good Music katika msala huo, hivyo anadai fidia alipwe na pande zote hizo nne.

Read More
 KANYE WEST NA UNIVERSAL MUSIC GROUP WABURUZWA MAHAKAMANI

KANYE WEST NA UNIVERSAL MUSIC GROUP WABURUZWA MAHAKAMANI

Rapa kutoka Marekani Kanye West pamoja na Universal Music Group wanakabiliwa na kesi ya wimbo wa “Power” alioutoa mwaka 2010. Kwenye wimbo huo, Kanye West alitumia vionjo kutoka kwenye wimbo wa King Crimson “21st Century Schizoid Man,” wa mwaka 1969,. Kwa mujibu wa Variety, Declan Colgan Music Ltd, ambao wanamiliki toleo la awali la wimbo huo, waliwasilisha kesi katika mahakama kuu ya Uingereza mapema mwezi Machi 2022. Madai hayo yanakuja kufuatia Kanye West kuweka wimbo huo kwenye mtandao wa Youtube mwaka 2010 kabla ya kuwepo kwa makubaliano ya awali ya matumizi ya sampuli hiyo ambapo wimbo huo mpaka sasa umepata jumla ya watazamaji takriban milioni 134. Inaelezwa wakati huo Declan Colgan Music Ltd ilimuomba Ye, na kampuni yake ya uzalishaji, Rock the World kutia saini mkataba ambao ulisema sampuli hiyo itapata mrabaha wa 5.33% katika kila sehemu ambayo nakala ya wimbo wa huo itauzwa au kutumiwa kwa namna yeyote. Declan Colgan Music Ltd, sasa inadai kwamba Universal Music Group imeshindwa, na inaendelea kushindwa, kutii wajibu wake wa kihasibu wa mrabaha kuhusiana na masharti sahihi waliyopaswa kuyafuata. Kwa mujibu wa Complex, kwa Sasa wanachotaka Declan Colgan Music Ltd ni mirabaha yao ya Streaming Royalties iwe sawa na mauzo halisi ya CD, badala ya asilimia zinazotolea na majukwaa ya malipo kama Spotify kwa kila stream moja.

Read More
 THE WEEKND ATISHIA KUJIONDOA KWENYE TAMASHA LA COACHELLA

THE WEEKND ATISHIA KUJIONDOA KWENYE TAMASHA LA COACHELLA

Mwanamuziki kutoka Canada The Weeknd ametishia kujiondoa kwenye orodha ya wasanii kinara ambao wametajwa kutumbuiza kwenye tamasha la Coachella. Kwa mujibu wa mtandao wa Page Six, The Weekd amedai kuwa hatotumbuiza kwenye tamasha la Coachella kama atalipwa shillingi billioni za Kenya ambazo Kanye west alipaswa kupewa. Kauli ya the Weeknd inakuja siku chache baada ya kutajwa na kundi la Swedish House Mafia kuwa watatumbuiza kwenye tamasha la Coachella, kuchukua nafasi ya rapa Kanye West ambaye alijiondoa kwenye orodha ya watumbuizaji kinara wa tamasha hilo. Tamasha la Coachella litaanza April 15 hadi 24  mwaka huu nchini Marekani.

Read More
 KANYE WEST AJIONDOA RASMI KWENYE TAMASHA LA COACHELLA

KANYE WEST AJIONDOA RASMI KWENYE TAMASHA LA COACHELLA

Rapa kutoka Marekani Kanye West hatotumbuiza kwenye Tamasha la Coachella mwaka huu. Rapa huyo ameripotiwa kujiondoa kwenye orodha ya watumbuizaji wa tamasha hilo huku akiwa msanii kinara. Wakati mashabiki wakiwa bado na maswali juu ya uamuzi huo wa Kanye West, Rapa Travis Scott naye ambaye angeungana na YE Jukwaani, hatokuwepo kwenye tamasha hilo linaloanza wikendi ijayo huko Indio, California. Bado haijafahamika sababu hasa ya Kanye West kujiondoa, lakini kiuhalisia alikuwa na mwezi mgumu sana, akishambuliana mitandaoni na Kim Kardashian pamoja na Pete Davidson. Lakini pia  sakata lake na Trevor Noah lililomfanya kuondolewa kwenye orodha ya watumbuizaji wa Tuzo za Grammy.

Read More
 KANYE WEST AONDOLEWA KWENYE TUZO ZA GRAMMY

KANYE WEST AONDOLEWA KWENYE TUZO ZA GRAMMY

Rapper kutoka Marekani Kanye West ameondolewa kwenye orodha ya Wasanii waliokuwa wamepangwa kutumbuiza kwenye ugawaji wa Tuzo za Grammy huko Las Vegas wiki mbili zijazo. Msemaji wa Kanye West amesema walipokea simu kutoka kwenye Academy kuwajulisha kuwa rapa huyo ameondolewa kwa sababu inayotajwa kuwa ni kuhusu tabia zake za mtandaoni. Mitandao ya Marekani imeripoti kwamba timu ya Kanye West haikushangazwa na uamuzi huo kutokana na Msanii huyo mwenye msimamo mkali kugonga vichwa vya habari kwa matukio yake ya hivi karibuni kwenye mitandao ya kijamii ambayo yalisababisha hadi akafungiwa akaunti yake ya Instagram kwa kukiuka sera za Mtandao huo. Kanye West ana shutuma za kutumia Instagram yake kuwapiga picha Watu kadhaa maarufu akiwemo Mke wake waliyeachana Kim Kardashian na mpenzi wake mpya Pete Davidson na pia alitumia Instagram yake kumkashifu Trevor Noah kwa kuzungumzia matukio yake kwenye kipindi chake cha The Daily Show.

Read More
 KANYE WEST AWEKWA KWENYE KITABU CHA SOMO LA HISTORIA KWA SHULE ZA NCHINI MAREKANI

KANYE WEST AWEKWA KWENYE KITABU CHA SOMO LA HISTORIA KWA SHULE ZA NCHINI MAREKANI

Rapa kutoka Marekani Kanye West amekuwa mfano na sehemu ya Wanafunzi kujifunza. Rapa huyo ameingia kwenye mtaala wa elimu kwa kuwekwa kwenye Kitabu cha somo la Historia kwa Wanafunzi wa Sekondari nchini Marekani. Kikao chake na aliyekuwa Rais wa Marekani Donald Trump katika Ofisi ya Rais (Oval Office) ndani ya Ikulu ya White House mnamo Oktoba 11, mwaka 2018 kimeingizwa kwenye mtaala wa Somo la Historia kwenye Topic isemayo: US Democracy and Participation.

Read More
 KANYE WEST NA KIM WAMEACHANA RASMI, MCHAKATO WA TALAKA WAKAMILIKA

KANYE WEST NA KIM WAMEACHANA RASMI, MCHAKATO WA TALAKA WAKAMILIKA

Ndoa ya Kim Kardashian na Kanye West imevunjika rasmi baada ya miaka 8. Mchakato wa talaka umekamilika Machi 3 na Jaji wa mahakama ya mjini Los Angeles ametangaza rasmi kwamba Kim Kardashian anaweza kuendelea na maisha yake ya U-single lakini pia ameondoa jina la ‘West’ kwenye majina yake matatu. Tovuti ya TMZ imebaini kwamba hakuna tumaini lolote kwa Kim na Kanye West  kurudiana kwani Kim amepigilia msumari kwenye maandishi kwamba jambo hilo haliwezekani kwa sasa. Kim Kardashian amesema alifanya kila awezalo kuyamaliza na Kanye West tangu afungue shauri la talaka mwezi Februari mwaka 2021 lakini Ye hakuonesha ushirikiano. Ikumbukwe Kim na rapa Kanye West wamedumu kwenye ndoa kwa takriban miaka 7 na amejaliwa watoto wanne ambao ni Psalm, Saint, Chicago na North.

Read More
 DOCUMENTARY KUHUSU MAISHA YA RAPPER KANYE WEST KUZINDULIWA MACHI 2 MWAKA HUU NETFLIX

DOCUMENTARY KUHUSU MAISHA YA RAPPER KANYE WEST KUZINDULIWA MACHI 2 MWAKA HUU NETFLIX

Sehemu ya tatu (3) ya filamu iliyojaa maisha ya Rapa kutoka nchini Marekani Kanye West iitwayo “Jeen-Yuhs” inatarajiwa kuzinduliwa Machi 2, Mwaka wa 2022 katika mtandao wa NetFlix. Filamu hiyo imetengenezwa kwa kuunganisha vipande vya video alizorekodiwa na marafiki zake waliokuwa wanamfatilia kwa takribani miaka 20. Matukio yaliyojumuishwa kwenye filamu hii ni kama kifo cha mama yake, Donda na matatizo yake ya afya ya akili pamoja na mchakato wake wa kugombea uraisi ulivyofeli. Documentary Hiyo Imeandaliwa na Waliokuwa Waongozaji Wa Video  Za nyimbo mbili za Kanye West Jesus Walk na Through The Wire  ambao ni Director Chike Ozah Pamoja na Clarence Simons. Hivyo Documentary ya Jeen-Yuhs Inatarajiwa Kuanza Kuonekana kwenye mtandao wa Netflix Machi 2 mwaka wa 2022.

Read More