KANYE WEST AWEKEWA VIKWAZO KUINGIA KWENYE BIRTHDAY  PARTY YA BINTI YAKE, CHICAGO WEST

KANYE WEST AWEKEWA VIKWAZO KUINGIA KWENYE BIRTHDAY PARTY YA BINTI YAKE, CHICAGO WEST

Kanye West ameamua kuanika wazi kila kitu ambacho kinaendelea baina yake na Kim Kardashian, usiku wa kuamkia leo ameeleza namna ambavyo aliwekewa vikwazo kuingia kwenye birthday party ya binti yake, Chicago West. YE anadai kwamba hakupewa kabisa location ya wapi party hiyo itafanyika,ila juhudi za Travis Scott zilisaidia kwani alimtumia location na alifika eneo hilo ambapo kulikuwa na party pia ya Stormi Webster. Stori kubwa ni kwamba baada ya kufika, walinzi wa Kim Kardashian walimzuia YE kuingia ndani ya party hiyo kitendo ambacho kilimkasirisha sana. Shukrani kwa Kylie Jenner kwani alimpambania hadi akafanikiwa kuingia na kufurahi pamoja na binti yake. Kwenye video ambayo anaonekana akizungumzia sakata hilo, YE anasema Kim anatengeneza mazingira watoto wake wamuone kama baba asiyejali. Hata hivyo sakata la Kanye kuzuiwa kuwa karibu na watoto wake halijaanza jana, kwenye mahojiano na Hollywood Unlocked, Kanye West alisema Jumatatu iliyopita aliwafata watoto wake shule ili kuwapeleka nyumbani, alipofika shuleni walinzi wa Kim Kardashian walimzuia getini. Hakubishana nao, siku nyingine alifanikiwa na kuwafikisha hadi nyumbani na North alimtaka aingie ndani lakini walinzi walimzuia, inadaiwa kuwa Pete Davidson ambaye ni mpenzi mpya wa Kim, alikuwepo ndani.

Read More
 KANYE WEST ADAIWA KUMPIGA SHABIKI NGUMI, AANGUKA CHINI VIBAYA

KANYE WEST ADAIWA KUMPIGA SHABIKI NGUMI, AANGUKA CHINI VIBAYA

Januari 13 mwaka huu haikuwa siku nzuri kwa Kanye West, alionekana mtu mwenye hasira sana. Taarifa zinasema kwamba hakutaka kusogelewa na mtu yeyote yule kwa ajili ya kupiga picha wakati anashuka chini ya jengo la studio, Los Angeles. YE alimaanisha, aliishia kumtwanga ngumi mbili jamaa mmoja ambaye alimfuata kupiga picha, ngumi ya kichwa na kisha ya shingo vilitosha kumuangusha chini shabiki huyo ambaye alibamiza kichwa chini baada ya kuanguka na kulala hapo hapo. Kwenye video anaonekana Kanye West akizozana na binamu yake huku akimwambia “get away from me” Kanye alionekana mwenye hasira huku binamu yake akimsisitiza waite polisi kwa ajili ya kumuangalia shabiki yule.

Read More
 KANYE WEST KUIPELEKA SUNDAY SERVICE NCHINI URUSI,APANGA KUKUTANA NA RAIS VLADIMIR PUTIN.

KANYE WEST KUIPELEKA SUNDAY SERVICE NCHINI URUSI,APANGA KUKUTANA NA RAIS VLADIMIR PUTIN.

Rapa kutoka Marekani Kanye West ana mpango wa kuipeleka Sunday Service nchini Urusi kwa mara ya kwanza. Mtu wake wa karibu ameiambia tovuti ya Billboard kwamba YE amepanga kukutana na Rais Vladimir Putin kwa ajili ya mazungumzo. Kwa mujibu wa Billboard Kanye West anataka kuweka makazi yake ya pili nchini Urusi pamoja na kuanzisha miradi mbalimbali ya kibiashara. Ikumbukwe Sunday Service ni huduma ya kiroho ambayo huongozwa na rapa Kanye West ambapo hubadilisha nyimbo za kidunia kuwa nyimbo za kumsifu Mungu.

Read More
 KANYE WEST ANUNUA MJENGO KARIBU NA NYUMBA YA KIM KARDASHIAN

KANYE WEST ANUNUA MJENGO KARIBU NA NYUMBA YA KIM KARDASHIAN

Staa wa muziki wa Hiphop kutoka nchini Marekani Kanye West ni kama amekubali yaishe kuhusu sakata la talaka na Kim Kardashian, ameona hawezi kumrudisha na sasa ameamua kumsogelea karibu ili apate nafasi ya kushirikiana naye kwenye malezi ya watoto wao. Tovuti ya Daily Mail imeripoti kwamba Kanye West amenunua nyumba yenye thamani ya dolla millioni 4.5 ambayo ni takribani shillingi millioni 508 kwa pesa za Kenya iliyopo kando ya mtaa ambao anaishi Kim Kardashian na watoto wake. Nyumba hiyo ipo kwenye eneo la mita za mraba 3,650 ikiwa na vyumba 5 vya kulala. Kanye West na Kim Kardashian ni wazazi wa watoto wanne ambao ni; North, Saint, Chicago, na Psalm, kwasasa hawako pamoja huku sakata la talaka likienda mahakamani. Hata hivyo tayari Kim Kardashian yupo kwenye mahusiano mapya na mchekeshaji Pete Davidson, uhusiano uliowekwa wazi hivi karibuni.

Read More
 KANYE WEST ANA MPANGO WA KUBADILISHA NYUMBA ZAKE ZOTE KUWA MAKANISA

KANYE WEST ANA MPANGO WA KUBADILISHA NYUMBA ZAKE ZOTE KUWA MAKANISA

Staa wa muziki wa hiphop nchini Marekani Kanye West anaenda kuwa mtu asiye na makazi, ametangaza mpango wake wa kubadilisha nyumba zake zote kuwa Makanisa. YE amefunguka hayo kwenye mahojiano na Jarida la Culture Magazine ambapo anukuliwa akisema “Nitageuza nyumba zangu zote kuwa makanisa pamoja na kutengeneza kituo cha watoto yatima ambacho kutakuwa eneo ambalo mtu yoyote ataweza kupata mahitaji yake ya muhimu na chakula kitakuepo muda wowote”. Ikumbukwe Kanye West amekuwa akiongoza huduma ya Sunday Service, huduma ya kiroho ambayo hubadilisha nyimbo za kidunia kuwa nyimbo za kumsifu Mungu.

Read More
 BIG SEAN AMJIBU KANYE WEST,ADAI ALICHOKISEMA KWENYE MAHOJIANO NA DRINKS CHAMPS NI UJINGA

BIG SEAN AMJIBU KANYE WEST,ADAI ALICHOKISEMA KWENYE MAHOJIANO NA DRINKS CHAMPS NI UJINGA

Rapa kutoka nchini marekani Big Sean amesema anampenda sana Kanye West na anampa heshima zote kwa upendo aliomuonesha kumshika mkono hadi kufahamika, lakini kwa alichokisema kwenye mahojiano na Drink Champs mwezi Novemba mwaka huu ni ujinga mtupu. Big Sean amekuwa mgeni mpya wa Drink Champs, kipindi ambacho kitaruka Jumamosi hii, Sean amesikika akisema “Nampenda Kanye. Nampenda kwa nafasi aliyonipatia na kila kitu. Lakini nafikiri alichokisema kilikuwa ni upuuzi na ujinga mtupu.” amesema Big Sean. Kanye West aliingia kwenye headlines baada ya kusema kwamba miongoni mwa vitu ambavyo anajutia kwenye maisha yake ni kumsaini rapa Big Sean kwenye label yake, GOOD Music.

Read More
 KIM KARDASHIAN ASHINDA KIPENGELE CHA UMILIKI WA NYUMBA KWENYE SHAURI LA TALAKA

KIM KARDASHIAN ASHINDA KIPENGELE CHA UMILIKI WA NYUMBA KWENYE SHAURI LA TALAKA

Mahakama ya mjini Los angeles nchini marekani imempatia ushindi Kim Kardashian wa umiliki wa nyumba kwenye shauri la talaka linaloendelea dhidi yaKkanye West. Kim ameshinda kipengele hicho na sasa ni mmiliki wa nyumba ambayo walianzia maisha na Kanye West na kuanzisha familia pamoja. Jumba hilo lenye thamani ya shilling billion 6.7  lipo mjini Hidden Hills California, mwaka wa 2014 walilinunua pamoja kwa shilling billioni 2.6 kisha baadaye mwaka wa 2020 Kanye West aliikarabati. Hii imekuja kufuatia mustakabali wa watoto wao ambao wamezoea kuishi mahali hapo. Taarifa hii imekuja ikiwa ni siku chache tangu kanye west aiweke kwenye mnada moja ya ranchi zake zilizopo huko Wyoming nchini kwa shilling billioni 1.2. Mwezi uliopita  Kanye West pia aliripotiwa kununua jumba la kifahari kwenye fukwe za malibu huko marekani kwa shilling billioni 6.3.

Read More