RAPPER KHALIGRAPH JONES MBIONI KUACHIA WIMBO WA INJILI

RAPPER KHALIGRAPH JONES MBIONI KUACHIA WIMBO WA INJILI

Rapper mnoma kwa michuano kutoka Kenya Khaligraph Jones huenda akageukia muziki wa injili baada ya kushare video clip ikimuonesha akiimba na kutayarisha wimbo wa dini. Hata hivyo rapper huyo ambaye amewahi kutamba na hitSong kama “Mazishi, Leave Me Alone, na Yes bana”  anatajwa kulelewa kwenye misingi thabiti ya dini ya Kikristo na mpaka sasa mama yake ni mhubiri. Kwenye moja ya mahojiano yake Khaligraph Jones amewahi kuthibitisha kuwa Mwaka 2004, alikuwa na matarajio ya kuwa mwimbaji wa nyimbo za injili, lakini yote yalibadilika mara baada ya kugundua uwezo wake wa kurap mwaka huo alirekodi wimbo wake wa kwanza pamoja na Hope Kid na walianzisha kikundi. “Nilitaka kufanya kitu ambacho nilitaka kufanya na sio kufanya kwa sababu ya ushawishi. Nilitaka kujitengenezea njia yangu.Wakati huo nilikotoka, kila mtu ambaye alikuwa msanii alikuwa anafanya injili, lakini sikuwa na raha”  alisema Khaligraph Jones.

Read More
 KHALIGRAPH JONES ASHINDWA KUFICHA UPENDO WAKE KWA KRISTOFF, AMTAKA RAPA HUYO ARUDI KWENYE MUZIKI

KHALIGRAPH JONES ASHINDWA KUFICHA UPENDO WAKE KWA KRISTOFF, AMTAKA RAPA HUYO ARUDI KWENYE MUZIKI

Rapa Khaligraph Jones ameshindwa kuvumlia ukimya  wa rapa mwenzake Kristoff ambaye amepotea kwenye tasnia ya muziki nchini kwa muda sasa bila kuachia kazi yeyote. Kupitia Instagram page yake Papa Jones amepost clip fupi ya rapa huyo akichana kwenye wimbo wa “We be happening remix” na kusema kwamba ameshangazwa na kilichomsibu Kristoff akapotea ghafla kwenye muziki wake kwani alikuwa mmoja wa marapa wakali nchini. Hitmaker huyo wa “Champez” ametoa changamoto kwa Kristoff ajikakamua mwaka huu ili aweze kurudi kwenye tasnia ya muziki nchini ikizingatiwa  bado mashabiki wanamhitaji kutokana na kipaji chake cha kurap kwenye muziki wa hihop. Hata hivyo mastaa wengi wa muziki nchini na mashabiki wameonekana kumuunga mkono khaligraph jones wakimtaka kristoff arudi kwenye muziki wa hiphop kwani ana uwezo mkubwa wa kuupeleka muziki wake kimataifa. Hajabainika sababu zilizompelekea khaligraph jones kumpost kristoff ila walimwengu wanahoji kuwa huenda wawili hao wana wimbo wa pamoja ambao wana mpango wa kuuachia hivi karibuni. Ikumbukwe kipindi cha nyuma wawili hao waliachia ngoma kali kama We be happening, Biashara wakiwa na Stella Mwangi, Fly na nyingine kibao

Read More
 ALBAMU MPYA KHALIGRAPH JONES INVISIBLE CURRENCY KUTOKA MUDA WOWOTE KUTOKA SASA

ALBAMU MPYA KHALIGRAPH JONES INVISIBLE CURRENCY KUTOKA MUDA WOWOTE KUTOKA SASA

Mkali wa muziki wa Hiphop nchini Khalighraph Jones yupo tayari kuiboresha playlist yako hivi karibuni, Kwa mujibu wa Papa Jones anasema albamu yake mpya kutoka studio “Invisible Currency” itaingia sokoni mwezi huu wa Januari. Khalighraph Jones ametoa taarifa hiyo kupitia ukurasa wake wa instagram ambapo ameandika ” Happy New year Everybody, 2022 we elevate, now I can finally drop Invisible Currency #respecttheogs ” hii ina maana muda wowote tunaweza kuipokea albam hiyo kutoka kwa rapa huyo. Tayari Papa Jones tayari ameachia rasmi orodha ya nyimbo zitakazopatikana kwenye album yake mpya ya ambayo ina jumla ya nyimbo 17 huku ikiwa na collabo 10 pekee. Hitmaker huyo wa “Luku” amewapa mashavu wakali kama Alikiba, Rude Boy, Dax, Mejja, Scar, Adasa na wengine wengi. Invisible Currency  itakuwa album ya pili kwa mtu mzima Khaligraph Jones  baada ya “Testimony 1990” ya  mwaka 2018 iliyokuwa na jumla ya ngoma 17.

Read More
 KHALIGRAPH JONES AGOMA KUTOA MATUMIZI KWA MTOTO WAKE

KHALIGRAPH JONES AGOMA KUTOA MATUMIZI KWA MTOTO WAKE

Aliyekuwa mpenzi wa msanii Khaligraph Jones,Cashy ameshambulia mwanamuziki huyo akidai kuwa amhudumii mtoto wake wa kiume aliyezaa naye mwaka wa 2018 pindi tu walipoachana. Cashy ameshukuru kufunguliwa kwa nchi ambapo amesema kuwa itakuwa afueni kwa wasanii kupata angalau matamasha ya kuwaingizia pesa kwani wengi wao walikuwa wanategemea matamasha kupata riziki. Kutokana na hilo amesema Papa Jones hatakuwa na sababu zingine za kuepuka majukumu ya kumlea mwanawe mwenye umri wa miaka mitatu kwa sasa ikizingatiwa kuwa tangu ujio wa Corona rapa huyo amekuwa akidai kuwa hakuwa na pesa za kumhudumia mwanae. Hata hivyo khalighraph jones hajetoa tamko kuhusiana na madai yaliyoibuliwa na baby mama wake kuwa amemtelekeza mtoto wake

Read More
 KHALIGRAPH JONES AFUNGUKA KUWAHI KUTAKA KUACHA MUZIKI.

KHALIGRAPH JONES AFUNGUKA KUWAHI KUTAKA KUACHA MUZIKI.

Rapa Khaligraph Jones ametusanua kuhusu changamoto alizokutana  nazo katika safari yake ya muziki ambayo ilimpelekea kutaka kuchukua maamuzi magumu kwenye maisha yake. Kupitia ukurasa wake wa instagram amepost picha akiwa jukwaani katika chuo kikuu cha St. Pauls limuru mwaka wa 2012 na kusema kwamba mashabiki waliikata perfomance yake na kumtimua jukwaani jambo ambalo lilimfanya kufikiria kuacha muziki. Lakini baada ya kujitafakari upya na kuweka bidii kwenye kazi zake za muziki aliweza kuwaaminisha watu waliombeza kipindi hicho kwamba anaweza kwenye tasnia ya muziki nchini. Khalighraph jones ni moja kati ya marapa maarufu barani afrika na licha ya kutimuliwa jukwanii mwaka wa 2012 nchini Kenya ametumbuiza kwenye majukwaa makubwa ya muziki duniani lakini pia ameshinda tuzo kadhaa za muziki ikiwemo B.E.T na Sound city Africa.

Read More