KANYE WEST KWENYE PENZI JIPYA NA MWANAMITINDO CHANNEY JONES

KANYE WEST KWENYE PENZI JIPYA NA MWANAMITINDO CHANNEY JONES

Rapper kutoka nchini Marekani Kanye West ametajwa kuwa kwenye mahusiano mapya na mwanamitindo Channey Jones. Tovuti mbalimbali Marekani zinasema kuwa, Kanye West amekuwa katika mahusiano ya siri na mrembo huyo kwa muda sasa. Uvumi wa Mahusiano yao ulianza kuvuma baada ya Kanye West kuonekana na Mwanadada huyo huko Calfornia, nchini Marekani Februari 9 Mwaka huu. Kumbuka ni wiki mbili tu nyuma zimepita tangu mtu mzima Kanye West abwagane na aliyekuwa mpenzi wake Julia Fox.

Read More
 KANYE WEST AWAFUTA KAZI MAFUNDI WA MITAMBO WALIOANDAA ONESHO LAKE LA DONDA 2 EXPERIENCE CONCERT

KANYE WEST AWAFUTA KAZI MAFUNDI WA MITAMBO WALIOANDAA ONESHO LAKE LA DONDA 2 EXPERIENCE CONCERT

Microphone ilimzingua sana rapa Kanye West wakati akitumbuiza Jukwaani,ambapo aliamua kuitupa kwa hasira kwenye maji. Rapa huyo alikuwa akitumbuiza kwenye Onesho la ‘Donda 2 Experience Concert’ lililofanyika februari 23 mjini Miami. Tatizo la microphone kusumbua liliripotiwa na baadhi ya kurasa za mitandao ya Kijamii na wadau waliokuwa wanafuatilia onesho hilo mtandaoni. Hata hivyo Kanye West ameripotiwa kuwafuta kazi kamati yake ya ufundi iliyokuwa ikishughulikia performance yake kwenye ‘Donda 2 Experience Concert’. Ikumbukwe Kanye west alipata nafasi ya kuwasikilizisha mashabiki zake midundo ambayo itapatikana kwenye DONDA 2 album ambapo baadhi ya wasanii walioshirikishwa ni pamoja na; XXXTENTACION, Don Toliver, Baby Keem, Quavo, Offset, Future, Travis Scott, Playboi Carti, Jack Harlow, Sean Leon, Soulja Boy, Fivio Foreign na Alicia Keys. Donda 2 Album tayari imeshatoka ikiwa na jumla ya mikwaju 14 na inapatikana kwenye  jukwaa lake la ‘Strem Player’,  kifaa maalum cha kusikiliza muziki Huu ni muendelezo wa album yake Donda ambayo ilitoka Agosti 29 mwaka 2021.  

Read More
 APPLE WAONDOA UDHAMINI WAO KWA KANYE WEST BAADA YA KUTANGAZA MSIMAMO WAKE KUHUSU ALBUM YA DONDA 2

APPLE WAONDOA UDHAMINI WAO KWA KANYE WEST BAADA YA KUTANGAZA MSIMAMO WAKE KUHUSU ALBUM YA DONDA 2

Kampuni ya Apple imetangaza kuondoa kiasi cha shilling billion 2.3 pamoja na kuondoa udhamini wake kwa Kanye West ambaye mishoni mwa wiki iiliyopita alitangaza rasmi kuwa album yake mpya “DONDA 2” itapatikana kwenye Jukwaa lake la ‘Strem Player’ kifaa maalum cha kusikiliza muziki. Kupitia ukurasa wake wa instagram wiki iiliyopita, Kanye West alifunguka makubwa ikiwemo kuyakandia maduka maarufu ya kuuza muziki mtandaoni ikiwemo Apple, Amazom, Spotify na YouTube akisema kwamba inawanyonya wasanii ambao hupata asilimia 12 pekee kwenye kazi zao. Hivyo ni muda wa wasanii kuanzisha maduka yao ya kuuza muziki. Stem Player, ni kifaa maalum ambacho kitauzwa kwa zaidi ya shilling elfu 19. Kwa mujibu wa The Daily Mail, Kanye West tayari ametengeneza kiasi cha shilling million 154 ikiwa ni ndani ya masaa 12 ya tangazo lake.

Read More
 UHUSIANO WA KANYE WEST NA MPENZI WAKE JULIA FOX WAINGIWA NA UKUNGU, WAMERIPOTIWA KUACHANA

UHUSIANO WA KANYE WEST NA MPENZI WAKE JULIA FOX WAINGIWA NA UKUNGU, WAMERIPOTIWA KUACHANA

Siku ya Valentine’s Day imeenda vibaya kwa rapa Kanye West na mchumba wake Julia Fox. Wawili hao wameripotiwa kuachana rasmi baada ya miezi miwili ya kuwa penzini. Chanzo cha karibu kimeuambia mtandao wa TMZ kwamba YE na Fox wamebaki tu kuwa marafiki na washirika kwenye masuala mengine. Kuisindikiza siku ya Valentine’s, Kanye West amemtumia Kim Kardashian maua ya kutosha kwenye gari lililofika hadi nyumbani kwake. Rapa kanye west Ni kama bado anatamani kurudiana na Baby mama wake kim kardashian Kwa sababu anazidi kuja na matukio mbalimbali kila kukicha.

Read More
 KANYE WEST AMTAKA BILLIE EILISH KUMUOMBA MSAMAHA TRAVIS SCOTT KWA KUMVUNJIA HESHIMA

KANYE WEST AMTAKA BILLIE EILISH KUMUOMBA MSAMAHA TRAVIS SCOTT KWA KUMVUNJIA HESHIMA

Rapa Kanye West ameonesha mahaba kwa rafiki yake wa karibu kabisa Travis Scott, kwani ametishia ujiondoa kwenye tamasha la Coachella mpaka pale mwanamuziki mwenzake Billie Eilish atakapomuomba msamaha travis scott kwa kum-diss kwenye moja ya tamasha lake alilofanya wikendi iliyopita. Billie Eilish alim-diss Travis Scott kwenye tamasha lake akidai kuwa yeye huwa anasitisha show kama mashabiki wakiwa katika hali mbaya. Kauli ambayo ilitajwa kumlenga rapper Travis Scott ambaye aliripotiwa kushindwa kusitisha tamasha lake la Astro-World festival baada ya baadhi ya mashabiki kufariki na wengine kujeruhiwa vibaya mwaka wa 2021. Hata hivyo Billie Eilish  ameibuka na kukanusha taarifa hizo kwa kusema kwamba hakuwa na nia ya kum-diss Travis Scott kama inavyotafsiriwa ila alikuwa anatoa msaada tu kwa shabiki.

Read More
 RAPA KANYE WEST AMRUDIA MUNGU KUINUSURU FAMILIA YAKE AMBAYO IMESAMBARATIKA

RAPA KANYE WEST AMRUDIA MUNGU KUINUSURU FAMILIA YAKE AMBAYO IMESAMBARATIKA

Rapa Kanye West ni kama bado anatamani kurudiana na baby mama wake Kim Kardashian kwa sababu anazidi kuja na matukio mbalimbali kila kukicha. Sasa kupitia ukurasa wake wa Instagram rapa huyo ameshare picha ya watoto wake wakiwa pamoja na mama yao, Kim Kardashian na kuandika kuwa mungu asaidie familia yake irudi kuwa pamoja. Baada ya Kanye West kuonesha kuwa bado anatamani familia yake irudi kama zamani, mpenzi wa sasa wa Kanye West, Julia Fox anasema hana wasiwasi kwa sababu anachojua kwa sasa Kanye West ni wa kwake na anajua kuwa bado ana mabaki ya hisia kwa mrembo Kim kardashian ila yeye anachukulia ni hali ya kibinadamu kumkumbuka ulietengana nae. Siku kadhaa zilizopita tuliona kupitia mitandao ya kijamii kanye west akimchana baby mama wake Kim kwa mambo mbalimbali ikiwemo kumuunganisha mtoto wao North West kwenye mtandao wa Tiktok bila idhini yake.  

Read More
 KANYE WEST NA KIM KARDASHIAN WARUSHIANA MANENO MAKALI KWENYE MTANDAO WA INSTAGRAM

KANYE WEST NA KIM KARDASHIAN WARUSHIANA MANENO MAKALI KWENYE MTANDAO WA INSTAGRAM

Rapa kutoka Marekani Kanye West ameonesha kutokupendezwa na kitendo cha Mwanae wa kike North West aliyezaa na mrembo Kim Kardashian kujiunga katika mtandao wa TikTok. Kupitia instagram page yake Kanye West ameibuka na kuomba ushauri ni kitu gani afanye juu ya hili la mwanae kuungwa kwenye mtandao huo maarufu wa TikTok “Hii Ni Talaka Yangu Ya Kwanza, Nahitaji Kufahamu Ni Kipi Nifanye Kuhusu Mwanangu Kuunganishwa Katika Mtandao Wa Tiktok Kinyume Na Mapendekezo Yangu” Baada ya Kanye West kuhoji na kuomba ushauri nini afanye baada ya mwanae kuwepo kwenye mtandao maarufu wa TIKTOK sasa mama wa North ambaye ni Kim Kardashian ameamua kumjibu Kanye West juu ya hilo. Kupitia Insta story ya Kim Kardashian amemjibu kudai kuwa Kanye West anawaumiza watoto kwa kuleta tofauti zao kwenye mitandao ya kijamii. “Mashambulizi ya Kanye West juu yangu kwenye vyombo vya habari na mitandao ya kijamii ni mabaya na yanaumiza zaidi kuliko mtoto kutumia mtandao wa TikTok. “Kama Mzazi na Muangalizi wa Mtoto wetu , nahakikisha nampa malezi bora huku nikimpa uhuru wa kuonyesha Vipaji Vyake Mbalimbali alivyonavyo . Talaka ni kitu kibaya kwa watoto wetu , Lakini vitendo vya Kanye West Kutoka kutuendesha vinaongeza maumivu zaidi kwenye Maisha yetu ” Hata hivyo bado Rapa Kanye West amelishikilia swala la Mwanae North kuwepo kwenye mtandao wa TikTok ambapo ameweka Taratibu na Sheria za kujiunga na mtandao huo. YE ameweka maelezo ya kujiunga na mtandao huo ambapo moja ya sheria ni mtoto mwenye umri wa miaka 13 na kushuka chini inabidi ajisajili kwa umri wake ili apate kuona maudhui yanayomfaa tu.

Read More
 DRAKE ALIPITA NA MREMBO JULIA FOX KABLA YA KANYE WEST

DRAKE ALIPITA NA MREMBO JULIA FOX KABLA YA KANYE WEST

Kumbe Rapa Kanye West kutoka nchini Marekani amepita sehemu ambayo rapa mwenzake Drake alipita kitambo. Taarifa mpya mjini zinadai kwamba Drake aliwahi kuwa na mahusiano na mrembo Julia Fox ambaye kwa sasa yupo penzini na Kanye West. Kwa mujibu wa tovuti ya Page Six, penzi lao lilianza mwaka 2020 kufuatia ukaribu ulioanza mwaka 2019 baada ya Drizzy kumtelezea DM mrembo huyo na kumsifia kuhusu ushiriki wake kwenye filamu ya Uncut Gems. Julia Fox aliachana na mumewe Artemiev na Drake ndiye akawa tulizo lake la muda mfupi. Kumbuka kuwa kipindi cha nyuma kabla ya wawili hawa kuzika tofauti zao walikuwa kwenye bifu zito huku sababu kubwa ikitajwa kuwa Drake aliwahi kusema kuwa yupo kwenye mahusiano na Ex wa rapa Kanye West ambaye ni Kim Kardashian na kwa kuthibitisha hilo alim-follow Instagram pamoja na kutoa ngoma yake ya “In My Feeling” akimuimba “Kiki” ambalo ni jina lingine la mrembo huyo.

Read More
 KIM KARDASHIAN AKANUSHA TAARIFA ZILIZOTOLEWA NA KANYE WEST KUHUSU UWEPO WA SEXTAPE YAKE NA RAY J

KIM KARDASHIAN AKANUSHA TAARIFA ZILIZOTOLEWA NA KANYE WEST KUHUSU UWEPO WA SEXTAPE YAKE NA RAY J

Kanye West ameiambia Hollywood Unlocked kwamba alifanikiwa kuupata mkanda wa ngono kutoka kwa Ray J, ikiwa ni sehemu ya pili ya ule ambao ulivuja mwaka 2007 ukimuonesha Ray J na Kim Kardashian wakifanya mapenzi. Kwenye mahojiano ambayo ameyafanya na Hollywood Unlocked, YE amesema Kim alitokwa na machozi baada ya kufikishiwa mkanda huo. “Nilikwenda na kuchukua laptop mwenyewe kwa Ray J, na nilimpatia Kim Kardashian kwenye saa mbili asubuhi. Alilia sana baada ya kuona Laptop, unajua kwanini? Ni kwa sababu iliwakilisha namna gani watu walikuwa wanamtumia na kumchukulia kama bidhaa” alisema YE kwenye mahojiano hayo. Wack 100 aliyekuwa meneja wa Ray J ndiye alitusanua uwepo wa sehemu ya pili ya mkanda huo wa ngono. Masaa machache baada ya kutoka taarifa hiyo, upande wa Kim Kardashian umeibuka na kukanusha taarifa hiyo ikisema hakukuwa na maudhui yoyote ya ngono na hakuna sehemu ya pili ya mkanda huo. Aidha kwenye laptop hiyo kulikutwa video za Kim na Ray J wakiwa kwenye ndege wakielekea nchini Mexico na zingine wakiwa kwenye kumbi za starehe na migawaha.

Read More
 KANYE WEST NA BIG SEAN WAZIKA TOFAUTI ZAO BAADA YA KUWA KWENYE BIFU KWA MUDA

KANYE WEST NA BIG SEAN WAZIKA TOFAUTI ZAO BAADA YA KUWA KWENYE BIFU KWA MUDA

Rapa Kanye West na Big Sean wamemaliza tofauti zao, wameonekana wakiingia studio pamoja. Kwenye picha zinazotembea kwenye mitadao ya kijamii wameonekana pia French Montana, Pusha T, Pressa, Fivio Foreign and The Game. Tetesi zinadai kwamba Kanye west yupo kwenye maandalizi ya album yake ijayo ‘Donda 2’ na huwenda sauti za wakali hao zikasikika kwenye album hiyo. Big Sean na Kanye west waliingia kwenye vita ya maneno mwishoni mwa mwaka jana, hii ni baada ya Kanye west kusema kuwa miongoni mwa vitu ambavyo anajutia kwenye maisha yake ni kumsaini Big Sean. Baada ya kuruka interview hiyo ambayo Kanye west alifanya kwenye Podcast ya ‘Drink Champs’ Big Sean aliomba kukaa kwenye kiti hicho pia na kumjibu Kanye west kwa kusema yote aliyozungumza ni upuuzi mtupu japo heshima yake kwake haiwezi kupotea. Big Sean ambaye aliondoka GOOD Music na kuanzisha label yake,  anamdai Kanye zaidi ya shilling million 147 za Kenya.

Read More
 AMBER ROSE AFUNGUKA KUHUSU TWEET YAKE  YA MWAKA 2015 INAYOONEKANA KUMPONZA EX WAKE KANYE WEST

AMBER ROSE AFUNGUKA KUHUSU TWEET YAKE YA MWAKA 2015 INAYOONEKANA KUMPONZA EX WAKE KANYE WEST

Mwanamitindo kutoka Marekani, Amber Rose amevunja kimya chake kuhusu sakata linaloizingira ndoa ya  Kim Kardashian na Kanye West baada ya watu kumkumbusha tweet yake ya zamani aliyomponda Kanye West. Tweet hiyo aliyoipost mwaka 2015 baada ya kuachana na Kanye West ilisomeka  “Kanye West, nitawaachia ‘Kartrashians’ wakudhalilishe pale ambapo watakuwa wamemalizana na wewe.” Hiyo ilikuwa baada ya Kanye West kufanya mahojiano na kituo cha break fast club na kusema kuwa ilimbidi aoge mara 30 kabla ya kukutana na familia ya The Kardashians kutokana na uchafu wa aliyekuwa Ex wake Amber Rose. Baada ya mashabiki kumkumbusha tweet yake hiyo katika hali ya kumbeza Kanye West ambaye amekuwa akipitia wakati mgumu kutoka kwa familia ya Kim, Amber Rose ameibuka na kusema tweet hiyo ilikuwa ni ya zamani na kwa sasa alishajifunza kutokana na makosa yake, hivyo hawezi kuingilia maisha ya familia yeyote na The Kardashians hawakutakiwa kuambiwa maneno kama yale. Utakumbuka Amber rose na Kanye west walikuwa kwenye mahusiano kati ya  mwaka 2008 na 2010 lakini walikuja wakaachana baada kanye west kuingia kwenye mahusiano na baby mama wake kim kardashian

Read More